KILIMO_BIASHARA_NA_UJASIRIAMALI Flipbook PDF


81 downloads 120 Views 1MB Size

Recommend Stories


Porque. PDF Created with deskpdf PDF Writer - Trial ::
Porque tu hogar empieza desde adentro. www.avilainteriores.com PDF Created with deskPDF PDF Writer - Trial :: http://www.docudesk.com Avila Interi

EMPRESAS HEADHUNTERS CHILE PDF
Get Instant Access to eBook Empresas Headhunters Chile PDF at Our Huge Library EMPRESAS HEADHUNTERS CHILE PDF ==> Download: EMPRESAS HEADHUNTERS CHIL

Story Transcript

KILIMO BIASHARA NA UJASIRIAMALI

Philipo F. Mrutu

Philipo F. Mrutu E-mail: [email protected] SIMU: +255 753 442 903/ 0629159492

Hakuna sehemu yoyote ya kitabu hiki ambayo inaruhusiwa kutolewa upya au kuhamishwa kielektroniki au ufundi wowote wa kurekodi au kufungua na kutoa nakala upya na kurudishia tena bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa mwandishi.

© Novemba 2017 Kimechapwa na Beanna Printing Solutions [email protected] +255766 770 422, +255713 360 853

ii

YALIYOMO UTANGULIZI ................................................................................................ 1 VIFUPI ............................................................................................................ 3 SHUKRANI..................................................................................................... 4 SURA YA KWANZA ...................................................................................... 5 KILIMO-BIASHARA...................................................................................... 5 Biashara ........................................................................................................ 5 Ujasiriamali sasa ni nini? ............................................................................... 6 FAIDA ZA KILIMO-BIASHARA............................................................... 7 KAZI YA KILIMO TANZANIA. ............................................................... 9 CHANGAMOTO ZA KILIMO BIASHARA. .......................................... 10 SURA YA PILI .............................................................................................. 12 MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIKA KWENYE KILIMO-BIASHARA NA UJASIRIAMALI KATIKA KILIMO...................................................... 12 MAZINGIRA NA HALI YA HEWA........................................................ 13 KUONGEZA THAMANI (VALUE ADDITION) ................................... 13 BEI YA MAZAO. ...................................................................................... 13 MUDA (Timing) ........................................................................................ 14 MNYORORO WA THAMANI (VALUE CHAIN) ................................. 15 FURSA ZILIZOPO KWENYE KILIMO BIASHARA. ........................... 16 KILIMO CHA MAHINDI ........................................................................ 17 KUANDAA SHAMBA, KUPANDA NA KUPALILIA ........................... 17 KUDHIBITI MAGONJWA NA WADUDU WANAOSHAMBULIA MAHINDI ................................................................................................. 21 KILIMO BORA CHA MAHARAGE ....................................................... 23

iii

KILIMO CHA KOROSHO ...................................................................... 25 KILIMO CHA PAPAI ............................................................................... 26 UCHANGANYAJI WA VYAKULA VYA WANYAMA NA MIFUGO. 29 UFUGAJI WA SAMAKI ........................................................................... 32 KILIMO ENDELEVU (MAZINGIRA /MSETO) .................................... 39 Benki za Maendeleo ................................................................................... 42 3.0 HITIMISHO ....................................................................................... 45 Vigezo vya kupata mkopo Benki ya CRDB ..................................................... 46 KILIMO CHA MAZAO YA NAFAKA .................................................... 47 KILIMO CHA MAZAO YA BIASHARA ................................................ 47 KILIMO CHA MBOGAMBOGA NA MATUNDA ................................ 48 UFUGAJI ................................................................................................... 49 SURA YA TATU ........................................................................................... 51 NAMNA YA KUFANIKIWA KUFANYA BIASHARA YA KILIMO AU UJASIRIAMALI BILA MTAJI WA KIFEDHA. .......................................... 51 SURA YA NNE ............................................................................................. 53 UJASIRIAMALI KWA UJUMLA NA KILIMO CHA KISASA .................. 53 SIFA ZA MJASIAMALI ............................................................................ 54 MTAJI KATIKA UWEKEZAJI. ............................................................... 54 KILIMO CHA KISASA. ........................................................................... 55 MAMBO YA KUZINGATIA ................................................................... 55 SURA YA TANO .......................................................................................... 59 MCHANGO WA SERIKALI KUINUA UCHUMI WA MKULIMA, BIASHARA NA UJASIRIAMALI. ............................................................... 59 SURA YA SITA ............................................................................................. 61 MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA KILIMO................ 61 KILIMO FORUM. .................................................................................... 62

iv

SURA YA SABA ............................................................................................ 63 USHAURI WA KITAALAMU KWA UJUMLA KUHUSU KILIMO UCHUMI NA BIASHARA............................................................................................. 63 SURA YA NANE........................................................................................... 66 UHUSIANO KATI YA KILIMO NA VIWANDA KWA NCHI KAMA TANZANIA................................................................................................... 66 Mambo ya kufanya kuboresha kilimo nchini Tanzania. .............................. 67 SURA YA TISA ............................................................................................. 69 UTAFITI ....................................................................................................... 69 Utafiti wa ngombe wa Kisasa na Nguruwe ................................................... 70 MAMBO YA KUZINGATIA KWENYE UCHAGUZI WA NG'OMBE MZURI WA MAZIWA ............................................................................. 72 AINA ZA NG'OMBE WA MAZIWA NA SIFA ZAKE ........................... 72 UKUZAJI WA MICHE YA MITI YA MATUNDA. ............................... 74 UFUGAJI WA NGURUWE ..................................................................... 76 AINA ZA NGURUWE ............................................................................. 79 MASWALI MUHIMU KWA MSOMAJI WA KITABU HIKI: .............. 81 MAREJEO/Reference .................................................................................... 83

v

UTANGULIZI Kitabu hiki kinatoa elimu ya Kilimo Biashara yaani namna, mbinu na njia za kufwata ili kulima au kufuga kwa tija na faida na kuachana na kilimo cha mazoea. Pia kitabu hiki kimeelezea ujasiriamali kwa ujumla. Kufanikiwa katika jambo lolote ni kanuni. Hivyo basi hata kwenye Kilimo Biashara, zipo mbinu ambazo mtu akizifwata anafanikiwa na kuepuka hasara zisizo za lazima. Katika kuvumbua kuwa kilimo ni fursa, likaja wazo hili la kuandika kitabu kizuri chenye msaada kwa vijana, wasomi, wakulima, wajasiriamali na wadau wengine wanaopenda kufanikiwa katika biashara zao. Kilimo kina mchango mkubwa sana katika uchumi wa taifa na wananchi wa mataifa mbalimbali kwakuwa ajira nyingi za rasmi na zisizo rasmi hupatikana kwenye sekta hii muhimu ya Kilimo. Pia fedha za kigeni zinapatikana kutokana na kuuza nje ya nchi, kwa mfano bidhaa nyingi zinazo uzwa nje ya nchi ni pamoja na bidhaa kama Tumbaku, Kahawa, Pamba, Korosho, Chai na Karafuu ambazo hutokana na Kilimo nchini Tanzania.

1

2

VIFUPI ADRI- Animal Disease Research Institute ARI -Agricultural Research Institute (UKIRIGURU) MARI -Mikocheni Agricultural Research Institute SAEBs- School of Agricultural Economics and Business Studies SUA- Sokoine University of Agriculture TADB- Tanzania Agricultural Development Bank TBS -Tanzania Bureau Of Standards TIEDF- Tanzania Institutional Economics Development Foundation TORITA -Tobacco Research Institute Of Tanzania TPRI-Tropical Pesticides Research Institute TRIT -Tea Research Institute Maruku YUNA-Youth of United Nations Association of Tanzania

3

SHUKRANI Kabla ya yote, napenda nimshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuandika kitabu hiki kilicho sheheni maarifa hasa juu ya kilimo biashara na ujasiriamali, na kutoa majibu ya maswali ya wengi juu ya namna ya kufanikiwa kwenye kilimo, biashara na uchumi kwa ujumla. Nakiri kuwa, hata sasa Bwana amenisaidia, kuweza kuandika kitabu hiki, wazo la muda wa takribanimiaka mitatu hadi kukamilisha uandishi. Kipekee napenda niwashukuru watu walio gusa sana maisha yangu kuweza kufikia ndoto na malengo yangu. Ni watu wengi sana walio na wanao gusa maisha yangu, hata hivyo nisinge weza kuwa taja wote. Nitawashukuru kwa makundi, wazazi wangu, waalimu wangu, wanafunzi tulio soma pamoja, ndugu, jamaa pamoja na marafiki wote. Mzee Fahamuel I. Mrutu (Baba mzazi), mama Nietiwe Fahamuel Mrutu, kaka zangu wote Stanley, Loti, Ezekiel, Eriki na dada zangu Edina, Tabea, Yuliana na Penina. Pia napenda kuwataja baadhi ya ndugu wa karibu kama, Baba wadogo Mkichumbi, Thomas, Vamba, Kathbety, Rajabu, Mahuzu, Eliyuko, Kidala na wengine wote. Bila kuwasahau shemeji zangu wote, wajomba, shangazi, na wote walio nilea hadi kuweza kufika nilipo.Kundi linguine ni la muhimu sana, ni waalimu wote walio nifundisha kuanzia darasa la kwanza shule ya primary Kweresha, Chanjagaa Sekondari, Lyamungo sekondari na Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA). Mathalani, Kitivo cha sayansi ya Uchumi Kilimo na Biashara (SAEBs). Pia namshukuru mshauri wangu wa taaluma Prof. Ntengua S.Y. Mdoe na aliyekuwa msimazizi wangu wa SP yaani special project (Utafiti) ambaye ni Dr. Elibariki E. Msuya. Wafuatao wamekuwa wakinishauri marakwa mara na kuwa msaada sana kwangu kwa maswala mbalimbali, Mr.Bedon Dickson, Prof. Andrew Temu,Dr. Charles Lyimo, Dr. Daniel Ndyetabula, Dr. Akyoo, Dr. Magomba,Dr. Anna Temu, Mch. Emmanuel M. Falanta, Mr. Uledi Kimbavala, Mr. Heneriko Siyawezi, Mr. Albert Kamala, Mr. Salum Komba, Mr. Kinshaga Elia na taasisi kama TIEDF, TPRI, SUA, YUNASUA, KILOMBERO SUGAR COMPANY, UNESCO na wadau wote kwa ushirikiano mlio uonyesha kwangu. “Tukiwa wote tutafika mbali”. Nashukuru sana sana Mungu awabariki.

4

SURA YA KWANZA KILIMO-BIASHARA Kilimo-Biashara ni neno moja linalo unganishwa na maneno mawili neno KILIMO na neno BIASHARA, na inaweza kuelezewa kuwa ni shughuli ya kilimo inayo husisha matumizi bora ya elimu ya ujasiriamali katika kujipatia faida. Katika hili nimuhimu sana kuzingatia mambo kadha wa kadha na ni kiini cha mafundisho ya kitabu hiki, kuwa watu wanatakiwa wafuate mbinu, teknolojia za kisasa na kwa faida. Inahusisha matumizi ya gharama ndogo katika uzalishaji ili kupunguza tatizo la ukata wa fedha na uchumi uliopo kulinda usiyumbe. Kilimo ni shughuli ya kiuchumi ya uzalishaji mazao shambani, misituni, pamoja na ufugaji wa wanyama. Kilimo kina maana pana inayo husisha mifumo ya uzalishaji mazao ya mimea, misitu, ufugaji wa wanyama (kama mbuzi, kondoo, ngombe), samaki, ndege (kama kuku, bata na njiwa) n.k. Watu wengi hujihusisha katika kilimo kwa namna moja au nyingine hasa kwa nchi zinazo endelea.Wapo wale wanaolima mazao kwaajili ya kupata chakula. Na kundi la pili ni wale wanao lima au kufuga kwa ajili ya biashara. Yote hayo ni kwaajili ya kujipatia kipato na kuishi maisha yaliyo bora zaidi. Hapa ni pamoja na kupata chakula, malazi, mavazi, elimu, maji na mambo mengine muhimu kwa binadamu kuishi vizuri."Kilimo sio sekta tuu ambayo inasaidia kukua kwa uchumi wa nchi

barani afrika, lakini lazima iwe sekta tegemezi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi za afrika" (Paul Kagame- Rais wa Rwanda)

Biashara Maana yake ni kuuza na /au kununua ili kujipatia faida na kukidhi matakwa ya mteja na matarajio. Zipo biashara nyingi duniani zinzfanyika, mfano: Biashara halali na zisizo halali kutegemea na sheria na taratibu za eneo au serikali husika. Biashara haramu zinzweza kuhusisha shughuli ambazo serikali imekataza kama kuuza na kununua madawa ya kulevya kama pombe haramu, konyagi, viroba, mirungi, gongo, bangi, kokeine na mengineyo madawa ya kulevya.

5

Zipo pia biasha nzuri sana na halali kabisa ambazo zinawaingizia watu kipato duniani kama biashara ya madini, biashara ya nguo, mazao, bidhaa mabali mbali za viwandani kama magari, ndege, meli, mashua, Computer na vitu vingine vingine vingi ambavyo mnaviona kwenye maduka, viosk, super market, hotel, stationary na mahali mahali. Ushauri mzuri ili kufanikiwa ni kuwa watu wajihusishe na biashara halali ambao si kikwazo kwa jamii, serikali na kwa Mungu aliye iumba mbingu na nchi. Zile biashara za magendo na ambazo hasiko rasmi zinaweza kuonekana zinakuingizia kipato lakini mtu asipo kuwa makini anaweza kujikuta ana ingia gharama marambili au zaidi kutokana na faini na mambo kama hayo. Kuipenda kazi yako ni kuithamini na kuilinda. Mtu yeyote ambaye anakitu chake cha thamani pale nyumbani si rahisi kumkuta anakiacha nje ovyo na hasa kama nyumba haina geti na ulinzi wa kutosha. Hii inaonyesha kuwa vitu vya thamani vinahitaji kulinda kupendwa na kuthaminiwa kama dhahabu na lulu vilivyo.

Ujasiriamali sasa ni nini? Kuna wanaoelezea kuwa ni mbinu au mikakati au ushawishi wa muuzaji kwa kumtaka mnunuzi anunue bidhaa au huduma hata kama mnunuzi alikuwa hana wazo na nia ya kununua ili huyo muuzaji apate faida (Salim, F.R). Kwa ujumla ujasiriamali ni hali ya kutumia ushawishi, ubunifu, akili ya ziada na

uwezo binafsi ilikufanikiwa kufanya jambo fulani katika maisha kwa kutumia vizuri fursa zilizopo. Sio lazima ujasiriamali uwe kwenye biashara, ujasiriamali unaweza kuwa katika kilimo, ujasiriamali kwenye matumizi ya fedha za mikopo mashuleni kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na mambo mengine mengi ya kimaisha ili kupata faida. Kusudi la Ujasiriamali. ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖

Kujiajiri Kukuza kipato Kusaidia jamii katika kutoa huduma za jamii Kupata faida na mafanikio kwa ujumla. Kukuza ubunifu na vipaji binafsi Kuongeza furaha na uhuru katika kujipangia majukumu Kutumia muda vizuri Uwekezaji na kukuza ndoto katika maisha Kuondoa umaskini

6

❖ Kuondoa utumwa wa fikra na mawazo finyu. Faida za ujasiriamali ❖ ❖ ❖ ❖ ❖

Kupata faida Kutumia vizuri rasilimali mbalimbali pamoja na karama zetu Kusaidia makundi ya watu wasiojiweza Kuwezesha miradi mingine ya kiuchumi Kuboresha mahusiano kati ya watu, jamii na serikali kwa ujumla.

Vikwazo katika ujasiriamali ❖ ❖ ❖ ❖

Ukosefu wa mtaji na teknolojia ya kutosha Elimu juu ya ujasiria mali Woga katika biashara Masoko ya bidhaa

FAIDA ZA KILIMO-BIASHARA ❖ Ajira.

Kilimo kinatoa fursa ya mtu kujiajiri mwenyewe, kuajiriwa au kuajiri watu. Wapo wataalamu wanaoajiriwa kutokana na fani zao ili kutoa ushauri wa kitaalamu (consultancy), kufundisha, utafiti au ajira kwa vibarua wa kawaida kufanya shughuli za uzalishaji shambani n.k. Takwimu zinaonesha zaidi ya asilimia 65 ya watu wanapata ajira kwenye kilimo moja kwa moja au kupitia njia nyingine (indirect). Hivyo kuna fursa kwasababu watu wanahitaji chakula kwaaajili ya kula, kuuza au kulisha wanyama (kuku, nguruwe, njiwa na wengineo). Hii ni fursa nyeti kwa wahitimu wa shule za sekondari na vyuo wanao kaa bila kufanya kazi kwasababu hawajapata ajira rasmi na wanasubiri kuajiriwa. ❖ Pato la taifa hasa la ndani (GDP). Pamoja na mambo mengine, kilimo hasa kilimo biashara kinasadia sana kukuza pato la ndani kwa kulipa kodi kwa serikali. Wakulima wanapo lima kwa ajili ya biashara wanalipa kodi, lakini wanapolima kwa ajili ya chakula au matumizi binafsi huwa maranyingi hawalipi kodi. Hivyo watu wakilima kibiashara, wenyewe wanafaidika lakini na serikali inanufaika kupitia kodi. Kwa Tanania, kilimo kinachangia asilimia 30% kwenye pato la ndani GDP, 2016. KILIMO BIASHARA KINALIPA!!!

7

❖ Kukua kwa biashara. Kilimo biashara ni shughuli ambayo inakuza biashara kwa ujumla wake. Biashara iwe ya bidhaa kutoka sehemu nyingine nje ya kilimo au kutoka shambani kama matunda, mbogamboga, nafaka au mazao ya biashara kama pamba au mkonge vinakuwa kwa sababu ya kilimo-biashara. Bila kilimo biashara, biashara nyingi zina dorora. Mathalani, wapo wafanyabiashara wengi ambao mtaji wao unatokana na faida toka kwenye kilimo, kukopesha wakulima au biashara yenyewe ni mazao ya kilimo. Kukua kwa viwanda Malighafi zinazo hitajika viwandani mara nyingi, hasa kwa nchi zinazo endelea kama Tanzania zinatoka kwenye shambani-kwenye kilimo. Kwahiyo, kwenye kuendeleza viwanda nilazima kuongeza nguvu ya uzalishaji kwenye kilimo. Mazao yatokanayo na kilimo yawe ya kutosheleza mahitaji ya viwanda na mahitaji ya watu kama chakula na vitu vingine. Pamoja na kuongeza uzalishaji, kuna sababu pia ya msingi kuangalia na kuzingatia ubora wa bidhaa. Ili kuzingatia hili, wakulima wapate elimu na waifuate tangia hatua za awali katika kulima, mbolea, palizi, ukuzaji, uangalizi, usafirishaji, upakiaji au uhifadhi mpaka mlaji husika apate mzigo katika myororo wa bidhaa husika. ❖ Kupatikana kwa chakula Faida nyingine kubwa sana ya kilimo-biashara ni kupatikana kwa chakula. Ni wazi kwamba, sio watu wote ni wakulima. Wapo watu wanafanya kazi ofisini au mazingira ya mijini na hawa gusi jembe. Kimsingi, wanalimiwa na wakulima wengine, wao wana nunua chakula. Kama ni mahindi, mchele, ndizi, maharagwe na mazao mengine. Katika hili, kuna mwingine anaweza akalima na kuuza ili aweze kununua chakula na mahitaji mengine. Mathalani, mazao yake yalikuwa ya biashara. ❖ Kuondoa/kupunguza umaskini. Kuna njia nyingi za kuondoa, au kupunguza umaskini kwa jamii au serikali. Mbinu moja wapo ni kupitia kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji ya muhimu mfano chakula kwa njia mbadala. Kulima, kunampa mtu ujasiri wa kuwa na chakula cha kutosha siku za usoni. Wakulima wakibarikiwa kuvuna kama hakuna magonjwa ya kutisha msimu huo, mvua ni za kutosha na mambo ya msingi yapo sawasawa, inawezekana wakavuna na kupata ziada hivyo kupunguza umaskini na ukata na kuishi maisha bora.

