MUDU SARUFI 5, 6 & 7 Flipbook PDF

MUDU SARUFI 5, 6 & 7

16 downloads 104 Views 479KB Size

Recommend Stories


& 0! 2! 5& 6! 9 % :7 75& %" :7 "% :7& # : ; #"
! " # $ %# & $ '( & ) # *+ ,. / & . ! 0 , *, & ) ! # 1 " #" " 2 23& 4 2 &! & 3 2 ! 5& 2 7 2 &! 6 ! , 2 ! 81 & % 9 7 5

"#.,%%"+5 52"#4&*" 6-7$%&(8$"
!"#$%"&'#()*++,(-$.&/*%0,/$),"&1 %"&+(/'"23"&)$&4%"-+"&/"#.,%%"+5 !"#$#%&'%( Pepita Grilla !"#$%&'()%)*+,%-. )*%+,*-*./'$'0*.#%.,'.*/"'. ..........

0. $!2+, 3!! "# 43 $ % & 5 6 ( 7 6 ( : 9-6 ( 6;. & 9 < -9
! ) * + ' , $! 2 , "- . ) * /0 + 3 ! ! ) * ' , $! 2 ) * . 1, ' , $! 2 " , "- . ) * /0 + . 1, + # + $ ) * . 1, % + , "- . ) * ' , $

6 5
DECRETO 6964/65 La Plata, 24 de agosto de 1965 VISTO el expediente Nº 2412-124 de 1963, por el que el Ministerio de Obras Públicas eleva el proyecto

Story Transcript

Mudu Sarufi ya KISWAHILI 5, 6 & 7