8

KAZI YA KILIMO TANZANIA. Watu wengi kwenye vyombo vya habari wanalalamika maranyingi wakiwemo vijana, wazee na watu wa umri wa kati kuwa hakuna kazi. Je, hivi nikweli kuwa hakuna kazi Tanzania? Anaye sema hakuna kazi inawezekana yupo sahihi lakini mara nyingi kazi zinakuwepo ila ni kuwa inawezekana kazi hiyo mhusika haipendi mathalani KULIMA. Wazee wetu wa zamani waliishi tena miaka mingi lakini kazi zao hasa vitabu vya historia vinaeleza kuwa zilikuwa ni Kilimo, ufugaji, uwindaji na kurina asali. Hivyo je, dunia kubadilika kwa teknologia haswa mfumo mpya wa “Digital” ndiyo na watu waache kabisa mambo ya zamani? Ni ukweli usio pingika kuwa edeni ni kuzuri. Shambani ndipo sehemu matunda mazuri yenye baridi yaliyo iva au matamu yanapo patikana bila kemikali. Pata picha ukienda kwenye shamba la mizabibu, miembe, michungwa, mapapai, mapeasi na matunda mengineyo ni kuwa unayakuta shamba lime limiwa vizuri hakuna vichaka, kumenyeshewa vizuri kwa kumwagilia au mvua kijani kibichi-sipati picha. Takwimu za dunia zina onyesha kunaongezeko la watu duniani, hivyo na mahitaji ya chakula yanaongezeka. Hivyo hii ni fursa kwa wakulima na wajasiriamali kuitumia fursa iliyopo ya uhitaji wa chakula duniani kuzalisha chakula kwa wingi kwa matumizi ya sasa nay a baadaye katika kujiwekea akiba kwani uhitaji huo utapeleekea njaa pasipo kuchukua tahadhari ya kuzalisha chakula kwa wingi na kuwa na tabia ya kujiwekea akiba. Mwaka 2016 idadi ya watu duniani ilikuwa takribabani bilioni 7.4 na kufikia 2050 wanaweza kufikia watu bilioni 9. Idadi ya watu hawa walio wengi ni masikini na wakulima wadogo. Kwa Tanzania takwimu zinaonyesha kilimo ni moja ya sekta muhimu katika nchi kama uti wa mgongo, inachangia pato la ndani (GDP) kwa asilimia 30%. Na watu zaidi ya 67% huajiriwa katika kilimo kama taarifa mbalimbali zinavyo ainisha. "Kijitabu cha The Economist Pocket World in Figures cha mwaka 2012 na mwaka 2017 kinaonyesha kwamba Pato la Taifa la Tanzania liliongezeka kutoka USD 21.4 bilioni mwaka 2009 hadi kufikia USD 48.1 bilioni mwaka 2014. Hii ina maana kwamba katika kipindi cha miaka 5 uchumi wa Tanzania ulipanuka mara mbili na zaidi. Licha ya Pato la Taifa kupanuka kwa 100%, kasi ya kuwaondoa Watanzania kwenye umasikini ni ndogo mno ambapo mwaka 2014 takribani asilimia 30 ya Kijitabu cha The Economist Pocket World in Figures cha mwaka 2012 na mwaka 2017 kinaonyesha kwamba Pato la Taifa la Tanzania

9

liliongezeka kutoka USD 21.4 bilioni mwaka 2009 hadi kufikia USD 48.1 bilioni mwaka 2014. Hii ina maana kwamba katika kipindi cha miaka 5 uchumi wa Tanzania ulipanuka mara mbili na zaidi. Licha ya Pato la Taifa kupanuka kwa 100%, kasi ya kuwaondoa Watanzania kwenye umasikini ni ndogo mno ambapo mwaka 2014 takribani asilimia 30 ya Watanzania walikuwa ni masikini" - Hotuba ya Arusha, 25/3/2017

CHANGAMOTO ZA KILIMO BIASHARA. Kukosekana kwa mitaji hasa kwa wakulima wadogo. Kilimo biashara kinahitaji rasilimali fedha kwaajili ya kununua pembejeo, teknolojia na gharama mbalimbali za kuwezesha kilimo husika. Ili kufanikisha kilimo biashara ni jambo la msingi kuwaelimisha wakulima wadogo namna ya kuweza kukopesheka na kuwawezesha kwa namna moja au nyingine kupata mikopo yenye riba nafuu na mazingira wezeshi. Katika utafiti nilio ufanya mwaka 2017 kwa wakulima wadogo wa miwa (outgrowers) mkoani Morogoro, utafiti ulionyesha kuwa wakulima wadogo walio wengi wanashindwa kumwagilia miwa yao kutokana na kukosa miundo mbinu ya umwagiliaji na pembejeo mbalimbali kuhudumia kilimo hicho cha miwa kama mbolea, madawa, n.k. Hii ipo maeneo mengi sana kuwa wakulima wadogo wanashindwa kufanya kilimo kuwa cha kibiashara na chenye tija zaidi kutokana na ukata wa fedha (mtaji) kupelekea wengi kulima kilimo cha kutegemea mvua na kilimo cha mazoea. Kilimo hiki cha kutegemea mvua kina changamoto na gharama (risk) ya kupoteza au kukosa mavuno kabisa kama kutatokea ukame kufuatia mabadiliko ya tabia ya nchi. Kukosa mfumo wezeshi katika kuweka mikataba na wawekezaji wakubwa. Katika kutambua kuwa wapo wadau na mashirika mbalimbali duniani yanayoweza kutoa huduma na misaada mbalimbali kuinua wanyonge, ingefaa kuwaunganisha wakulima wadogo hasa wenye fursa na nia kulima kibiashara kupewa uwezo wa kulima kimkataba na wadau hao. Hii ingesaidia kwenye maswala ya masoko, ukosefu wa mitaji, pembejeo za kilimo na teknolojia mpya nzuri za kigeni. Vikundi vya wakulima wadogo vikiwezeshwa vitazalisha kwa tija na faida kupatikana. Kupata soko la uhakika. Soko ndio jambo la kwanza kwa mkulima kuangalia, kama mkulima huyo analima kilimo cha kibiashara. Soko linaweza kupatikana kwa uhakika hasa kama kutakuwa na mpangilio maalum wa mkulima na mnunuzi wakubaliane kuwa mazao yatanunuliwa kwa bei elekezi na mambo kama hayo. Kimsingi ukuwaji wa sayansi na teknolojia na vyombo vya habari vimesaidia kukuza soko la bidhaa na huduma za mauzo kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa watu

10

wengi ulimwenguni. Kupitia mitandao ya kijamii wakulima washauriwe na kupewa elimu namna ya kuitumia vizuri kwa faida.

11

SURA YA PILI MAMBO YA MSINGI YA KUZINGATIKA KWENYE KILIMOBIASHARA NA UJASIRIAMALI KATIKA KILIMO. SOKO. Hili ni jambo la msingi sana la kuzingatia kabla ya kuingia kwenye kilimo biashara au kufanya ujasiamali kwa ujumla wake. Ni mtazamo mpya kuacha ule wa kuzalisha kwanza ndipo kutafuta soko, huu ni mfumo ambao ni wa kisasa na wataalamu wa uchumi na maswala ya ujasiamali wanashauri watu waangalie na kutafuta soko kwanza ndipo swala la uzalishaji liendelee. Nakumbuka mwaka 2016 nilipata fursa ya kushiriki kwenye kongamano la utafiti chini ya shirika moja la mazao endelevu SAT, ambapo tulipo kuwa kwenye utafiti na mafunzo yale kwa vitendo (New lecture theatre Main Campus, Chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine SUA), Nilipata fursa ya kuwauliza swali hili wakulima kuwa Je, wanapo lima mazao wana tafuta au kuangalia kwanza soko au wana lima kwanza na kuzalisha ndipo watafute soko? Lilikuwa swali mtambuka, na kila mmoja alikuwa anawaza anavyo dhani au anavyo fanya. Ila takwimu ilionyesha wengi hawana uelewa juu ya swala la kutafuta soko kabla ya kulima na kuzalisha. Wengi walijibu na kujieleza vizuri kuwa wanalima kwanza ndipo watafute soko au wateja. Hii ni bahati na sibu, je wateja wasipo penda au taka bidhaa zalishwa inakuaje? Hii ni hatari(risk) kwa mzalishaji au mkulima anaweza akawa amefanikiwa kuzalisha vizuri sana na pasipo soko vitu hivyo vika teketea “hasara- waziwazi”.

12

Katika kulima au kuzalisha inashauriwa kutafuta soko kwanza hatakama ni utafiti wa hapa na pale maswali ya udadisi, kujua bidhaa hiyo ita hitajika au laa. Baada ya kujiridhisha mkulima au mzalishaji anaweza kutoa bidhaa kulingana na mahitaji ya watu, viwango, madaraja na bei tofauti elekezi au tarajiwa kwa bidhaa au huduma husika.

MAZINGIRA NA HALI YA HEWA. Mazingira yetu yanayo tuzunguka yamebadilika sana, hii pia ina changiwa na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo ina mambo kadha wa kadha ndani yake kamaUKAME, JUA KALI, UPEPO, ARDHI NA MAMBO MENGINE KAMA

HAYO. Kwakuwa sikila kitu kinaweza kanyika kilaa sehemu. Kuna sehemu maalumu ambapo vitu Fulani vikifanyika inakuwa ni njema sana. Kila jambo lina hitaji lifanyike mahali husika, kwa muda husika na vigezo na masharti husika kuzingatiwa. Kama ni misimu ya kulima hapa Tanzania ni Vuli na Masika. Hiyo ndiyo hasa wakulima wanatakiwa wazingatie ni wakati upi wa kupanda nini wapi. Maandalizi ni lazima ya fanyike kwa wakati husika ili kuhakikisha hakuna upotevu wa muda hapo. Maandalizi ya shamba, upandaji mbegu, kuweka mbolea, palizi, umwagiliaji na uanalizi wa karibu kwa mimea husika ni muhimu sana ili kupata mazao yenye tija. Kwenye swala la ufugaji nalo ni kuzingatia kama wataalamu wanavyo tueleza. Mfano, kujenga banda au nyumba sahihi nzuri ya mifugo husika, kuandaa chakula cha kutosha na kinacho hitajika kitaalamu ili kupata tija na matokeo chanya katika ufugaji huo, kuzingatia tiba na chanjo kwa mifugo pia vinahitajika.

KUONGEZA THAMANI (VALUE ADDITION) Mazao yote yanayo tokana na mimea au wanyama yanaweza kuboreshwa, kuthaminiwa na kuongezewa thamani. Kwamfano, kutengeza uji, supu, keki, mkate, juisi, mkorogo na michanganyo mbalimbali ya vyakula kwa wanyama ni moja ya kuonesha ongezeko la thamani (value addition). Kiuchumi ili watu wapate faida, wanashauriwa kupunguza gharama za uzalishaji na gharama zingine na kuongeza thamani ya bidhaa ili kuuza kwa bei kubwa na kuongeza mapato, faida kwa ujumla wake.

BEI YA MAZAO. Bei ni kitu cha msingi sana kwenye biashara yoyote. Ni lazima kuangalia mwenendo wa bei katika soko, na taarifa muhimu kuwa nayo kabla ya kufanya maamuzi ya kuuza

13

au kunu nua. Serikali ina weza kutoa bei elekezi iwe ya juu au ya chini (maximum or minimum price) ili kusudi kuwalinda walaji (wananchi) au kuwalinda wakulima (wauzaji). Japo kuwa mara nyingi bei inaamuliwa na nguvu ya soko wauzaji na wanunuzi, lakini pia wakulima wamekuwa hawana uelewa pengine wakutosha kujua nini cha kufanya ili kuuza kwa faida. Taarifa ni muhimu sana kwa mkulima kabla hajaenda shambani. Kwasababu hiyo, niushauri kuwa kabla ya kuamua kulima mazao au kufuga mifugo, kujiridhisha na soko, magonjwa, hatari zinazo weza kujitokeza na ikiwezekana kuongea na wanunuzi kuwa utawauzia ki mkataba inasaidia kupunguza hatari ya hasara.

MUDA (Timing) Changamoto kubwa inayo wakumba wakulima wengi ni kushindwa kujua majira na muda sahihi wa kupanda au kuuza kwa faida na wapi….! Kunaumuhimu watu kuachana na kilimo cha mazoea. Kilimo cha mazoea ni kilimo cha kulima bora mradi umelima. Wengine wanaiga kulima kwasababu mwingine analima. Nivyema kujua nilini nipande nini, wapi ili niuze wapi kwa nani na kwa kiasi na kiwango gani. Kabla hujaanza kulima, tengeneza tetwork na wanunuzi, yaani mpango wa kuuza, kama ni hotelini, kwenye taasisi au wafanya biashara na watu mbalimbali itasaidia kuuza bidhaa kiurahisi na kuondoa gharama za kushindwa kuuza kwa kukosekana soko la uhakika. Kama nyanya wengi wamelima, wewe usilime nyanya kwa muda huo kama utaona ushindani ni mkubwa, wewe lima vitunguu, mbogamboga au mazao mengine ili upate soko, au kama umejiridhisha na soko lima sasa. Kilimo cha mazoea ni kilimo cha kubahatisha na kisicho na tija. Ongeza thamani, uaminifu, bidii, juhudi, usafi, ukarimu na mvuto kwa mteja ili upate mafanikio. Na haya ni kwa watu mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao kwa uweledi na ustadi kwa faida ya wote.

14

MNYORORO WA THAMANI (VALUE CHAIN)

Chanzo (Mtandao, internet) Kwa mfano wa myororo wa thamani hapo juu, inaangaliwa wahusika/wadau wa shughuli zote kuanzia uzalishaji hadi sokoni ambapo kila hatua thamani ya bidhaa inaweza kuongezeka kulingana na uborehaji, mahitaji, mahali n.k. Kuanzia nafaka hadi mimea, mimea hadi bidhaa sokoni ni mfano wa mnyororo wa thamani kama ulivyo chorwa namba 6. Katika mnyororo wa thamani kwenye kila hatua kuna ongezeko la thamani kwa namna moja au nyingine, tujifunze zaidi. Kuongeza thamani kwa kila mkulima na mjasiriamali yeyote ni jambo la msingi katika kuongeza tija na faida zaidi. Watu wawili wanaweza kuwa wanauza bidhaa zinazo fanana asilimia 100%, lakini kati ya wafanya biashara hao, mmoja anaweza kuuza kuliko mwingine na kwanini? Nilijifunza kuwa watu wanapenda kuthaminiwa, na kuhudumiwa vizuri. Kadiri unavyo mhudumia mteja vizuri kwa ukarimu, tabasamu na utu, atakuwa na shauku ya kurudi na siku nyingine. Hivyo watu wasifanye biashara kwa pesa tu!, bali wafanye biashara kama huduma na iwe huduma nzuri. “Ukimhidumia mteja hakikisha anarudi”

15

Utunzaji wa mahesabu/uhasibu Utunzaji wa vitabu vya mahesabu ni muhimu sana kwasababu husaidia katika mambo mengi kama ifuatavyo; ❖ Kufanya makadirio ❖ Kulipa kodi ❖ Kujua muelekeo wa biashara Katika biashara utunzaji wa hesabu za fedha ni muhimu sana kutunza mahesabu, ambapo ni hali ya kurekodi miamala yote inayofanyika katika biashara husika kama ilivyo ainishwa kwenye mtiriko unaofwata.Rekodi hizi zinahusisha; ❖ ❖ ❖ ❖

Manunuzi Mauzo Matumizi na Mapato

-Hivyo ni vyema mtu anaye taka kufanya biashara, kuwa na ujuzi au kuulizia wazoefu namna gani mtu anaweza kupanga vizuri mahesabu hayo ya “Cash book” ili kufanya biashara kwa kujiamini na kujua faida halisi, mapato, matumizi n.k.

FURSA ZILIZOPO KWENYE KILIMO BIASHARA. Fursa zilizopo Tanzania kwenye Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ni nyingi sana. Ikumbukwe kuwa, mambo mengi watu wanayo fanya kikubwa ni tumbo. Watu wazamani walisema, “KIKUBWA NI TUMBO, WENGINE NI WATUMISHI” Mikono, miguu, kichwa, mgongo ni watumishi kwa tumbo kuhakikisha mkono unaenda kinywani. Vivyo hivyo, katika uchumi, mambo mengine ni ziada, lakini Chakula ambacho ni kwa kila mtu na cha lazima ni muhimu mno haijalishi mtu ni mkulima au sio mkulima. Hata taifa la Tanzania linatambua kilimo kama uti wa mgongo wa mwananchi au Taifa ki-uchumi. Hivyo kwa ardhi nzuri ambayo ni hazina na tunu tuliyo pewa na Mungu inatoa fursa kwa kila mtu kujikita kwenye kilimo. Hakuna mtu ambaye akitaka kulima atakosa hiyo fursa, tofauti na kuomba kazi hasa kwa wahitimu ambapo wanaweza kuwa na vigezo na uhitaji wa kuajiriwa lakini soko lisiwahitaji na wasipate kazi wote. Fursa hizi ni nafasi ambazo watu wanazo bado na wanaweza kuzifanyia kazi na kujipatia kipato au faida mfano;

16

KILIMO CHA MAHINDI “Kulingana na msimu mahindi hupandwa mwanzoni mwa mwezi wa 11 baada ya mvua za kwanza kunyesha (specifically from 1st to 15th day of November) ambayo huvunwa mwezi Machi mwishoni au aprili mwanzoni. Pia mahindi hupandwa mwanzoni mwa mvua za masika yaani mwezi wa pili mwishoni na mwezi wa tatu mwanzoni ambayo huvunwa mwezi Julai katikati na Agosti mwanzoni....”

KUANDAA SHAMBA, KUPANDA NA KUPALILIA Kuandaa Shamba, Kusafisha, Kulima/Kutifua Ni vyema mashamba yaandaliwe mapema kabla ya msimu wa kupanda haujaanza ili kumpa mkulima fursa ya kupanda kwa wakati unaotakiwa. Kuna njia mbalimbali zinazotumika kuandaa mashamba. Kati ya njia hizi ni pamoja na kufyeka, kung’oa visiki na kulima. Shamba linaweza kulimwa kwa kutumia: ❖ ❖ ❖ ❖

Jembe la mkono - wengi wanatumia Jembe la kukokotwa na wanyama kama ng’ombe Power tillers Matrekta

Matumizi ya trekta, power tillers na jembe la kukokotwa na wanyama yanapunguza nguvu kazi kwani vinachimbua udongo na kuufanya kuwa tifutifu (kufanya isiwe na mabonge makubwa, wala isiwe vumbi vumbi). Hii husaidia: ❖ ❖ ❖ ❖

Mizizi ya mimea kupenyeza ardhini kirahisi Udongo kuweza kuhifadhi maji Udongo kuwa na hewa inayohitajika na mimea Ukuaji mzuri wa mimea hivyo kuongeza mavuno

Mbegu Bora za mahindi Matumizi ya mbegu bora ni muhimu katika upatikanaji wa mavuno mengi na bora. Kuna makundi mawili makuu ya mbegu ambayo ni: Mbegu za asili: Ni zile ambazo zimetumika miaka mingi katika historia ya kilimo Mbegu zilizoboreshwa: Hizi ni zile zilizoboreshwa kutoka mbegu za asili. Kundi hili linagawanywa kwenye makundi mawili - composite varieties na mbegu chotara (Hybrids).

17

Ushauri wa matumizi ya mbegu zilizoboreshwa unatofautiana kutoka eneo moja na lingine kwa sababu ya: ❖ Mwinuko kutoka usawa wa bahari ❖ Kiasi cha mvua katika eneo husika ❖ Muda unaotumia mbegu hadi kukomaa Mbegu za mahindi zilizoboreshwa ni kama TMV1, TAN 250, TAN 254, Staha, Situka na zingine zote zinazoanza na herufi “H” kama vile H 250, H 251 na H 615. Pia mbegu mpya zilizotangawa na Kamati ya Taifa ya Mbegu mwaka huu ni WE4102, WE4106, WE4110, WE4114, WE4115 kutoka ARI ILONGA. Jinsi Ya Kuweka Mbolea Za Kupandia Mbolea hizi zinawekwa shambani kabla ya kupanda/kusia mbegu. Zinawekwa kwa njia mbalimbali kama vile kusambaza kwenye eneo husika na kuchanganya na udongo, au kuweka kwenye mistari au mashimo ya kupandia. Ni bora zaidi kuchanganya mbolea za Minjigu Phosphate au Minjingu Mazao na udongo kuliko kutia kwenye shimo la kupandia. Pia kuchanganya mbolea na udongo huondoa athari za mbolea kwenye uotaji wa mbegu, hasa kama kuna uhaba wa unyevunyevu.

Viwango Vya Mbolea Za Kupandia mahindi Kiwango cha mbolea za kupandia kilichopendekezwa ni kilo 20 fosfati (P) kwa hektari ambayo ni sawasawa na kiasi cha mifuko 2 ya DAP (= mfuko mmoja kwa ekari). Ikiwa mbolea ya minjingu phosphate itatumika basi mifuko mitatu itatosa kwa hekta (= mfuko mmoja na nusu kwa ekari). Na endapo utaamua kuitumia mbolea ya minjingu mazao basi tumia mifuko minne na nusu kwenye hekta moja au mifuko miwili kwa ekari moja. Upandaji wa mahindi Muda wa kupanda: Kulingana na msimu mahindi hupandwa mwanzonimwa mwezi wa 11 baada ya mvua za kwanza kunyesha (specifically from 1st to 15th day of November) ambayo huvunwa mwezi Machi mwishoni au aprili mwanzoni. Pia mahindi hupandwa mwanzoni mwa mvua za masika yaani mwezi wa pili mwishoni na mwezi wa tatu mwanzoni ambayo huvunwa mwezi Julai katikati na Agosti

18

mwanzoni. Katika msimu huu utayarishaji wa shamba hufanyika mwezi wa pili mwanzoni. Muda wa kupanda unatofautiana kutoka eneo moja kwenda jingine kulingana na majira ya mvua. Kwa mfano katika wilaya ya Morogoro tarehe za kupanda ni kuanzia februari 15 hadi Machi 15. Mkulima anashauriwa afuate kalenda ya muda wa kupanda kama anavyoshauriwa na bwana shamba wake. Nafasi ya kupandia mahindi Kupanda kwa nafasi ni kati ya njia bora za kilimo inayomwezesha mkulima kupata mazao bora. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia kupanda kwa mistari na kufuata nafasi zinazoshauriwa na wataalamu wa kilimo. Zifuatazo ni nafasi za kupanda mahindi na idadi ya mbegu kwa kila shimo na kiasi cha mbolea (kwa vizibo vya soda) inayotakiwa kuwekwa kwa shimo: Kwa nafasi ya 90 sm X 30 sm, panda mbegu moja na uweke kizibo kimoja cha mbolea Kwa nafasi ya 90 sm X 25 sm, panda mbegu moja na uweke kizibo kimoja cha mbolea Kwa nafasi ya 90 sm X 50 sm, panda mbegu mbili na uweke vizibo viwili vya mbolea Kupalilia Ni muhimu shamba lipaliliwe baada ya mimea kuota ili kuondoa magugu. Magugu ni mimea hivyo hushindana na mimea iliyopandwa na mkulima kwa kunyonya virutubisho ardhini. Magugu yanaweza pia kuhifadhi wadudu na magonjwa yanayoweza kushambulia mimea iliyopandwa na hivyo kupunguza mavuno. Magugu yaweza kuondolewa wa palizi ya mkono (yaani) kung’olea (ikiwa magugu yapo mbali mbali sana) au kulima kwa jembe la mkono au kwa kutumia dawa/viuagugu (HERBCIDES) hasa 2-4D. Mbolea za kukuzia mahindi Ni mbolea zinazotumika baada ya mimea kuota kwa lengo la kuikuza mimea ili itoe mavuno bora. Mara nyingi mbolea hizi zinatoa kirutubisho cha naitrojeni. zifuatazo ni mbolea za kukuzia na kiwango chake cha naitrojeni:

19

UREA: 46% N Calcium Ammonium Nitrate, CAN: 23% N Sulphate of Ammonia, SA: 21% Urea inakirutubisho cha naitrojeni (N) kwa kiwango kikubwa na watu wengi wanauzoefu nayo. Vilevile bei yake ni nafuu ikilinganishwa na mbolea zingine za kukuzia. Mbolea hii iko katika hali ya chengachenga za mviringo (granules) za rangi nyeupe. Kiwango cha urea ni nusu kizibo cha soda kwa kila shina. Mbolea hizi hazidumu kwenye udongo kwa muda mrefu kwa hiyo huwekwa shambani wakati mimea inapokuwa na mahitaji makubwa ya kirutubisho cha naitrojeni na wakati udongo una unyevunyevu na shamba halina magugu. Pia wakulima hutumia mbolea za kukuzia zinazopatikana kwa bei nafuu kama vile BOOSTER (foliage nitrogeneous fertilizers) ambayo hupigwa kwa kunyunyizia katika majani ya mmea kila baada ya wiki 3, kwa mara 2-3 mpaka mahindi kuvunwa. Kiwango cha kupiga ni mchanganyo wa mls 50-80 ktk lita 15 za maji. Mbolea za kukuzia huwekwa kuzunguka kila shina la mimea au pande mbili au tatu au nne za kila shina. Cha muhimu ni kwamba mbolea isirundikwe sehemu mmoja. Minjingu Mazao (kg 50/ekari = gramu 10kwa shimo) pia yaweza tumika kwa kukuzia, hivyo mkulima yko huru kuchagua kulingana na uwezo na upatikanaji wake. Viwango Vya Mbolea Za Kukuzia Vinavyoshauriwa Kiwango kinachopendekezwa ni kilo 60 naitrogeni kwa hektari, ambacho ni sawasawa na kiasi cha mifuko miwili ikiwa utatumia UREA. Hata hivyo mbolea zingine kama SA inaweza kutumika kama kuna mahitaji ya salfa. Hivyo basi utumie mifuko mitatu kwa hekta ambayo ni sawa na mfuko mmoja kwa ekari. CAN inaweza kutumika kama kuna mahitaji maalum ya nitrate na ammonium na endapo utaitumia basi mifuko minne na nusu itatosha kwa hekta, ambapo kwa ekari moja utatumia mifuko miwili tu. Kwenye mahindi mbolea ya kukuzia inawekwa baada ya palizi ya kwanza ambayo ni kama wiki tatu mpaka wiki nne baada ya kupanda. Kwa kila mmea mmoja weka kiasi hiki cha mbolea: UREA: kizibo kimoja cha soda CAN: vizibo viwili vya soda, na

20

SA: kizibo kimoja cha soda Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Kuweka mbolea: Sehemu za nchi ambazo muda wa kukua mahindi ni mrefu (zaidi ya miezi mitatu), ni vyema kuweka mbolea za kukuzia mara mbili, yaani nusu ya kiwango kinachopendekezwa baada ya mwezi mmoja, na kurudia tena (kutumia nusu iliyosalia) baada ya wiki tatu. Kupalilia: Katika kilimo cha mahindi, ni muhimu shamba lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda. Wataalamu wanashauri kwamba katika kilimo cha mahindi, shamba lipaliliwe mara 2-3, kufuatana na hali ya magugu katika shamba. - Utafiti unaonyesha kwamba, shamba la mahindi ambalo halijapaliliwa linaweza kupunguza mavuno kwa asilimia 60 hadi 100 ya mavuno yanayotarajiwa. Hata kama mkulima atatumia mbegu bora, aina na kiasi cha mbolea zinazoshauriwa, kupanda kwa mstari pamoja na mbinu nyingine bora zinazoshauriwa, bila kupalilia hali hii itaathiri mavuno yake.

KUDHIBITI MAGONJWA NA WADUDU WANAOSHAMBULIA MAHINDI Magonjwa Yanayoshambulia Mahindi i) Maize streak virus Dawa/Kudhibiti: Mbegu bora inayostahimili ugonjwa, kupanda mapema, kung’oa mimea iliyoathirika ama kunyunyiza dawa za kuua ‘vectors’ kama vile inzi weupe (white flies). ii) Smut (Fugwe) Dawa/Kudhibiti: Tumia Helerat ukifuata maagizo kamili. iii) Cob rot (kuoza kwa mhindi) Dawa/Kudhibiti: Tumia mbegu zinazostahimili kuoza. Wadudu Na Wanyama Wanaoshambulia Mahindi a) Viwavi Jeshi

21

Ni wadudu aina ya funza ambao hutokana na Nondo.Hushambulia mahindi kwa kula majaniyake pamoja na shina. Wadudu hawa huangamizwa/kudhibitiwa kwa njia zifuatazo; Kuondoa vichaka karibu na shamba Kunyunyizia sumu za asili kama vile Mwarobaini majuma mawili ya mwanzo. Kunyunyizia sumu za viwandani endapo wadudu wameanza kuonekana kama vile Karate 1ml/1L

b) Funza wa Mabua (Maize Stalk Borer) Funza wa mabua hutoboa shina la mahindi na kusababisha kudumaa kwa mahindi. Matundu, ungaunga kama wa msumeno huonekana kwenye majani yaliyoathiriwa. Mashambulizi huanza juma la pili hadi la tatu baada ya mahindi kuota. Njia za kudhibiti zinazotumika Kuchanganya mahindi na mazao jamii ya mikunde km vile maharagwe Kung’oa mahindi yaliyoshambuliwa Sumu za asili mwarobaini Sumu za viwandani km vile Karate. pia waweza tumia Malathion, sumithion, vumbi ya cymbush au Sevin 5G na ufuate maagizo kamili. c) Cutworms (Vikata Shina) Dawa/Kudhibiti: Tumia Dragnet FT na ufuate maagizo kamili. d) Wanyama waharibifu Kudhibiti: Kuwatishia na kuwafukuza wanyama. Ili mkulima aweze kupata mazao mengi na bora inashauriwa kutumia dawa za kuzuia magonjwa na wadudu washambuliao mimea na njia zinginezo.

22

KUVUNA, KUKAUSHA, KUSAFISHA NA KUHIFADIHI Kuvuna Mahindi yako tayari kuvuna wakati kikonyo kimekuwa dhaifu na mahindi yanaangalia chini. Mahindi yakishakauka vizuri yanatenganishwa na bua halafu majani ya mhindi kutolewa. Kukausha Kama mahindi hayajakauka vizuri hukaushwa zaidi katika juani siku 3-4 ili kupunguza unyevunyevu kufikia kiwango kinachofaa kwa kuhifadhi (14%). Ni muhimu mahindi yakauke vizuri ili yasioze yakiwekwa ghalani. Ili kujua kama mahindi yamekauka vizuri, tia mahindi kadhaa kwenye chupa ya soda iliyokauka na uongeze kiganja kimoja cha chumvi. Tingisha chupa halafu uwache itulie kwa dakika tatu. Chumvi ikikwama kando ya chupa, basi mahindi hayajakauka vizuri. Kusafisha Mahindi yaliyokauka vizuri hupepetwa na vilevile mahindi mabovu huondolewa. Kuhifadhi Mahindi huhifadhiwa ghalani baada ya kuwekwa viatilifu vya kuzuia bungua wa mahindi Njia za kisasa za uhifadhi hutumiwa kama vile matumiz ya ACTELLIC SUPER DUST katika uwiano wa 1kg kwa gunia 5-10 za ujazo wa 100kg. Kiatilifu kingine ni actellic solution katika rate ya 5mls katika gunia moja la kg 100. Njia nyingine ya kienyeji katika kuhifadhi mahindi ni kuweka juu ya ghala ambalo chini yake kuna jiko la kupikia ambalo hutoa moshi unaotumika kufukuza na kuua wadudu.

KILIMO BORA CHA MAHARAGE “Maharage ni moja kati ya mazao ambayo yanalimwa sana na ni moja kati ya mazao yanayo waongezea kipato wakulima wengi sana nchini Tanzania lakn kwa kufuata kanuni za kilimo bora MAHALI PA KUPANDA Maharage hupandwa mahari kwenye muiniko wa mita 400-2000 kutopka usawa wa bahari kwenye udongo usio tuamisha maji WAKATI WA KUPANDA

23

Sehem za umwagiliaji panda wakati wa kiangazi na sehem zenye mvua nyingi zinazo anza mwezi november hadi disemba april na may panda mwezi februali na machi. MAANDALIZI Shamba; lima shamba vizuri na kufukia yale magugu na lima kufuatana na mwinuko wa ardhi Mbegu; Andaa mbegu bora mapema kulingana na chaguo lako Mbolea;andaa mbolea kilo 75 DAP au 150 mijingu kilo 50 TSP na CAN kwa ekari KUPANDA Maharage yanatakiwa kupandwa eneo lenye unyevu wa kutosha weka ulefu wa sentimita 2.5 hadi 3 na fukia vizuri na hakikisha mbolea aigusani na mbegu kuepusha kuunguza mbeguna kwa maharage madogo ni kilo 25 had 30 kwa hekari na maharage makubwa ni kilo 40 48 Kwa maharage pekee panda sm50 kati ya mstari na mstari na sm10 kati ya shina na shina kwa kilimo mseto panda mahindi sm75 mstari na mstari na sm60 shina na shina weka mbegu 3 kwa maharage yanayo tambaa na 6 kwa maharage mafupi PALIZI Palizi inatakiwa kufanyika siku 14 baada ya maharage kuota na rudia tena kabla ya kuchanua. unaweza kutumia madawa ya kuuwa magugu kama galex,stomp, dual gold,sateca WADUDU WAHARIBIFU FUNZA WA MAHARAGE ni wadudu wadogo wanao shambulia mimea michanga ya maharage wanaweza kusabisha uharibifu hadi kufikia asilimia 100 njia nzuri ya kuwazibiti ni kuwanynyuzia dawa mfano karate 5EC au actelic50 EC ndani ya sku nne hadi 5 baada ya maharage kuota wadudu wengine ni wanao kula maua kutoboa vitumba na mbegu pamoja na wale wanao bungua ghalani MAGONJWA Magonjwa makubwa ni Ndui ya maharage

24

Madoa pembe Kutu Magonjwa yanayo sababishwa na bakteria na virusi punguza magonjwa hayo kwa kupanda mbegu safi, aina znazo vumilia na kutunza shamba na unaweza kutumia madawa kama kocide,fugulani,Bayleton kwa kuzuia magonjwa yanayosababishwa na ukungu na bakteria UVUNAJI Maharage yanatakiwa kuvunwa pale yanapo kauka kuepusha kuoza na kupasuka na yanapo kauka piga vizuri mbegu zisipasuka au kuruka mbali pepeta na chambua kuondoa uchafu anika yakauke vizuri kabla ya kuifadhi HIFADHI Ghara au chombo cha kuifadhia lazima kiwe safi na zuia wadudu kwa kutumia dawa asili na zaviwandani NOTE; Maharage yanaweza kuzaa gunia 6 hadi 10 ukifuata kanuni bora za kilimo cha maharage” (Lubaba, I )

KILIMO CHA KOROSHO Korosho ni zao la biashara hapa Tanzania linalostawi vizuri katika ukanda wa pwani; mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani. Korosho ina matumizi mengi ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa mafuta ya kula, Keki na hutumika pia kama nuts kwa binadamu. Hata hivyo mbali na kuwepo kwa matumizi hayo kuna fursa ambayo bado mbichi kutokana na bibo la korosho ambalo huwezakutengeneza wine (mvinyo), Juice, Jams na local beer (pombe za kienyeji) Fursa hii ya usindikaji wa mabibo ya korosho katika kutengeneza mazao tajwa hapo juu, inahitaji uwekazaji katika techolojia ili kuweza kusindika bibo hizo na kupata rasimali watu wenye uwezo katika kufanikisha hilo. Ni wakati mzuri kujikita katika fursa hii ili mabibo yanayopotea kuweza kugeuzwa katika bidhaa ambazo zitatuletea kipato; changamkia Fursa hiyo hapa Naliendele Mtwara na maeneo yanayozalisha Korosho nchini.

25

KILIMO CHA PAPAI

Papai ni tunda lenye ladha nzuri, na rahisi kuliwa. Aina hii ya tunda ni chanzo cha virutubisho muhimu mwilini, ambavyo husaidia kujenga mwili. Zao hili asili yake ni ukanda wa kitropiki ambao hauna baridi kali na joto kiasi. UDONGO Mipapai hustawi vizuri kwenye udongo usiotuhamisha maji. Endapo maji yakituama kwenye eneo lililopandwa mipapai kwa muda wa siku mbili, mpapai unaweza kuoza kwa haraka na kufa. Kwa kuwa mipapai haina mzizi mkuu, inahitaji udongo wenye rutuba ya kutosha. Halikadhalika, zao hili halihitaji udongo wenye kina kirefu, hivyo ni muhimu kumwagilia mipapai wakati wa kiangazi. Wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hali hiyo huongeza ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema baada ya kuvunwa. KUPANDA

26

Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mkali. Hii itasaidia mipapai kukua vizuri bila kuvunjika kwani mti wa mpapai huvunjika kirahisi. Inashauriwa kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka shamba la mipapai. Ili kuwa na tija zaidi, unaweza kupanda aina nyingine ya miti ya matunda kama vile miparachichi, na miembe. Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai. Miti hiyo inaweza kutangulia kupandwa miezi kadhaa kabla ya kupanda mipapai. MBEGU Kusanya mbegu toka kwenye mapapai makubwa na yaliyo komaa na kuiva, kisha kausha mbegu vizuri kabla ya kupanda. Inashauriwa kununua mbegu kutoka kwa wazalishaji wanaoaminika na waliothibitishwa, ili kuwa na mazao bora zaidi na yanayoweza kukabiliana na magonjwa. Mbegu aina ya red royal F1, inasifika zaidi kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na magonjwa yanayoshambulia mipapai, na huanza kuvunwa mapema zaidi, kati ya miezi 6 hadi 12. Aina hii huvunwa mfululizo kwa miaka 5 hadi 7. UANDAAJI WA SHAMBA Inashauriwa kuandaa shamba vizuri kwa kuondoa visiki na magugu yote. Shamba lilimwe vizuri, na kuhakikisha udongo umelainika vizuri. MASHIMO Chimba shimo kwa ajili ya kupanda mpapai, liwe na kina cha sentimita 60 na upana wa sentimita 60. Weka mboji debe moja kisha changanya na nusu ya udongo uliotoa kwenye shimo, kisha rudishia kwenye shimo. Mwagilia maji kwa kipindi cha wiki mbili kabla ya kuotesha. KUOTESHA Sia miche kwenye kitalu, kasha hamishia shambani inapokuwa na urefu wa sentimita 30. Chomeka mche kwenye ardhi kina cha kati ya sentimeta 1 – 2 chini ya udongo kwenye shimo uliloandaa. Hii itasaidia mche kupata joto la wastani na kuepuka mche

27

kuoza na kufa. Baadhi ya wakulima hupenda kuotesha mipapai moja kwa moja shambani. Endapo unapenda kufanya hivyo, zingatia haya; Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea ya kuku au mboji sehemu unayokusudia kupanda. Mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia kukinga mipapai na magonjwa. Panda mbegu 3 – 4 kila shimo, hii ni kwa sababu miche mingine inaweza kufa kutokana na magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota mipapai dume. NAFASI Shimo hadi shimo, liwe na nafasi ya mita 3, na mstari hadi mstari mita 3. Hii itasaidia miche ya mipapai kukua vizuri bila kusongamana. PUNGUZA MICHE Baada ya miezi 3 – 5 tangu kupanda, mipapai itaanza kutoa maua na hapo jinsia ya mipapai itajulikana. Inapofikia wakati huo inabidi kupunguza mipapai mingine hasa midume. Mipapai yenye jinsi zote isizidi asilimia 10 – 20 ya miche yote iliyopo shambani, na midume ibaki mmoja katika kila majike 25. UTUNZAJI Weka kilo 2 – 5 za samadi kwenye kila mpapai kwa mwaka ili kuongeza ukuaji na uzalishaji. Mabaki ya mimea yanaweza kuwekwa kama matandazo. Hii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu usipotee. Chunguza mipapai mara kwa mara ili kuangalia kama kuna magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au kufukiwa chini endapo itabainika kuwa na maonjwa. Unaweza kunyunyiza dawa zisizo na madhara za kukinga au kukabiliana na magonjwa ya ukungu na virusi.

28

KUPOGOA Kata matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai. Hili lifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa. Ondoa mipapai yote ambayo hayakuchavushwa vizuri na ubakize yenye afya tu. PALIZI Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili kuzuia uoataji wa magugu. Magugu yang’olewe yakiwa machanga. Epuka kuchimbua sana wakati wa palizi kwa kuwa mizizi ya mipapai huwa juu juu. MAGONJWA Zao la papai halina magonjwa mengi sana yanayoshambulia endapo litatunzwa vizuri. Hata hivyo kuna baadhi ya magonjwa ambayo yamezoeleka kwenye zao hili kama vile Ugonjwa wa madoa kwenye majani (Papaya spot) na Ugonjwa wa virusi unaojulikana kama Mozaic virus. Mimea yenye magonjwa inaweza kung’olewa na kufukiwa ili kudhibiti ueneaji kwenye mimea mingine. MASHINE ZA KILIMO

-Wasiliana na Tanzania Institutional Economics Development Foundation (TIEDF), watakuelekeza na kukushauri wadau wanao uza aina zote za mashine na pembejeo za kilimo. Simu 0753442903 Barua pepe, [email protected]

UCHANGANYAJI WA VYAKULA VYA WANYAMA NA MIFUGO. Kwanza ifahamike kuwa kuna formular nyingi Sana unazoweza kuzitumia kwa lengo la kutengeneza chakula cha mifugo yako lengo tu ni uweze kupunguza angalau gharama za uendeshaji wa mradi wako, Hapa mimi nawapa mojawapo ya formular

29

hizo na faida ya kujua kuchanganya chakula peke yako nyumbani ni kupunguza gharama za kununua chakula cha kiwandani, uweze kutumia malighafi zinazopatikana eneo lako n.k. Ili kuweza kufikia huko unahitaji vitu ama malighafi utakazozitumia ili ziweze kukupatia virutubisho vikuu anavyohitaji mfugo wako ili aweze kukuzalihishia unachokitaka na virutubisho hivyo ni proteins, vitamins, madini, fat, na carbohydrates. Malighafi tutakazotumia hapa ni _pumba mahindi =carbohydrates, Mashudu alizeti=protein+fat, dagaa sagwa=protein+madini, chokaa mifugo=madini, and madini mchanganyiko/premix=madini na chumvi=madini_. CHAKULA CHETU TUTAKACHOTENGENEZA NI CHA KILO 100. *VIFARANGA NYAMA ANZA /BROILER STARTER* Pumba mahindi.... 76kg Mashudu alizeti.... 12kg Dagaa sagwa........ 10kg Chokaa mifugo..... 1kg Premix... .................0.5kg Chumvi sagwa......0.5kg *VIFARANGA NYAMA KUZIA* Pumba mahindi 76kg Mashudu alizeti 15kg Dagaa sagwa 7kg Chokaa mifugo 1kg Premix 0.5kg Chumvi sagwa 0.5kg *VIFARANGA MAYAI ANZA* Pumba mahindi 76kg Mashudu alizeti 16kg Dagaa sagwa 5kg Chokaa mifugo 2kg Premix 0.5kg Chumvi sagwa 0.5kg *KUKU MAYAI KUZIA* Pumba mahindi 80kg

30

Mashudu 12kg Dagaa 5kg Chokaa 2kg Premix 0.5kg Chumvi 0.5kg *KUKU MAYAI TAGA* Pumba 80kg Mashudu 14 kg Dagaa 3kg Chokaa 2kg Premix 0.5kg Chumvi 0.5kg *NGURUWE WATOTO* Pumba 76kg Mashudu 15 kg Dagaa 6kg Chokaa 2kg Premix 0.5kg Chumvi 0.5kg *NGURUWE KUKUZIA* Pumba 78kg Mashudu 15kg Dagaa 4kg Chokaa 2kg Premix 0.5kg Chumvi 0.5kg *NGURUWE NENEPESHA* Pumba 80kg Mashudu 15kg Dagaa 2kg Chokaa 2kg Premix 0.5kg Chumvi 0.5kg

31

*NG'OMBE MAZIWA* Pumba 80kg Mashudu 17kg Chokaa 2kg Premix 0.5kg Chumvi 0.5kg -Pia sehemu yenye Pumba mahindi unaweza usiweke tu pumba yenyewe bali unaweza kuchanganya pumba nusu na paraza nusu kwa mfano kama pumba imeandikwa 76kg unaweza kugawa nusu 38kg ikawa pumba na hiyo 38kg nyingine ikawa paraza lakini iwe tu ni kwa kuku isiwe kwa nguruwe au ng'ombe, na pia sehemu yenye chokaa unaweza ukagawa ikawa chokaa na mifupa sagwa ukifanya hivi chakula chako kitakua vizuri zaidi_. *KUKU KIENYEJI/BATA* _UJAZO NI KILO 50_. Pumba mahindi 38kg Mashudu 7kg Dagaa 2kg Mifupa/chokaa 2kg Premix 0.5kg Chumvi 0.5kg

Kimsingi, hapa ni fursa mbalimbali za kilimo biashara, hawa ni baadhi tu ya wadau ila wapo wengi sana, mimi, wewe na yeye tunahusika na tunaweza kuwa na biashara hizo.

UFUGAJI WA SAMAKI Kwa tafiti zilizo fanyika, ufugaji wa samaki nchini Tanzania ulikuwa na takribani wafugaji 17,100 wanaofanya ufugaji wa maji baridi na 3,000 wanafanya ufugaji wa maji chumvi. Katika jarida moja nililopata kulisoma kuhusu ufugaji wa samaki, Bwana Ayubu Nnko anasema, “Mbali na kuwa kuna aina nyingi za samaki wanaofugwa

duniani, lakini hapa nchini ni aina kuu mbili ndizo zinazofugwa nazo ni perege na kambale. Ufugaji huu umetokana na sababu kuwa samaki hawa ni rahisi kuwafuga na mahitaji yao si makubwa sana”.

32

Perege Samaki huyu anakuwa vizuri katika nyuzi joto kati aya 16˚C hadi 30˚C kutegemeana na ukubwa na umri wa samaki. Kambale 83, wenye angalau sentimeta 30 kila mmoja, wanaweza kukaa katika eneo la mita 100 za mraba. Aidha hukua vizuri hasa maji yakiwa katika nyuzi joto kati ya 26˚C hadi 33˚C lakini kwa wastani wa nyuzi joto 28˚C.

Umuhimu wa kufuga samaki Soko: Soko la samaki limekuwa likiongezeka siku hadi siku kutokana na ongezeko la watu na mahitaji kwa ujumla. Hivyo uhitaji wa samaki ndani na nje ya Tanzania kuongezeka kwa kasi inapelekea samaki wanaozalishwa wasitosheleze mahitaji.Hii ni fursa ya watu kuwekeza katika kufuga samaki kwa wingi zaidi ili kukidhi mahitaji na kuondoa tatizo la upungufu linalosababisha kuagiza samaki kutoka nje ya nchi. Inasemekana kupungua kwa samaki asili kwenye mito, maziwa na bahari kunakotokana na uvuvi haramu na wa kupindukia. Urahisi na fursa ya ufugaji wa samaki kwa ujumla. Kimsingi gharama za malisho ya samaki simakubwa sana kiasi cha watu wengi kushindwa kufuga samaki. Hawahitaji eneo kubwa sana wala chakula chao sio cha gharama kubwa sana. Faida lukuki: Uvunaji wa samaki ni kuanzia miezi mitatu au minne hadi miezi kumi na mbili(6-12). Pamoja na kufuga samaki mkulima anaweza kuanzisha bustani ya mboga mboga na matunda katika kutumia vizuri rasilimali maji na ardhi karibu na bwawa la samaki. Upatikanaji wa maji ni fursa kubwa na sababu ya kufuga samaki kwa wingi nchini Tanzania. Nchi ya Tanzania ni moja ya nchi duniani zenye eneo kubwa lililo zungukwa na maji ya kutosha kama bahari, mito, maziwa, mabwawa na chemichemi kadha wa kadha. Kwa watu pia wenye maji ya bomba wanaweza kufuga samaki kabisa na hata wanaotunza maji ya mvua. Upatikanaji wa chakula/ mboga. Ni kweli kwamba watuwengi wanapenda sana samaki, hata wataalamu wa afya wanasifia samaki kama nyama zisizo na madhara kwa

33

binadamu kama zilivyo nyama nyekundu. Kitoweo cha samaki kinasifika kwa upatikanaji wa protini ya kutosha. Pato la taifa (GDP): Biashara ya samaki ni moja ya biashara zinazochangia pato la taifa kupitia kodi kwa wafanya biashara (wavuvi). Huvumilia magonjwa: Samaki niwavumilivu sana kwa magonjwa mbalimbali na gharama za kuwatibu sikubwa sana kama ilivyo mifugo mingine.

Mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza ufugaji wa samaki Ili kufuga kwa tija na faida kuepuka kufuga kwa mazoea, nivyema kufwata kanuni bora zinazo tokana na tafiti za wataalamu na sayansi hiyo. Kimsingi nimambo mengi yanayohitajika kuzingatiwa. Baadhi ya mambo hayo ni kama:Aina bora ya samaki: Mfugaji nivyema achague mbegu bora yenye tija na soko la uhakika kwa faida. Chakula bora kwa samaki cha kutosha: Samaki wapewe chakula chenye viini lishe vinavyo hitajika na cha kutosha ili samaki wakue na kuongezeka kwa wakati. Samaki wanavyo kuwa wengi wanagombania chakula (struggle for fittest), hivyo mfugaji ahakikishe idadi ya samaki wanaoweza kuenea kwenye bwawa ndiyo hao hao, wakiongezeka zaidi wakubwa waanze kuvunwa (kuvuliwa). Makazi bora: Nilazima kama ni bwawa la samaki liwe na mazingira rafiki kwa samaki kustawi na kuongezeka kwa kuzaliana. Mazingira bora ni pamoja na hali ya joto, baridi kuwa nzuri kwa samaki wanaofugwa ili kuepusha magonjwa. Tiba kwa samaki wagojwa: Wale samaki wote wanao umwa au kuwa na dalili za ugonjwa, wapewe tiba kwa wakati ili ugonjwa usisambae kwa samaki wengine au kusababisha kifo cha samaki mgonjwa. Anzia sokoni: Hii inamaanisha kuwa, mfugaji wa samaki aangalie uhitaji wa soko ili kupanga kufuga kibiashara. “Kutazama soko ni kutazama muelekeo” Eneo la kufuga samaki liwe zuri kwa ufugaji wa samaki: Hapa mfugaji aangalie vitu kama upatikanaji wa maji ya kutosha, aina ya udongo, mwinuko na lisiwe mbali sana na nyumbani ili iwe rahisi kwa huduma na ulinzi. Namna ya kuanza ufugaji

34

❖ Mazingira yameandaliwa vipi tayari kwa ufugaji? Mfugaji atengezeze eneo bora kwa ajili ya kufuga samaki kwa kuzingatia ainaya samaki, idadi ya samaki na uwezo wa huduma au kifedha. Eneo hilo linaweza kuwa bwawa au tanki kutegemea na aina ya eneo au malengo na mtazamo wa mfugaji. ❖ Kagua ardhi na mazingira kwa ujumla unapokusudia kujenga bwawa ili kutambua ni bwawa gani linafaa kujenga katika eneo hilo. ❖ Safisha vizuri eneo hilo, fyeka kama kuna majani na kata miti. ❖ Ondoa udongo wa juu kwenye eneo husika. KAMBALE ❖ Samaki huyu hukua katika joto dogoau kubwa sana na pia katika oksijeni kidogo. Majike wana uwezo wa kutaga mayai hadi 10,000 hadi 15,000 na ana uwezo wa kukua hadi kufikia gramu 500 ndani ya miezi nane(8) kamauzalianaji wake utadhibitiwa vizuri na akapewa chakula cha kutosha. Samaki huyu anaweza kupevuka mara tu afikishapo miezi 2 au akiwa na urefu wa sm 10 japo kwa kawaida ni kati ya miezi 4 hadi 6.Kitaalamu inashauriwa kuweka samaki wawili katika kila mita moja ya mraba hii itasaidia kutokana na kuwa samaki hawa huzaliana kwa wingi na hivyo kujazana kwenye bwawa. ❖ Mambo ya kuzingatia kabla ya kujenga bwawa. ❖ . 1. Eneo la ardhi ❖ Ukubwa wa eneo hutegemeana na samaki unaokusudia kuwafuga. Hakikisha eneo la ardhi ni tambarare lakini pia na mwinukokidogo unaruhusiwa isipokuwa eneo hilo lisiruhu kuwepo kwa mafuriko. Pia, eneo lisiwe na uchafuzi wowote wa mazingira na lisiwe na miti mingi na vichaka vitakavyozuia kuwepo kwa mwanga na jua.

2. Upatikanaji wa maji ❖ Maji ndiyo maisha ya samaki kwani upumuaji wake (kutumia matamvua) hutegemea maji kwa asilimia miamoja (100%). Kwa mantiki hiyo, eneo la

35

kufugia ni lazima liwe na upatikanaji wa maji kwa kipindi chote cha mwaka. Vyanzo vya maji kwa ajili ya ufugaji wasamaki ni kama chemichemi, mito, maziwa, na maji ya ardhi (visima). Hakikisha vyanzo hivyo vya maji ni salama kwa maana kuwakusiwe na madawa yanayoweza kuathiri samaki kama vile madawa ya kupulizia nyanya au mbogamboga. Maji yaliyo ndaniya bwawa yanapaswa kuwa na joto kiasi fulani kwani ni muhimu sana kwa ufuigaji wa samaki. Tilapia anakuwa vizuri katika maji yenye uvuguuvugu (nyuzi joto 25-30) katika nyanda za chini japo pia anaweza kuishi katika maji ya baridi sehemu za mwinuko akikua taratibu na kuzaliana polepole.

3. Aina ya udongo Udongo mzuri unatakiwa usiwe na changarawe, mawe wala usiwe na mchanga mwingi kwani hautakuwa na uwezo wa kutuamisha maji kwa muda mrefu. Eneo lenye udongo kama ule unaotumika kutengenezea vyungu au udongo wa mfinyanziwa bwawa na wa kufyatulia matofali ndiyo mzurisana la linalofaa kwa kujenga bwawa la samaki. Mambo mengine ya kuangalia katikakuchagua eneo la ufugaji wa samaki: 4.Ukaribu wa soko la samaki: Nivyema kujenga bwawa la ufugaji wasamaki karibu na soko la samaki, mbalina hapo basi kuwepo na miundombinu ya uhakika ili kuweza kuwasafirisha samaki hao hadi sokoni bilakuharibika. Hili ni muhimu sana hasapale unapokusudia kufanya ufugajimkubwa na kibiashara. Upatikanaji wa pembejeo: Upatikanaji wa vifaranga katika eneo lakaribu ni vizuri ili kupunguza vifo vyambegu za samaki wakati wa kusafirisha. Pembejeo nyingine ni pamoja na upatikanaji wa wa mbolea (samadi)lazima vizingatiwe kwani ni muhimu kwa urutubishaji wa bwawa wakati wautengenezaji wa chakula cha samaki. Miundo mbinu: Hakikisha miundombinu ya mawasiliano inapatikana,mfano simu, barabara na umeme hasakama unakusudia kufanya ufugajimkubwa. Nyenzo hizo

36

zitakusaidiakupata soko kwa haraka na kufikisha samaki sokoni kwa wakati kabla yakuharibika.

Ushindani: Ni vyema kuwajuawashindani wako katika ufugaji nanguvu waliyonayo kibiashara katikaeneo lako. Hii itakusaidia kujua kama mradi wako utakuwa na manufaa kibiashara. Aina ya mabwawa ya kufugiasamaki Kuna aina kuu tatu ya mabwawa yakufugia samaki na aina ya bwawa lipilijengwe hutegemeana na eneo la ardhikatika eneo husika.

Mabwawa ya kukinga mto: Mabwawa haya yanatengenezwa kwakujenga ukuta utakaowezesha majiusimama kwa kukinga kwa kukingakutoka mtoni au kwenye kijito kwaajili kufuga samaki. Mifereji ya kuchepusha mto hujengwa ili kuruhusu majiyapungue pale yanapokuwa mengi namengine huwekewa chujio sehemu yakutolea maji katika ule usawa unaohitaji ili maji yakifika pale yatoke bilakutoka na samaki.

Mabwawa ya eneo la mwinuko: Katika maeneo ambayo ardhi yakeni ya mwinuko, basi mabwawa ya aina hii huhitajika. Aidha, aina hiiya mabwawa huweza pia kujengwa katika mahali ambapo si pa mteremkolakini kwa chini sakafu yake huwa ya mwinuko. Maji huingia na kutokakwenye bwawa kwa njia ya mifereji au bomba.

Mabwawa ya eneo la tambarare: Mabwawa haya huchimbwa katika Minyoo hudhoofishaukuaji wa samaki

37

Mara nyingi imezoeleka kuwa wafugaji wanapoanzisha miradi ya samaki,jambo muhimu la kufanya ni kuwana maji, bwawa la kufugia, pamojana lishe, kisha kukaa kusibiri mavuno bila kufanya jambolingine lolote.Ni muhimu kwa wafugaji kufahamukuwa, samaki piah u s h a m b u l i w ana minyoo, jambo ambalo huzorotesha uzalishaji wa samaki hao. Unatakiwa kufahamu dalili za samaki kushambuliwa na minyoo kisha kuchukua hatua zinazostahili ili kuwanusuru samaki na kupata mavuno bora. Fahamu dalili za minyoo Dalili zipo nyingi na zinategemeana na aina ya minyoo aliyonayo samaki. Minyoo inayoshambulia matamvua na ngozi Tabia ya samaki hubadilika na huonyesha dalili za muwasho kama kujirusharusha na kujikwangua kwenye vitu. Rangi ya samaki hubadilia kuwa angavu mwenye rangi ya kufifia. Samaki hupumua kwa haraka huku akinyanyua mifuniko ya matamvua akiweka wazi matamvua yaliyovimba na angavu. Muonekano wa damu na majeraha baadhi ya maneo ya ngozi. Macho pia yanaweza kuathirika na kupoteza uwezo wa kuona. Vifo vingi vinaweza kutokea au wakawa na ugonjwa wa muda mrefu bila kufa.

Minyoo inayoshambulia ndani (matumbo) ❖ ❖ ❖ ❖

Uwepo wa majeraha au vidonda kwenye kuta za utumbo Minyoo huonekana kwenye tumbo lililovimba Minyoo pia yaweza kuonekana ikining’inia sehemu ya kutolea haja kubwa Kwa samaki wadogo ukuaji wao huwa hafifu

Inaweza kusababisha upungufu wa damu

Matibabu ya minyoo kwa samaki

38

Dawa za kutibu minyoo ya samaki kama ilivyo kwa wanyama wengine kama ng’ombe, mbuzi au kondoo inategemea aina ya mnyoo alionao samaki. Hivyo ni vizuri kuchukua sampuli ili kujua aina ya minyoo kabla ya kumpa matibabu. Minyoo aina ya Tegu: Praziquantelinafaa kwa samaki wa urembo tu na si kwa samaki wengine Minyoo wa tumbo: Levamisole (10mg/L) waoge kwenye maji yenye dawaInaendelea Uk. 8kwa siku tatu mful

KILIMO ENDELEVU (MAZINGIRA /MSETO) Kilimo endelevu ni kilimo kinacho zingatia mabadiliko ya tabia ya nchi na hali ya hewa. Kwa miaka ya usoni kumekuwa na mabadiliko ya tabia ya nchi (CLIMATE CHANGE ) inayo sababishwa na shughuli za kibinadamu na zingine sababu zisizo za kibinadamu na kupelekea kuongezeka sana kwa joto duniani, ukame, mafuriko, mingurumo, radi na matetemeko ya ardhi (EARTHQUAKE) na mambo mbalimbali ambayo kwa ujumla huwa na athari kwa mimea na viumbe hai wengine ambapo baadhi ya viumbe hushindwa kustahimili mabadiliko hayo na kupelekea wanadamu kubuni mbinu mbadala ili kusaidia kuishi maisha salama na yenye uhakika. Katika kukabiliana na hali ya hewa watu wanatumia “green house” ili kupunguza miale ya jua kupenya mojakwa moja na kuepuka madhara yanayotokana na kuharibika kwa “ozon layer” na utandawazi (GLOBALIZATION). Nilipo kuwa mwaka wa pili chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) nilikwenda mafunzo ya vitendo yaani field (FPT) ambapo pamoja na mambo mengine nilipata kujifunza namna kituo cha utafiti cha Arusha (TPRI) kinavyo fanya kazi na kujishughulisha na maswala ya viwatilifu, screen house, green house na tafiti mbalimbali kuhakikisha kilimo nchini Tanzania kinakuwa endelevu na kutunza mbegu za asili na mambo mbalimbali ya maabara na kisayansi ya kilimo na taarifa kwa biashara ndani na nje ya Tanzania likiwemo swala la vibali n.k. Kilimo endelevu pia hakiachi mbali kilimomseto. Hiki ni ni kilimo kinacho husisha kulima mambo mbalimbali kwenye eneo moja yaan mfano mazao ya kunde na mahidi au mazao mengine. Hii inasaidia kutunza shamba na kuongeza rutuba ya ardhi hiyo. Taasisi za kilimo hapa Tanzania ni pamoja na;❖ Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)

39

❖ Animal Disease Research Institute (ADRI) ❖ Mikocheni Agricultural Research Institute (MARI) ❖ Agricultural Research Institute KATRIN, IFAKARA. (ARI KATRIN IFAKARA) ❖ Agricultural Research Institute (ARI) UKIRIGURU ❖ Tanzania Pesticide Research Institute (TPRI). ❖ Tea Research Institute Maruku (TRIT) ❖ Tobacco Research Institute Of Tanzania (TORITA) 2. INDUSTRY AND ENERGY INSTITUTIONS ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖

Tanzania Bureau Of Standards (TBS) National Construction Council (NCC). National Housing And Building Research Agency (NHBRA) Tanzania Automotive Technology Centre (TATC) Tanzania Engineering And Manufacturing Design Organization (TEMDO) Tanzania Atomic Energy Commission (TAEC). Centre For Agricultural Mechanization And Rural Technology (CAMARTEC)

TAASISI ZA KIFEDHA Kwakuwa kilimo biashara kinahitaji fedha maranyingi, ni vyema kufahamu taasisi mbalimbali ambazo zinatoa huduma za kifedha nchini Tanzania ili iwe rahisi kuchagua taasisi inayo kufaa kwa uhitaji wa huduma yako. Zipo taasisi nyingi sana na zitaendelea kuongezeka mpya. Miongoni mwa taasisi hizo ni;1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9.

Access Bank Tanzania Advans Bank Tanzania Akiba Commercial Bank Amana Bank Azania Bank Banc ABC Bank M Bank of Africa Tanzania Bank of Baroda (Tanzania) 40

10. Bank of India (Tanzania) 11. Barclays Bank of Tanzania 12. Citibank 13. Commercial Bank of Africa (Tanzania) 14. CRDB Bank 15. DCB Commercial Bank 16. Diamond Trust Bank Tanzania 17. Ecobank 18. Equity Bank (Tanzania) 19. Exim Bank (Tanzania) 20. FINCA Microfinance Bank(Tanzania) 21. First National Bank of Tanzania 22. FBME Bank 23. Habib African Bank 24. I&M Bank (Tanzania) 25. International Commercial Bank 26. Kenya Commercial Bank 27. Mkombozi Commercial Bank 28. National Bank of Commerce (Tanzania) 29. National Microfinance Bank 30. NIC Bank Tanzania 31. People's Bank of Zanzibar 32. Stanbic Bank Tanzania Limited 33. Standard Chartered Bank 34. United Bank for Africa 35. UBL Bank Tanzania Limited 36. Mwalimu Commercial Bank Taasisi zingine za kifedha zilizo rasmi ni pamoja na:1. 2. 3. 4. 5. 6.

Covenant Bank For Women Efatha Bank Limited EFC Tanzania M.F.C Limited Kagera Farmers’ Cooperative Bank Limited Kilimanjaro Cooperative Bank Limited Maendeleo Bank 41

7. Mbinga Community Bank Limited 8. Meru Community Bank Limited 9. Mufindi Community Bank Limited 10. Mwanga Rural Community Bank Limited 11. Mwanza Community Bank 12. Njombe Community Bank Limited 13. Simiyu Community Bank 14. Tandahimba Community Bank Limited 15. Tanzania Mortgage Refinance Company 16. Tanzania Postal Bank 17. Tanzania Women's Bank Limited 18. Twiga Bancorp Limited 19. Uchumi Commercial Bank Limited Benki za Maendeleo 1. Tanzania Agricultural Development Bank 2. TIB Development Bank Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Na nukuu “Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuweza kuwezesha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuhamasisha taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwa wakulima. TADB imeanzishwa kwa madhumuni makubwa mawili ambayo ni: 1. Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania; 2. Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

42

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ilizinduliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wakulima nchini, mnamo tarehe 8 Agosti, 2015 mjini Lindi. Benki ilizindua utoaji wa mikopo tarehe 30 Disemba 2015 mkoani Iringa. Tarehe tarehe 8 Agosti, 2017 ilitimiza miaka miwili (2) tangu izunduliwe na takribani mwaka mmoja na nusu wa kutoa huduma kwa wakulima wadogo wa Watanzania ikiwa imefanikiwa kufanya yafuatayo: 1.2 MAFANIKIO YALIYOPATIKANA TANGU JANUARI 01, 2017 MPAKA KUFIKIA AGOSTI 31, 2017 1. Benki imeongeza kiasi cha mikopo kwa wakulima wadogo wadogo kutoka Shilingi 1.0 Bilioni hadi Shilingi 8.917 Bilioni; 2. Benki imeweza kukopesha kutoka vikundi 8 hadi kufikia vikundi 21, Taasisi moja ya Umma na Kampuni moja ya Maziwa; 3. Benki imekopesha wakulima 2610 kutoka wakulima 857; wanawake 910 na wanaume 1699; 4. Benki inaendelea kufanya uchambuzi wa miradi 17 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi 35.473 Bilioni; 5. Benki imeweza kuvijengea uwezo vikundi 672 vya wakulima wadogo wadogo vyenye jumla wa wanachama 91,684 kutoka vikundi 336 vilivyokuwa vinajumuisha wakulima wadogo wadogo 44,000 katika mikoa ya Iringa, Morogoro na Tanga. Hivyo kuwezesha jumla ya vikundi 19 kutimiza masharti na maandalizi ya msingi ya kuweza kukopa; Vikundi vingine vilivyobaki vinaendelea kupatiwa mafunzo ili viweze kufikia hali ya kuweza kukopesheka;

43

6. Kuwaunganisha wakulima wadogo 2,328 na wanunuzi kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya mahindi, mpunga, mboga mboga na miwa; 7. Kutoa mafunzo ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo kwa wafanyakazi ya zaidi ya 60 kutoka mabenki ya biashara na taasisi za kifedha nchini ili kuwaandaa kukopesha kwa ufanisi shughuli za kilimo. Mafunzo haya yaliendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TADB, Benki ya Taifa ya Kilimo na Maendeleo Vijijini India (NABARD) na Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF); 8. Benki imeweza kupata fedha zaidi za kukopesha toka Serikalini kiasi cha Shilingi 209.5 Bilioni na nusu yake tayari zimeshapatikana kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika; 9. Kuongeza wigo wa mikoa kwenye huduma kutoka mikoa sita (6) kwenda kwenye Kanda Nane (8) kwa utaratibu wa Kongani, na pia idadi ya mazao ya kipaumbele toka 14 kwenda 20 kulingana vipaumbele vya mikoa; 10. Kupanua wigo wa wateja toka vikundi vya wakulima wadogo wadogo pekee hadi makampuni binafsi na ya umma, miradi ya halmashauri za wilaya inayojiendesha kibiashara; 11. Kujumuisha viwanda vidogo vidogo na vya kati vya uchakataji na usindikaji wa mazao ya kilimo vyenye kuongeza thamani ya mazao; 12. Kuhuisha utaratibu wa kutoa mikopo na kusimamia utekelezaji kwa kuhusisha uongozi wa Serikali za Mikoa na Wilaya, Kata na Vijiji moja kwa moja na wadau wengine. 2.0 MIKAKATI WA KUJITANUA KUPITIA KONGANI Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria na kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika 44

kuleta

Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji wa fedha na sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini. Hivyo, katika kutekeleza mkakati wa kuwafikia wakulima wengi zaidi nchini Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imejipanga kutoa huduma kupitia Kongani nane (8) ili kuongeza tija kwa wakulima nchini. 2.1DHANA YA KONGANI NA MINYORORO YA ONGEZEKO LA THAMANI Tanzania ni nchi kubwa na yenye maeneo tofauti ya kimazingira/kilimo (Makundi) ambayo yana faida linganifu kwa ajili ya kuzalisha mazao maalum au seti ya bidhaa (mazao, mifugo, uvuvi). Kongani ni njia ya kimkakati ya kijiografia yenye kujikita katika shughuli za kilimo zinazohusiana, wasambazaji, na taasisi zinazohusishwa katika kujenga usawa wa moja kwa moja miongoni mwa wadau. Ni njia yenye kujenga fursa ya ushindani kwa njia endelevu. Upekee wa njia hii ni kuwepo kwa uhusiano na ushirikiano miongoni kwa mlolongo wa uongezaji wa thamani hasa katika makundi mbalimbali ya minyororo ya thamani, pamoja na taasisi na mamlaka za udhibiti zinazosaidia sekta ya kilimo. Ukaribu wa kitaasisi uchagiza uwezekano wa kurahisisha ushiriki na usambazaji wa maarifa na ujuzi ulio wazi na ule ujuzi usio wazi 3.0 HITIMISHO Kama ilivyo ada, Benki inatoa wito kwa wananchi hususan wakulima kuunga mkono kwa vitendo nia ya dhati ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwawezesha wakulima nchini kwa kuwapatia mikopo ya gharama nafuu inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania. Pia, wakulima wanaombwa kuwasiliana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kwa anuani na njia nyingine zilizoainishwa hapa chini ili kuweza kupatiwa maelezo ya kina kuhusu huduma zinazotolewa na jinsi ya kunufaika 45

na fursa zilizopo. Vile vile, TADB inayakaribisha mabenki mengine na wadau mbali mbali wa Kilimo kuchangamkia fursa zinazotolewa na TADB.”

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa Benki, Bw. Augustino Matutu Chacha (wapili kushoto) wakati wa Mkutano wao na Wanahabari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo. Kushoto ni Afisa habari Mwandamizi wa Idara ya Habari, Bw. Jonas Kamaleki na kulia ni Meneja wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa TADB, Bw. Joseph Mabula.

Vigezo vya kupata mkopo Benki ya CRDB 1. Uwe na shughuli/biashara rasmi…. hii inammanisha kuwa lazima uwe na leseni ya biashara, leseni hizi hutolewa na afisa biashara wa wilaya yako. 2. Uwe na namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN), hii itasaidia kudhibitisha kuwa wewe ni mlipa kodi 3. Uwe na dhamana, yaweza kuwa nyumba, shamba, kiwanja 4. Uwe na barua ya utambulisho toka serikali ya mtaa 5. Uwe na kitambulisho 46

6. Uwe na akaunti CRDB au benki nyingine yoyote. Kama una akaunti benki nyingine utatakiwa kupeleka taarifa ya akaunti yako (Bank statement). -Hizi ni mifano tuuu ya taasisi za kifedha watu wanaweza kukopa na kufanya kilimo biashara. Zipo nyingi sana japo masharti ya msingi yanaweza kufanana kwa sehemu . Mkulima akopesheke!!! 3. NATURAL RESOURCES INSTITUTIONS ❖ ❖ ❖ ❖

Tanzania Fisheries Research Institute (TAFIRI) Tanzania Forestry Research Institute (TAFORI) Tanzania Wildlife Research Institute (TAWIRI) Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA)

Sasa tuangalie fursa mbalimbali katika baadhi ya mazao yanayo limwa Tanzania;

KILIMO CHA MAZAO YA NAFAKA ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖

Mahindi Maharagwe Karanga Korosho Uwele Kunde Mtama Mpunga Ngano Mbaazi n.k

KILIMO CHA MAZAO YA BIASHARA ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖

Katani/mkonge Kahawa Migomba Pareto Maua Chai Pamba Korosho Tumbaku

47

❖ Miwa n.k

KILIMO CHA MBOGAMBOGA NA MATUNDA ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖

Maeple Nazi Machungwa Zabibu Nyanya Mnavu Karoti Maembe/miembe Mananasi Vitunguu maji Vitunguu saumu Mapapai/mipapai n.k

Kimsingi yapo mazao mbalimbali na kilimo cha aina mbalimbali isingewezekana kutaja vitu vyote. Mfano hatujataja Viazi, kisamvu, shayiri, mapera, mmapeasi mafenesi, machenza, limao, karatasi, mbao n.k.

Jedwali Na.1 Uzalishaji wa Mazao Makuu ya Biashara Tanzania

Zao

Kahawa

Uzalishaji (Tani)

Uzalishaji (Tani)

2005/06

2006/07

34,334

48,869

48

Badiliko (%)

42.3

Tumbaku

56,463

65,299

15.7

Chai

30,000

34,446

14.8

Pareto

2,800

1,500

-46.4

Mkonge

27,794

30,934

11.3

Korosho

77,158

92,232

19.5

Pamba

376,591

130,565

-65.3

Sukari

263,317

192,535

-26.9

Chanzo: Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

UFUGAJI Ufugaji wa Samaki ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖

Ufugaji wa Ngombe Ufugaji wa Nguruwe Ufugaji wa kuku Ufugaji wa njiwa Ufugaji wa kondoo Ufugaji wa mbizi Ufugaji wa Sungura n.k

Mgawanyo ulivyo ni kulingana na jamii na asili ya mimea au wanyama husika. Japo kuwa ni mtazamo tu, pia nivizuri ieleweke kuwa mazao ya biashara yanaweza pia kuwa ya chakula na ya chakula yanaweza kuwa ya biashara kwa njia tofauti na inategemea na zao husika na malengo ya mkulima. Mfano zao la mahindi, wapo watu wengi ambao wanalima mahindi kwaajili ya kupata chakula na wapo wale wanaolima mahindi kwa dhana ya ki-biashara. Yaani wapate kumuuzia mlaji au mnunuzi kwa faida. Maranyingi hasara ni kwa mlaji. Kwa sababu mfanya biashara atahitaji kurudisha gharama zilizo tumika na kupata faida ili naye ajipatie kipato. “PENDA KUWA MJASIRIAMALI”

49

Mjasiriamali ni mtu mjanja sana anawaza kujipatia faida endelevu na kubwa inavyo wezekana kwa wakati. Ana weza kubuni mbinu za kuongeza thamani kwenye bidhaa au huduma husika. Mjasiriamali wa mahindi anaweza badala ya kuuza mahindi jinsi yalivyo aka saga unga na kupakia vizuri kwenye viroba na kuweka alama yake(logo/trade mark) na vitu vinavyo fanana na hivyo. Hivyo mazao yote yanaweza kuwa ya biashara, ila sio mazao yote ya biashara yanaweza kuwa chakula mojakwa moja, japo fedha itakyo patikana inaweza kununua chakula.

50

SURA YA TATU NAMNA YA KUFANIKIWA KUFANYA BIASHARA YA KILIMO AU UJASIRIAMALI BILA MTAJI WA KIFEDHA. Mara nyingi watu wamezoea kuwa ili kufanya biashara ni lazima wawe na fedha za kuanzia yaani mtaji(capital). Ni kweli kabisa mtaji ni muhimu katika kuanzisha biashara au mradi fulani, lakini kwa kutambua kuwa wapo watu wanahitaji kufanya biashara lakini hawana pesa kama mtaji zipo njia mbadala ambazo ni kama ifuatavyo; Nguvu kazi Katika kuangalia nguvu kazi hapa watu wanatakiwa kama ni kilimo waende wenyewe shambani kuchukua jembe na kulima au kufanya shughuli zote zinazo husiana na kilimo husika hadi kuvuna. Mfano, kuandaa shamba, kupanda au kuotesha mbegu, palizi, kuweka mbolea hasa ile ya mifugo au ya majani(green manure) na shughuli nyingine zinazo husiana na utunzaji wa mimea iliyo pandwa au kuoteshwa hadi itakapo fikia wakati wa kuvuna. Baada ya kuvuna kuna kukausha au kuhifadhi kwa njia husika kasha kusafirisha na kuuza kwa mlaji wa mwisho kuzingatia aina ya mnyororo wa thamani uliopo. Vijana nivyema tuwekeze nguvu katika kilimo kwani shambani tutakula, tutakunywa, tutavaa na kuishi maisha bora kuliko kukaa tu mtaani kwenye vijiwe bila kazi ya kuingiza kipato. Maandiko mengine yanasema “tunawaandikia vijana kwasababu wana nguvu….” Kufanya ushirika na mwenye mtaji au shamba. Hii inafanyika sana maeneo ya vijijini ambapo mtu anaweza kumuona mzee mwenye shamba na kumuomba alime kwa muda fulani, au walime wote alafu apate chochote.

51

Baada ya hapo mhusika atakuwa ameshapata kianzio kama ni mbegu au pembejeo zingine kwaajili ya msimu unao fuata. Wazo la biashara. Wahenga wanasema, “akili ni nywele kila mtu ana zake”. Wazo lako ni mtaji wako. Mtu anaweza hana fedha yoyote ya kuanzisha shughuli ya kilimo au biashara ili kuji kwamua ki maisha lakini kutokana na wazo lake anaweza fika mbali. Je wajua? Ukiwa na wazo la biashara unaweza kufika kwenye taasisi ya kifedha kama benki mfano CRDB na kuwaeleza, kama wata jiridhisha na wazo lako wanaweza kukuambia uandike mpango wa biashara(business plan). Katika hili inahitaji ubunifu wa hali ya juu, ujuzi na wapo wataalamu wanao fahamu namna ya kuandaa mipango mikakati katika biashara hizo. Pia kwa Tanzania mojawapo ya watalamu hao ni kutoka chuokikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA ambao wanajihusisha sana na utafiti na uandishi wa mipango biashara kama hiyo(business plan) na ushauri wa kitaalamu(consultancy). Fikiria ninini kinahitajika katika soko, kwa kiasi gani na kwa wakati gani. Kisha tafuta nini unadhani unaweza kufanya na unakipenda toka moyoni, weka katika maandishi au onana na mtaalamu akusaidie mawazo na ushauri wa kitaalamu. Kutambua rasilimali zinazo kuzunuka na kuangalia namna ya kuzitumia Zipo rasilimali nyini sana ambazo zina tuzunguka, kama rasilimali watu, fedha, ardhi, maji, mifugo, samaki, mimea na wataalamu au wajasiriamali. Katika hili, nilazima kuangalia namna ya kutumia rasilimali hizo Mungu alizo tupatia kwa manufaa yetu na hata kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Kwa anaye ishi kijiji ambacho kimezungukwa na misitu, ipo fursa ya ufugaji wa nyuki hapo. Kwa sababu ufugaji wanyuki hauwezi kufaanyika mijini bali ni maeneo kama hayo, tusiiache misitu ikae tuu bila kuzalisha. Kuliko kuanza kulima kwenye misitu na kuchoma moto kwa kasi nivyema kufuga nyuki na kuendelea kutunza mazingira huku watu wakijipatia kipato na chakula au dawa ya asali. Vipo vitu vingine kama maji, kutokana na mazingira yetu na mabadiliko ya tabia ya nchi, tusikubali maji yapotee bure tu alafu mtu anashindwa kuanzisha hata angalau bustani ya mboga mboga na matunda pamoja na kupanda miti. Hizi zote ni fursa katika rasilimali zinazo tuzunguka. Kuunda vikundi na kuomba msaada wa pembejeo au namna nyingine kutokana na aina ya kikundi na uhitaji.

52

Mara nyingi umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Hivyo inakuwa ni rahisi vijana au kundi lolote katika rika liki unganisha nguvu zao katika kufanya jambo Fulani na wanapo kwama kuomba msaada kwa serikali, wadau na watu wengine kulingana na mpangilio husika. Zipo sheria, kanuni na taratibu za kufuata ili kuanzisha kitu kama hicho katika mtaa au kijiji husika. Sio tu kuanzisha kwa habari ya mambo ya kisiasa, ina tija sana pia kuanzisha vikundi hivyo kwa ajili ya maswala ya kiuchumi hasa ili kuinua kipato au ajira kwa vijana n.k. Msaada si lazima uwe wa kifedha, unaweza kuwa msaada wa kimawazo, ushauri, vifaa au fedha tasilimu pia ambapo uadilifu na uaminifu vitapima mafanikio ya kikundi husika. Uaminifu na nidhamu Naamini kuwa mtaji si lazima uwe fedha, tabia na mwenendo wa mtu katika maisha ni mtaji tosha wa kumsaidia kufanikiwa au kutofanikiwa katika jambo fulani. Kauli, uaminifu na mambo kama hayo kwenye biashara ni ya kuzingatia sana. Mjasiriamali aliye fanikiwa, ni lazima atakuwa anajua kuongea na watu vizuri, kuwasikiliza watu, kuwaheshimu watu, kuwajali na kuwaona kuwa nao ni binadamu na wanahitaji heshima, nidhamu na kila jambo ambalo ni jema. Hasa kwa wauzaji wa bidhaa, namna utakavyo mpokea mteja wako leo, ni mtaji tosha wa kukuletea wateja wengine wengi kesho au kukunyanyanya. Kwanza mteje akija, msalimie na mkaribishe vizuri kwa upendo na ucheshi. Muulize anahitaji nini? Akisha nunua muambie “KARIBU TENA”. Haya ni maneno madogo lakini mimi kama mjasiriamali na mkufunzi wa mambo ya uchumi, ujasiriamali na biashara nimejifunza na kuona wateja wana thamini sana kuthaminiwa kama kwa namna hizo. Kama mteja amesahau kitu mhifadhie vizuri akija mrudishie au umtafute inajenga ukaribu na uaminifu una imarika.

SURA YA NNE UJASIRIAMALI KWA UJUMLA NA KILIMO CHA KISASA Ujasiriamali unaweza kuelezwa kwa namna nyingi, kwa hapa maana ya ujasiamali ni kitendo cha mtu kutumia rasilimali zilizopo kama watu, ardhi, mtaji na rasilimali

53

zingine kuhakikisha anajipatia faida katika kuzalisha bidhaa au huduma na kwa utashi, weledi na ujuzi mkubwa alio nao mtu huyo. Kwa ujumla ujasiriamali ni hali ya kutumia ushawishi, ubunifu, akili ya ziada na

uwezo binafsi ilikufanikiwa kufanya jambo fulani katika maisha kwa kutumia vizuri fursa zilizopo. Mjasiriamali ni mtu yeyote anayefanya ujasiriamali. Mtu huyo anakuwa na mtazamo wa mbali sana katika kufikiri na kutafuta namna ya kuongeza kipato ama kupitia mnyororo wa thamani na kuongeza thamani za bidhaa au kuongeza uzalishaji na usambazaji wa bizaa husika au huduma au vyote kwa pamoja.

SIFA ZA MJASIAMALI ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖

Anakuwa jasiri Huchukua uamuzi mapema na sikusubiri tatizo likue na kuongezeka. Anakuwa ni mvumbuzi Mwenye uwezo wa kuona na kutumia vizuri fursa zinazo patikana. Mtazamo chanya Kuchukua hasara (risk taker)/ kuwa tayari kupambana na hatari yoyote. Mwenye kukubali matokeo Awe na afya njema na nguvu Anaye kubaliana na kushinda ushindani Anakuwa na ubunifu Mwenye kutaka faida Kuwatayari kupambana na hatari yoyote inayo jitokeza Mjasiriamali ni mtu mwenye maono na biashara au shughuli yake Ana ubunifu na kuchukua maamuzi Ni kiongozi, ni mtu mwenye ushawishi wa watu anaweza kutoa muongozo nini kifanyike au kuonyesha njia ambapo wengine hawaoni nyia ili kufikia malengo fulani.

MTAJI KATIKA UWEKEZAJI. Mtaji ni kitu chochote ambacho hutumiwa kuzalishiazaidi na au kuanzisha na kukuza kipato katika biashara. Kimsingi uwekezaji wa aina yoyote unahitaji mitaji mbalimbali kulingana na aina ya uwekezaji na bidhaa au huduma yenyewe. Ipo mitaji ya aina nyingi baadhi ni kama ifuatavyo:-

54

❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖

Fedha Vifaa Uwezo binafsi Bidha Zipo Namna mbili za kupata mtaji Kukopa Uwezo binafsi

KILIMO CHA KISASA. Ki msingi, kilimo ni shughuli ambayo inapo fanyika kwa kutumia mbinu za kisasa, teknolojia mpya, kufwata ushauri wa kitaalamu na mambo mengine unakuwa ni wenye tija zaidi na hapo ndipo watu wanakuwa matajiri kwa kujipatia pesa kutokana na ujasiriamali huo.

MAMBO YA KUZINGATIA Teknolojia Teknolojia ambayo inatumika huwa ni ya kisasa ili kuongeza uzalishaji, viwango na usanifu. Mfano, kutumia mipira kwenye kumwagiliaji (trip irrigation), green house, screen house, mbegu za kisasa(GMO) na mambo mengine ambayo hufanyika kufuata utaalamu, sayansi na utafiti ili kuboresha viwango katika mazao(quality assuarence). Watu wanashauriwa wawekeze kwenye kilimo kwa kujidhaiti ili kuweza kumudu gharama za uzalishaji, kuongeza thamani, bidhaa bora na hatimaye kujipatia faida iliyo nzuri ya kutosha.

Miundo mbinu Katika swala la miundo mbinu viko vitu vya msingi vya kuangalia kama vifaa, barabara, kama ni ufugaji kuwe na nyumba nzuri za kufugia au mabanda ya kisasa ya kulishia mifugo husika. Inaweza ikawa ni banda la kuku, banda la ngombe, mbuzi au kondoo. Ni lazima miundo mbinu itakayo saidia katika uzalishaji wa mimea au wanyama kuanzia uzalishaji, usafirishaji, kuchakata kwenye viwanda na kutoa bidhaa mpya na kuhifadhi (maghala) na haatimaye kumpatia mlaji wa mwisho katika ongezeko la thamani kupitia mnyororo wa thamani husika.

55

Uwezeshwaji au ufadhili Zipo taasisi za kifedha kama benki ambazo hutoa fedha au mikopo kwa wakulima. Mara nyingi ili mkopaji aweze kukopesheka I lazima awe mkulima rasmi, yaani awe amejisajili rasmi kuwa anafanya kazi hiyo. Awe anatunza kumbukumbu na mradi wake uwe unaasilimia kubwa ya kufanikiwa kutokana na anavyo jaili biashara yake hiyo, uzoefu, utaalamu au dhamana ya mali kwa ajili ya kulinda mkopo huo. Pakiwepo na uwezeshwaji au ufadhili kwa wakulima itakuwa ni rahisi wao kufanya kilimo chenye tija. Kwa kuwa wakulima walio wengi ni wale wanao tumia jembe la mkono na ni masikini kwa asilimia kubwa, ingebidi wapatiwe mikopo ya riba nafuu pamoja na ruzuku ili waweze kuendesha kilimo ambacho tuna kiita uti wa mgongi wan chi yetu, kutokana na umuhimu wake na mchango wake katika serikali, katika jamii na kwamba iwe iweje bila kilimo hakuna chakula na bila chakula watu hawata ishi. Ni kama ilivyo mtu asipokuwa na uti wa mgongo….” Kutumia mbolea Katika kilimo, udongo unachoka kadiri unavyo tumika hasa kwa kilimo cha zao moja kwa mfululizo. Katika hili, ili kuuongezea udongo rutuba wataalamu wanashauri matumizi ya mbolea. Hapa inategemea na aina ya udongo, kama udongo umepungukiwa madini ya urea basi mbole ya urea inahitajika itumike mahali hapo. Vivyo hivyo kama udongo umepungukiwa na base au aina nyingine ya madini basi madini husika yanatakiwa ya ongezewe kwenye udongo au kwenye mimea kupitia nyia ya kuspray kwenye majani n.k. Mifano mizuri ya mbolea ni kama; UREA, NPK, DAP na samadi (Organic na Inorganic). Kabla mkulima hajatumia. Kuongeza thamani ya mazao katika mnyororo wa thamani Kupitia kuzingatia usafi, kuhifadhi kwa matumizi ya baadaye kwa njia mbali mbali, kukausha, kulebo, kuweka kwenye mifuko au makopo safi,kusindika, kupeleka sehemu soko lipo. Kupitia njia tajwa, mkulima atakuwa amengeza thamani ya bidhaa kuliko kuiuza kama ilivyo toka shambani. Kuzingatia ushauri wa wataalamu na tafiti katika kuongeza tija Kutokana na ripoti ya HOTUBA YA WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA MHESHIMIWA STEPHEN WASIRA (MB.) KUHUSU

56

MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA KWA MWAKA 2007/2008,

“..ili kupata teknolojia sahihi zinazokidhi mahitaji ya kilimo na kuhakikisha kwamba matokeo ya utafiti yanawafikia wakulima, Wizara itaendelea kufanya utafiti wa mazao kama ifuatavyo:Kutathmini aina za mbegu mpya za mazao zenye tija kubwa, kustahimili ukame, zenye ukinzani dhidi ya magonjwa na visumbufu vya mimea na zinazokidhi viwango vya ubora na matakwa ya walaji wa ndani na nje ya nchi; Kubuni na kutathmini mbinu shirikishi za udhibiti visumbufu na magonjwa ya mimea na mazao; Kutathmini madawa asilia na ya viwandani yanayofaa kutumika nchini; Kusambaza matokeo ya utafiti uliofanyika; … Kutunza na kuzalisha mbegu mama za mazao ya jamii ya nafaka, mikunde na ya mbegu za mafuta na mazao ya jamii ya mizizi; Kuendeleza utafiti wa mazao ya bustani kwa lengo la kupata vipando bora; Kutathmini viwango vya matumizi ya mbolea vya sasa kwa lengo la kutoa mapendekezo ya viwango sahihi kulingana na hali ya udongo, hewa na aina ya zao linalozalishwa katika eneo husika; Kuzalisha na kusambaza miche bora ya chai 9,000,000 na kahawa miche 10,000,000 kupitia taasisi za utafiti za TRIT na TaCRI kwa wakulima na vikundi vya wakulima”. Kutokana na ripoti hiyo, ningependa kusisitiza kwenye swala la kutumia teknolojia zinazo endana na mabadiliko ya tabia ya nchi kama, ❖ Kilimo chaumwagiliaji (Matone na aina zingine za umwagiliaji) ❖ Green house na screen house

57

❖ Kilimo cha matuta ❖ Kutumia mbegu bora ❖ Kulima kilimo cha biashara kwa tija na faida zaidi mfano (kutunza kumbukumbu, kuangalia soko na kuongeza thamani kwa njia mbalimbali).

58

SURA YA TANO MCHANGO WA SERIKALI KUINUA UCHUMI WA MKULIMA, BIASHARA NA UJASIRIAMALI. Yako mambo mengi kimsingi ambayo serikali ndiyo inawajibu, jukumu na inafanya kuhakikisha wakulima, wajasiriamali na wakulima wanapata mafanikio katika shughuli zao. Ni pamoja na kudhibiti bei ya wanavyo viuza au kuvizalisha (maximum or minimum price), kuweka mazingira rafiki kwa wananchi hao, kutengeneza miundo mbinu bora kwaajili ya kusafirishia bidhaa mfano: Barabara, reli, bandari, masoko n.k. Kwahiyo, madhumuni ya serikali ni kuhakikisha maingira bora ya wakulima kama mashamba ya kulima kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji kwa mfano, biashara kudhibiti uingizwaji holela wa bidhaa bila kuzingatia sheria, kanuni na taratibu ili kulinda wazalishaji wa ndani ususani viwanda kama viwanda vya sukari kama inavyo fahamika. Pia wajasiriamali ni nguzo ya msingi sana katika taifa kwenye uchumi kuongeza kasi ya uzalishaji, kutengeneza ajira, kupunguza au kuondoa umaskini na mambo mengine kama hayo. Hivyo ni bora masomo, semina, makongamano na motisha mbali mbali zitolewe kwa wa-Tanzania hasa vijana kwasababu ndio wenye nguvu na ni taifa la leo na kesho kuhakikisha wamejengwa katika misingi ya kufanya kazi na kuepuka uzembe au uvivu. Ama kwa hakika kwa mtu mwenye nguvu akiwa maskini amejitakia. Unamkuta mtu anazonguvu, badala ya kwenda kulima huko vijijini anakuja mjini na kuwa ombaomba? Hii ni sahihi kweli??. Kazi ni kazi tuondoe mitazamo hasi kuwa wakulima ni watu wa kudharaulika, unaweza kulima pia hatakama umesoma. Unaweza kufanya hivi, tafuta soko la bidhaa Fulani, alafu nenda vijijini uwaelimishe wakulima namna ya kulima na hatua zote za uzalishaji, simamia viwango na ubora alafu nunua mazao yao na umuuzie mnunuzi huko aliko, tayari na wewe ni mkulima au mjasiriamali wa kilimo –biashara. Baadaye ukipata mtaji mzuri na kuongeza thamani ili kuongeza bei ya bidhaa tayari utakuwa umefika mbali ndugu yangu unayesoma na kuguswa na wazo hili.

59

Wazo ni pesa. Tumia mawazo kuzalisha pesa, pesa uitumie kuzalisha pesa sio wewe ufanye kazi kutafuta pesa tuuu… Huo ni mtazamo wa kijasiriamali kama unataka usije kufa masikini.Taasisi na wadau wengine ni nguzo muhimu sana katika kusimamia na kuhakikisha shughuli hizo zinafanikiwa kwa ufanisi mkubwa.

60

SURA YA SITA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA KILIMO Vijana wengi wanapenda na kutumia mitandao ya kijamii kama vile face book, watsap, twiter, instergram n.k. Mimi nikiwa mmoja wao. Pamoja na kupenda kutumia mitandao hii ya kijamii kwa mawasiliano, kuchatt, kujifurahisha na kujifunza mengi, mitandao hii inaweza kuwa fursa ya kilimo biashara. Katika kutambua tatizo kubwa la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, “KILIMO NI AJIRA MBADALA”. Mkulima anaweza kutangaza biashara yake, mfano ”mazao” au “mbogamboga”kwa kupiga picha na kutoa maelezo anauza kwa bei gani, ana patikana wapi na ki-vipi na anauza nini hasa, mathalani namba za simu zinzweza kuwa msaada mkubwa. Ni kwa sababu taarifa ndio kila kitu katika mafanikio. Ni ushauri wangu kwa vijana waitumie vizuri mitandao ya kijamii kwa maendeleo na kwa kutimiza ndoto zao. Mitandao ya kijamii ni pamoja na matumizi ya simu za mikononi kama “smart phones”, “laptops” na vifaa vingine hasa vya kidigitali kutumia mtandao yaani internet. Pia vyombo vingine vya mawasiliano kama redio, television, magazeti na makala mbalimbali au vitabu vinaweza kumpatia mtu taarifa kuhusu bei za mazao, sehemu zinapo patikana na mbegu za mazao pamoja na masoko. Tanzania kwenye kilimo hatufanyi vizuri sana, sababu mojawapo ni kukosa taarifa sahihi kwa wakati na maarifa au utaalamu katika kuongeza tija. Japo wapo wataalamu wa kilimo, lakini bado wakulima wengi hawazingatii ushauri wa kitaalamu na kulima kisasa na mpango maalumu bali walio wengi wanalima kwa mazoea. Tukizingatia kwamba wakulima na watu wanaotegemea kilimo ni wengi sana Tanzania, ni zaidi ya 65% ya idadi ya watu. Hivyo hata wataalamu waliopo hawatoshi au sio wakulima wote wanapata ushauri huu wa kitaalamu. Jitihada binafsi ni muhimu ili mtu kupata tija katika kilimo. Njia moja wapo ya kujipatia ujuzi ni kupitia maarifa kwa kusoma na kuwa watafiti kuhusu kilimo husika. Wengine wanafanyaje? Kuhudhuria kwenye maonyesho mbalimbali ya kitaifa,

61

kuuliza kwa wataalamu, kuchukua namba zao, kutaka kubadilisha maisha na kuongeza tija. Kwa uchunguzi niliofanya katika mitandao ya kijamii, yapo makundi mengi sana ya kiujasiriamali yameanzishwa, ya facebook, ya wattsap ambapo watu wanajadili kilimo, ufugaji, ujasiriamali na namna mbalimbali za kujikomboa. Biashara za mtandao zimeshamiri katika karne hii ya kidigital, watu wana uza na kununua kwa kupitia mtandao, soko kubwa linapatikana mtandaoni, niswala la mtu kuchukua fursa ya mtandao na kuimarisha au kufanikisha biashara zako. Ufuatao ni mfano bora wa mtandao unaowaunganisha wakulima, wataalamu wa kilimo na watu mbalimbali hasa vijana kwa asilimia 70%. Katika kutumia mitandao ya kijamii ili kupata taarifa sahihi na kwa urahisi zipo namna nyingi lakini Tanzania Institutional Economics Development Foundation (TIEDF) inatoa taarifa kwa kushirikiana na majukwaa na wadau wengine wa Kilimo, Ufugaji na kadhalika. Mojawapo ya wadau tunaoshirikiana nao ni KILIMO FORUM (KF).

KILIMO FORUM. Hili ni jukwaa linalo jihusisha na maswala ya kilimo, hivyo mtu anaweza pata taarifa mbalimbali kuhusiana na kilimo. Mathalani, wataalamu mbalimbali, wakulima, kuunganishwa na watu wa masoko na kurahisisha mafanikio katika kilimo biashara. Wasiliana nao kwa, Simu: +255 684 891 717 au +255 714 085 617 .Pia kwaBarua pepe(email): [email protected] wasiliana nao. Ushauri: Wajasiriamali na wakulima wawe na “network” yaani mtandao na wadau wanaofanya jambo husika yaani iwe kwa simu au namna nyingine. Taarifa na maarifa sahii hujenga uwezo na ujuzi ambao ni hekima ya maendeleo ya mtu huyo. Pata taarifa sahihi kwa muda sahihi na fanya jambo sahihi (“Do the right thing….”)

62

SURA YA SABA USHAURI WA KITAALAMU KWA UJUMLA KUHUSU KILIMO UCHUMI NA BIASHARA. Ni mambo mengi watu wanaweza kufanya ili kufanikiwa katika maisha. Chamsingi ni kupenda, kuthamini na kuwa na bidii katika maarifa sahihi ujuzi na ubunifu kufikia malengo tarajiwa. Ki msingi uchumi wa mtu ili ukue nilazima kufuata kanuni na mbinu za kiuchumi. Mfano mtu apatapo fedha, utajiri wake hauta pimwa kwa hizo hela zilizopo, bali nidhamu na maisha endelevu kuhakikisha fedha ipo na inatengenezwa kujipatia mahitaji ya kilasiku. Watu wajifunze kuweka bajeti, kuweka kumbukumbu ya mapato na matumizi ili kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima na kuongeza kipato kwa kubuni njia tofauti za kuongeza kipato. Kwa mtu aliye ajiriwa ningeweza kumshauri asitegemee mshahara tuu, bado anayo nafasi ya kuanzisha biashara mathalani kilimo biashara akawa anatoa ajira kwa wafanya kazi hao, huku naye akiongeza kipato na uchumi kwa ujumla. Swala la kilimo ni la kila mtu, wapo wanaolima, wanao nunua na wanao tumia. Hivyo ni lazima kuweka nguvu kubwa kwenye maeneo muhimu kama hili la kilimo kwasababu ukiwa na chakula utakuwa na maendeleo. Huwezi kulima ukiwa na njaa, huwezi kusoma ukiwa na njaa, huwezi kuwa mbunifu ukiwa na njaa na huwezi kuwa na amani au furaha ukiwa na njaa. Msanii mmoja aliwahi sema, “KULA LAZIMA KUOGA HIARI”. Kuhusu Soko la Ajira na Fursa za Kilimo. "Mazingira ya kujiajiri bado ni magumu kwa Tanzania, na kama hatujajipanga kuwa na sera nzuri za kutengeneza uchumi rafiki na mazingira mazuri ya biashara na ajira, hali itaendelea kuwa mbaya zaidi hasa kwa vizazi vijavyo; jambo ambalo mimi binafsi sipendi liwatokee watoto wetu baadae. Soko la Ajira: "Takwimu nilizonazo mpaka sasa zinaniambia kuwa kila mwaka vyuo vyote Tanzania vinatoa wahitimu zaidi ya Milioni 1.2 na zipo dalili za idadi hii kuongezeka katika ngazi zote za elimu. Kati ya hao wastani wa wahitimu 200,000 tuu ndio wanapata fursa ya kuajiriwa(sawa na wastani wa 20-25%) kundi lililobaki linaingia katika ajira zisizo rasmi na lingine wanakosa ajira kabisa kwa kipindi cha

63

mwaka mmoja. Tatizo ni kubwa na si Tanzania tuu, hili ni tatizo la nchi nyingi duniani hata zile zilizoendelea. Unemployment rate ni 12%(2015) Tanzania, wenzetu Kenya ni 14% na nasikia imepanda hadi 18% sasa hivi, Tukumbuke kuwa serikali haiwezi kuajiri kila mtu, hivyo ubunifu na ujasiliamali kwa vijana wa Leo haukwepeki, lazima vijana tujiamini na kujituma, kutumia vipaji, nguvu na uwezo wetu kukuza vipawa vyetu. Na serikali pia iwekeze katika kukuza na kuendeleza ubunifu (Creative industry) wa vijana. Pia Vyuo vyetu viangalie mfumo wa ufundishaji, Tumekua tuna"Teach" zaidi (Nadharia) badala ya Ku"Train" (Vitendo), chakula kizuri kinatengenezwa kuanzia jikoni, hivyo turekebishe namna ya kuwafundisha/kuwapika vijana wetu kwanza vyuoni, wasipate elimu ya kuajiriwa peke yake. Tatizo la Mitaji/Mikopo: "kuhusu mitaji ni kweli nakiri kuwa limekua changamoto. Lakini tusilaumu mabenki na taasisi nyingine za kifedha, Tukumbuke mabenki nao wanafanya Biashara, hawawezi kukopesha kila mtu, lazima waangalie sifa stahiki za kukopesha ili wawe na uhakika wa faida ya riba itakayopatikana kutoka kwa mkopeshwaji, wanaweka Sera zao kulingana na hali ya uchumi wa nchi husika, Riba za mabenki ya Marekani ni ndogo kufananisha na zetu maana nchi zao zina uchumi mzuri na mazingira mazuri ya Biashara hivyo mabenki yanaweza kutengeneza faida na kukopesha zaidi kutoka na mfumo na mazingira mazuri ya biashara kuliko sisi (US Federal Lending Interest Rate ni 6-8%), China inacheza kwenye asilimia 5%, Lakini Tanzania Riba ni kuanzia 8-21% wastani wa mabenki yote, tatizo ni uchumi wa nchi na mazingira ya Biashara, Leo CRDB akipunguza riba toka 20% hadi 10% hata pata faida. Hivyo tusilaumu mabenki, Jukumu la serikali ni kutengeneza mazingira mazuri, tujenge uchumi wetu. Lakini taasisi za fedha hazitoi mtaji kwa "wanaoanza" Biashara, wanatoa mtaji kwa "aliyeanza" Biashara, kwa hiyo nawashauri vijana waanze kidogo, lakini wawe na nidhamu ya Pesa, kuweka kumbukumbu za Biashara ili taasisi hizi ziwafikirie baadae kuwakopesha. Lakini pia nawachallenge management za mabenki, Je, wamefanya nini hadi sasa kuhakikisha wanalifikia soko la wajasiliamali ambao hawakopesheki ili watengeneze soko jipya la mitaji. *Ningeshauri watu wajiunge na vikundi, taasisi au mitandao ya kutoa elimu, taarifa juu ya kilimo, masoko na kadhalika. Namshukuru mungu mwaka 2015 nilianzisha ukurasa wa facebook “Tanzanian Young Economists” nilikuwa na shauku ya kuwaunganisha wachumi wa Tanzania kujadili namna ya kuinua uchumi wa taifa letu kwa kutumia vizuri rasilimali tulizo nazo. Nilifanikiwa kuwaunganisha watu mbalimbali na kuwa tunajadili na kupeana

64

fursa mbalimbali hasa za ki-uchumi kutoka ndani na nje ya Tanzania. Mnamo mwaka 2017, ilionekana tubadilishe jina la taasisi hiyo tuite “Tanzania Institutional Economic Development Foundation (TIEDF)” kwa kuwa ili uchumi ukuwe unahitaji taasisi imara na mapinduzi ya ki-uchumi kwenye kilimo, biashara, utalii, uchimbaji madini, viwanda nakadhalika kwa kuongeza tija na thamani. Hivyo ni rai yangu watu kuwa na tamaduni za kubadilishana uzoefu, ujuzi, fursa na elimu juu ya kilimo na sekta zingine ili kuboresha maisha ya wananchi.

65

SURA YA NANE UHUSIANO KATI YA KILIMO NA VIWANDA KWA NCHI KAMA TANZANIA. Hakika kuna uhusiano mkubwa sana uliopo kati ya sekta ya kilimo na sekta nyingine kama sekta ya viwanda hasa kwa nchi zinazo endelea, hata nchi zilizo endelea pia. Ni ukweli usio pingika kuwa kilimo kinategemewa sana katika kuwezesha viwanda kufanya vizuri na viwanda vinategemewa sana pia ili kuinua sekta ya kilimo kwa kuchakata bidhaa ghafi na kuongeza thamani na kupatia wakulima soko kubwa na la uhakika. Kwakuwa soko ni kitu muhimu sana kwa mkulima na mfanya biashara yeyote, ni muhimu basi kupenda wateja wetu ambao ni viwanda na wateja binafsi wanao nunua mazao au chakula kwa ajili ya biashara na matumizi binafsi kulingana na aina ya mazao, mazingira na wakati au malengo ya mnunuzi.

Fig 1. Kukua kwa Viwanda

Kukua kwa kilimo Mchoro hapo juu Fig 1. Unaonyesha kuna uhusiano chanya kati ya kukua kwa viwanda na kukua kwa kilimo. Kadiri viwanda vinavyo kuwa vingi na kufanya kazi zaidi ndipo watu wengi wanaweza kukuza kilimo kwa kutumia fedha au kipato cha kiwandani kununua pembejeo za kilimo na kulima kilimo cha biashara na kuachana

66

na kilimo cha mazoea. Pia kwa kupatikana soko la uhakika wakulima wataweza kuwekeza kwa kilimo cha kisasa kwakuwa kitawalipa na kina tija kwa kuwepo kwa soko. Mambo ya kufikirika katika mchoro hapo juu (assumptions). Wafanyakazi hawataacha kilimo kwasababu wanafanya kazi kwenye viwanda au makampuni mengine. Kilimo kinategemewa kupatia viwanda malighafi kwaajili ya kuchatwa kutengeneza bidhaa mpya au kuongeza thamani. Kuna sekta mbili, Viwanda na Kilimo. Kilimo kina nafasi kubwa sana katika kukuza viwanda nchini Tanzania. Kilimo kikiwa cha tija kinacho zalisha na ziada, ndio mafanikio ya viwanda. Viwanda vingi vinategemea malighafi toka mashambani, mathalani viwanda vya sukari, nguo, kahawa, chai n.k mathalani katika ulimwengu wa sasa. Kulingana na ongezeko la watu duniani, inasemekana chakula kitakuwa mali adimu kadiri watu wanavyo ongezeka na mabadiliko ya tabia ya nchi. Kufikia mwaka 2050 watu wanategemewa kufikia Billion 9 kutoka billion 7.5 kwa 2017, ambapo chakula kinatarajiwa kuwa na ongezeko la mahitaji kwa zaidi ya asilimia 70%.

Mambo ya kufanya kuboresha kilimo nchini Tanzania. Kuanzisha mifumo ya umwagiliaji kudhibiti tatizo la ukame na matumizi ya maji. Kuanzisha mashamba darasa kila mkoa kulingana na mazingira na uhitaji Kutoa elimu kwa vitendo kwa wakulima namna ya kulima kwa faida, kilimo biashara. Kutengeneza mazingira rafiki kwa wakulima kupata soko la mazao yao ndani na nje ya nchi. Sekta binafsi kupewa kipaombele na serikali katika mikataba na uwekezaji. Serikali kusimamia na kubuni miradi ya kilimo itakayo wanufaisha wadau walio wengi ki-uchumi. Kutumia wataalamu waliopo vizuri na au kuongeza wataalamu au kuwaongezea ujuzi kulingana na mabadiliko ya teknolojia(Tehama).

67

Kutumia nguvu kazi kubwa ya vijana wa mtaani kuwekeza kwenye kilimo kwa wingi hii itapunguza tatizo la upungufu wa ajira na uhalifu unaofanywa na vijana wanapo kosa kazi (ajira). Kuwapa watu changamoto ya ushindani na fursa zilizopo, namna ya kufanikiwa katika maisha. Hii inaenda sambamba na kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa makundi tofauti tofauti katika jamii na kuwajenga ki-mawazo, fikra, ujuzi na hasa kuwa wajasiriamali. Kuinua na kukuza vipaji kwa vijana na watoto wadogo, ili wanapo kuwa watu wazima wawe na uwezo mkubwa wa kufikiri namna ya kufikia ndoto na malengo yao ya msingi. Mfano mzuri ni kuanzisha na kuboresha academy za michezo. Michezo inasaidia watu kiafya na wanaweza kufikiri vizuri namna ya kuendesha maisha yao baada ya kuliwaza na kupata muda wa ku-“relax”. Uwekezaji katika kilimo kuwa kwa kiwango kikubwa (kilimo biashara).

68

SURA YA TISA UTAFITI Nilifanya utafiti mbalimbali ukiwemo utafiti wa matumizi ya maji kwenye kilimo cha miwa kwa wakulima wa Miwa bonde la Kilombero na Kiwanda cha Sukari mwaka 2017. Utafiti ulionyesha kuwa wakulima wadogo wengi hawamwagilii bali wanategemea mvua za misimu. Mathalani, kampuni ya sukari yenye mashamba ya Nyamvisi, Msolwa, Ruembe, Ruaha, Simba na Magombera kwa pamoja yakiwa na ukubwa wa takribani hekari 10,026hawategemei mvua tu, bali wana miundombinu ya umwagiliaji (irrigation). Pia ilionekana kuwa wakulima wa nje hawavuni kwa tija (waliowengi) kwasababu mbalimbali zikiwemo kukosekana kwa matunzo mazuri kwasababu ya umaskini unaosabisha waliowengi kushindwa kumudu gharama za mbolea, madawa na huduma mbalimbali katika kuhakikisha tija kwa kilimo cha miwa.Swala la soko sio tatizo sana kwa kuwa wanauhakika wa kuuza miwa kwa kiwanda cha sukari cha Kilombero. Japo kuwa miwa ya wakulima wa nje(Outgrowers) haistawi sana kama miwa inayolimwa na kampuni ya sukari, ila miwa ya wakulima wa nje inakiwango cha chuu zaidi cha sukari(sucrose) kutokana na sababu mbalimbali kama maji ya msimu na kutotumia zaidi madawa ya kemikali ukilinganisha na kilimo cha kampuni. Aina za miwa zinatofautiana katika kiwango cha Sukari na tija kwa ujumla. Mbegu nyingi zipandwazo kwenye bonde la kilombero hasa kwa upande wa kampuni zinatoka Afrika Kusini. Nikiasi kidogo tu cha mbegu za miwa ambayo hutoka Tanzania (ya asili). Wengi wanaofanikiwa wanazingatia mafunzo, utaalamu, ujuzi na kanuni bora za kuanzia upandaji, ukuzaji, uvunaji na utunzaji hadi usafirishaji na kufikisha mazao kwa soko. Pia kufanikiwa katika kilimo cha biashara ni kuwa na uwezo wa kukopesheka, hivyo kwa wale wakulima ambao hawajakidhi vigezo vya kukopeshwa na taasisi za kifedha inakuwa nivigumu kustawisha mashamba au biashara zao. Hata hivyo kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ingekuwa vyema wakulima kuwa na mbinu mbadala na kuacha kilimo cha mazoea cha kutegemea mvua. Hapa

69

tunazungumzia umwagiliaji, kulingana na gharama za kutokuwa na umwagiliaji kuwa kubwa hasa kutokana na ukame. Ni vyema kuwa na kinga kuliko tiba, inawezekana. Kwa ujumla ardhi na bonde la Kilombero ni zuri kwa kilimo cha mazao mbalimbali na Morogoro kwa ujumla kwa kuwa mkoa wenye maji mengi ya kutosha na hali ya hewa nzuri kwa mazao kukua haraka kutokana na joto napia urahisi wa kufikia soko kama mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Dodoma na mikoa ya kusini mwa Tanzania. Hivyo kupitia utafiti huo niligundua kuwa Morogoro ni mojawapo ya mikoa yenye fursa nyingi za Kilimo, ufugaji na viwanda katika kuongeza thamani kupitia mnyororo wa thamani (value chain).

Utafiti wa ngombe wa Kisasa na Nguruwe Katika kutafuta taarifa sahihi na za msingi ili kuandika kitabu hiki nilitembelea sehemu mbalimbali, ilibidi kuongea, kuhojiana na kuwadadisi na wadau wa kilimo hasa wakulima, ili nijue ni changamoto gani wanakumbana nazo namimi nitafute majibu ya maswali yao na kutoa ushauri wa kitaalamu ikiwa ni pamoja na kusoma maandishi mbalimbali kama vitabu na tafiti nyingi kuona wataalamu wamefanya nini na nini kinaweza kufanyika ili kuongeza thamani, tija na faida kwa wakulima na wafanya biashara.

Hawa ni ngombe wa kisasa wanakula majani makavu(SUA Farm). Katika kuhojiana na wanaolisha ngombe hao, ilionekana kuwa, ili ngombe watoe maziwa mengi na yakutosha kuna wakati wanapelekwa malishoni porini na wanaenda kwa shift, wakirudi wanaendelea kula kwenye banda majani yaliyo andaliwa vizuri na nimakavu kama yanavyo onekana kwenye picha.

70

Zipo sababu nyingi ngombe kutoa maziwa mengi au kidogo, hasa kulingana na aina ya chakula na je wanashiba? Jambo lingiine ni aina ya ngombe, hali ya hewa, magonjwa n.k. Kwa kuwa nilibahatika kukutana na mtu kutoka kitengo cha ufugaji nchini Israel nilimuuliza aniambie maziwa wanazalishwa kiasi gani cha lita kwa siku, ni lita sitini (60) hadi tisini (90) lita za maziwa kwa ngombe mmoja kwa siku. Anakamuliwa kwa siku mara tatu, hivyo anaweza kutoa maziwa kiasi cha lita 30 kwa mara moja. Asubuhi lita 30, mchana lita 30 na jioni(usiku) lita 30 jumla lita 90 kwa ngombe mmoja. Hawa wanafanya vizuri zaidi kulinganisha na wale wa Ki-Tanzania ambao nilivyo hoji ni lita tatu hadi tano kwa ngombe mmoja. Chakula ni jambo la msingi sana, ukizingatia lishe bora maziwa yatakuwa mengi na yenye ubora unao hitajika. Kwa ushauri zaidi wasiliana na wataalamu wa mifugo na kilimo waliopo karibu yako au unao wafahamu utapata ushauri zaidi.

Ngombe wanakamuliwa kwa kutumia mashine za kukamulia (SUA, Mazimbu Farm), picha ya pili inaonyesha majani yaliyo kauka ambayo ni chakula cha mifugo, huandaliwa na kuhifadhiwa vizuri ili kutumika hasa wakati wa ukame. Kimsingi, kuna makundi mawili ya ng'ombe kuna wa nyama pamoja na wamaziwa. na kuna aina nyingine pia ni wazuri kwa nyama pamoja na wamaziwa mfano mpwapwa na sahiwal. Hizi ni aina za ngombe wa maziwa:

71

❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖

Holstein Friesian Brown swiss Ayrshire Guernsey Jersey Mpwapwa Sahiwal Red poll

MAMBO YA KUZINGATIA KWENYE UCHAGUZI WA NG'OMBE MZURI WA MAZIWA Umbo : siku zote ngo'mbe wa maziwa anatakiwa awe na umbola pembe tatu, humpless pia awe na miguu imara pamoja na tumbo kubwa kwa sababu ng'ombe mwenye tumbo kubwa anaweza kula sana na kutunza chakula kingi.na chakula kingine kinabadilishwa na kua maziwa.hivyo ng'ombe mwenye tumbo kubwa anauwezo wa kutoa maziwa mengi sana. Kiwele na chuchu: siku zote ng'ombe mzuri wa maziwa anakiwele kizuri kimeshika vizuri kwenye mwili na kiwele kizuri hua kinabonyea kama spongy.na pia kiwele na chuchu vinatakiwa kua kubwa. Rangi ya mwili: sikuzote ng'ombe mzuri wa maziwa anarangi moja au mbili tu kwenye mwili wake e.g brown, red white and black. Asili : siku zote ng'ombe mzuri wa maziwa anatokea katika maeneo yenye hali ya hewa ya kati e.g Holland, Switzerland, Scotland and other part of Europe and Asia.

AINA ZA NG'OMBE WA MAZIWA NA SIFA ZAKE Holstein friesian Hii ni aina ya ng'ombe wa maziwa ambayo ni kubwa kuliko aina zote SIFA ❖ Asili yake ni Holland ❖ Wanamabaka meupe na meusi ❖ Maziwa yao yana mafuta kiasi cha 3.5%

72

❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖ ❖

Hawa wanatoa maziwa mengi 6000 liters kwa kila msimu wa kukamua Watoto wake wanazaliwa wakiwa na 40 kg na zaidi. Ngombe jike anauzito wa 400-600kg na dume 600-1000kgs Brown swiss Hii ni kati ya aina za zaman sana, ili gunduliwa katika milima ya Switzerland? SIFA ZAKE:Wame gunduliwa Switzerland Hii ni aina nzito inayo fuata baada Friesian Wanalangi ya brown inayo koza Niwapole Uzito wa jike 450-550kg na dume 600-900kgs

❖ Ayshire ❖ Hii ni aina kubwa inayo fata baada yaFriesian na brown Swiss ▪ SIFA ZAKE: ❖ Niwakubwa zaidi ya jersey na Guernsey ❖ wanarangi nyekundu kuelekea mahogany mchanganyiko na nyeupe ❖ asili yao ni South west Scotland ❖ maziwa yao yanamafuta 4% ❖ wanachuchu na kiwele kizuri sana ❖ Guernsey ❖ ❖ ❖ ❖ ❖

▪ SIFA ZAKE: wanatoa maziwa yenye langi kama ya dhahabu wanarangi nyeupe na nyekundu maziwa yao yanamafuta 4.5% wanatoa maziwa 4200litres kwa msimu mmoja wa kukamua uzito wa jike 450-500kgs na dume 600-700kgs

Jersey ❖ Jersey hii ni aina ndogo kuzudi zote.

73

SIFA ZAKE: ❖ ❖ ❖ ❖

Hawa asili yao ni visiwani kati ya UK na France Jersey maziwa yao yanamafuta kuzidi wote 5% Jersey wanarangi ya “blackish brown” Jersey uzito wa jike 400-450kg dume hadi 500-600kgs.

UKUZAJI WA MICHE YA MITI YA MATUNDA.

74

Katika kuendelea kukusanya taarifa mbalimbali kuhusu Kilimo biashara, nilifanikiwa kutembelea idara ya Shamba Kitalu cha miti ya matunda, chuo kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA). Wanazalisha miti ya matunda na aina mbalimbali kama michungwa, miembe, mipapai, miparachichi, michenza na aina nyingine nyingi ambapo wanatumia utaalamu kuzalisha aina bora na za kisasa zinazo endana na

75

mabadiliko ya tabia ya nchi. Kwa kuwa soko la matunda linakuwa kwa kasi, ni fursa mojawapo niliyo iona kwenye kilimo.

UFUGAJI WA NGURUWE Hawa ni moja kati ya wanyama wenye faida sana. Pamoja na uzoefu wa kufuga nguruwe kwa muda Fulani, nilijifunza na bado najifunza namna ya kufuga kisasa. Ndugu Imani Lubaba alielezea kwenye makala yake kama ifuatavyo, …“Ufugaji wa Nguruwe ni lazima uwe wa kisasa ili kupata nguruwe bora. Jamii nyingi hapa Tanzania huchukulia nguruwe kama mnyama mchafu na asiyefaa kuwa karibu naye na hata kwa matumizi kama lishe. Zaidi, nyama yake inapendwa na haina madhara kwa afya na inapendekezwa kuliwa zaidi kuliko nyama nyekundu. Unaweza kuanzisha mradi wa nguruwe kwa gharama ndogo lakini baada ya kipindi cha miezi tisa tu ukaanza kujipatia kipato kutokana na ufugaji huo. Ufugaji Nguruwe hawa itaji mtaji mkubwa sana ili kuwafuga,hata wakulima wadogo wanaweza kumudu kufuga nguruwe kwa kua huitaji mtaji mkubwa sana ili kuwa fuga na pia huleta faida kubwa pale wanapo fiki hatua ya kuya wakubwa BANDA Nguruwe wanahitaji kuwa na banda lililojengwa kwa sakafu ya zege au ukachanganya mchanga na siment unaweza chagua kulingana na uwezo wako . Ukubwa wa banda unategemeana na idadi ya nguruwe unaotaka kufuga. Mita 3 kwa mita 2.5 zitawaweka nguruwe 8-10 wanaonenepeshwa kwa soko au nguruwe jike mmoja na nguruwe ndume mmoja.

CHAKULA Uzuri wa nguruwe hua hawana gharama kubwa sana katika kuwalisha. Unaweza kuwalisha kwa kutumia majani laini ya aina mbalimbali,pumba.napia unaweza kuwalisha na mashudu aina ya Wheat Poland,au mabaki ya chakula chabinadamu.japo kua kunakua na aina maalum kwa ajili ya chakula kwa ajili ambacho unaweza kuwalisha kilo 1-2 kwa siku

KUPANDISWA

76

Nguruwe wakike yan sow ka lugha ya kitaalam anapandishwa pale anapo ingi kwenye joto kama mnyama yoyote yule na unaweza kujua kama ameingia kwenye joto pale anapokua msumbufu/lestless, anakua anawapanda wenzae,uteute mweupe unatoka kwenye uke wake,na pia vulva inabadilika nakua nyekundu. KUZAA Nguruwe hubeba mimba kwa kipindi cha siku 114 yan miez mitatu na na siku kadhaa. Nguruwe mmoja ana uwezo wa kuzaa watoto 6 hadi 14 kwa mara moja. Watoto wa nguruwe (piglets) huanza kula chakula cha kawaida wanapofika umri wa mwezi mmoja na nusu mpaka miezi miwili. Endapo nguruwe watapata matunzo mazuri, baada ya miezi 6 wanakuwa na uzito kati ya kilo 50-70 na wanaweza kuuzwa. JINSI YA KUWATUNZA Baada ya nguruwe kuzaa anatakiwa kupatiwa chakula na maji ya kutosha cha kutosha na ili kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto wake. Watoto wa nguruwe wachomwe sindano ya madini ya chuma (Iron injection) baada ya siku2 au3 toka kuzaliwa. Hii ni muhimu sana vinginevyo wanaweza kufa wote. Kata meno (tooth clipping) baada ya miezi mitatu. Unaweza kuhasi madume (castration) baada ya miezi miwili. BAADHI YA MAGONJWA YA NGURUWE Kila siku magonjwa mengi kwa binadamu na wanyama yanatokea.lakinm kunamagonjwa ambayo kama mfugaji lazima uyajue kwakua ndio yanayo jitokeza. UGONJWA WA MIGUU NA MIDOMO Ugonjwa huu huathiri midomo na miguu ya nguruwe. Ni ugonjwa ambao hushambulia nguruwe mara kwa mara hasa wasipokuwa na matunzo mazuri. Ugonjwa wa miguu na midomo, hudhoofisha nguruwe kwa haraka sana, ikiwa ni pamoja na kupungua uzito. Chanjo: Chanjo yake huitwa FMD VACCINATION nautolewa kila baada ya mwaka mmoja Dalili,dalili zake miguu na midomo ya nguruwe inabadilika na pia nguruwe anadhoofika Tiba: Ugonjwa huu hauna tiba halisi. Inapotokea nguruwe wakawa wameshambuliwa kinachofanyika ni kutibu magonjwa nyemelezi kwa kutumia antibiotics. HOMA YA NGURUWE (SWINE FEVER)

77

Ugonjwa huu unasambaa kwa kasi kama mmoja akiambukizwa wengine pia wataambukizwa na kufa Dalili, nguruwe anakua na vidonda na vitu kama vibarango mwili mzima pia mdomo na masikio yanabadilika rangi nakua mekundu. Chanjo: Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba. Kinachofanyika mlipuko unapotokea ili kuwa salama ni kuwateketeza nguruwe wote walioathirika na kuanza upya. Unaweza kuteketeza kwa kuwachoma moto. Muhimu: Baada ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa aiana ya Acon au Ectomin, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja kabla ya kuweka nguruwe wengine kwa kua huu ni viral disease UGONJWA WA MAPAFU (PNEUMONIA) Ushambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe,Ugonjwa huu husababishwa na bacteria (Secondary bacterial), joto kupita kiasi, vumbi na gesi inayotokana na madawa makali. Dalili, nguruwe hukooa na kupumua kwa shida sana Tiba: Homa ya mapafu kwa nguruwe inatibika kwa kutumia antibiotics. Pamoja na kuwaweka wanyama sehemu safi, isiyo na baridi kali au joto la kupitiliza kiwango. KIMETA(ANTHRAX) Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis, wadudu hawa wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline. Muhimu:nguruwe alie kufa kwa kimeta usimshkew kabsa kwa sababu hata binadamu anaupata huu ugonjwa, chimba shimo mbali na watu mwagia mafuta ya taa ndani ya hilo shimo kisha fukia mzoga., dalili ya nguruwe alie kufa kwa kimeta damu hua aigandi na pia hata nzi hawasogei kwenye mzoga kwa hiyo kua makini.

78

AINA ZA NGURUWE Largewhite

SIFA ❖ ❖ ❖ ❖ ❖

Hii ndio aina kubwa kabsa kuliko aina zote tatu Anakua na mwili mweupe pote Masikio yake yamesimama wima Ni mama mzuri Anakua na mdomo mbinuko

landress

79

SIFA ❖ Anakua mweupe pia au anaweza kua na mabaka meusi ❖ Ni mkubwa kiasi ❖ Masikio yake yamelala Saddleback

80

SIFA ❖ ❖ ❖ ❖

Anakua mweusi ila anakua na mkanda mweupe shingoni Pia ni mpole Anamasikio ya kulala Anakua mkubwa kiasi”

MASWALI MUHIMU KWA MSOMAJI WA KITABU HIKI: 1. Soko lipo, wapi, wakati gani na kwa kiasi gani?

81

2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20.

Je unao mpango wa biashara yako (Business plan)? Je una bajeti ya mapato na matumizi kwenye biashara yako? Umefungua akaunt ya biashara au laa..? Huwa unalima kwanza ndio utafute soko, au unatafuta soko ujiridhishe ndipo uende kulima shambani (Market research)? Je, uliwahi kujifunza kwa wakulima na wajasiriamali walio fanikiwa? Nidhamu ya kazi huwa unaizingatia? Nikivipi unatumia mitandao ya kijamii kutangaza kazi zako? Muda wako unautumia vizuri? Je umeweka miundo mbinu ya umwagiliaji shambani mwako? Je, usimamizi wa biashara yako uko vizuri kiasi gani na unapata faida? Fursa za kilimo zipo nyingi sana, je umeweza kuona fursa na kuzifanyia kazi? Ni sababu gani zinakufanya usilime na au kufuga kwa tija na faida zaidi? Ni hazina gani ungependa umrithishe mtoto wako? Je ardhi yako inakupa faida gani na unaitumiaje (Ardhi ni hazina)? Ni mambo gani yanakuletea hasara kwenye biashara yako ya kilimo? Nidhamu ya fedha inasemekana ni elimu ya muhimu sana ya kumfanya mtu afanikiwe ki-biashara akiitumia vizuri. Hivi ni kweli? Una mikondo mingapi ya kipato? Si inawezekana kuwekeza? Je unawafurahisha wateja wako? Je unaongeza thamani kwenye bidhaa au huduma yako?

82

MAREJEO/Reference Hotuba ya waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika (2008), 1–67.

Kamoyani, P. B., Huduma, K. W. a, & Kilimo, Z. a. (2004). Kilimo cha mseto katika nchi za hari, (October).

Kutoka Shamba Hadi Sokoni. (n.d.)

Mbunifu, M. (2015). Epuka kuchunga mifugo kwenye maeneo hatarishi.

Ongeza mavuno ya Alizeti kwa kupanda mimea mseto. (2008), 25.

83

Get in touch

Social

© Copyright 2013 - 2024 MYDOKUMENT.COM - All rights reserved.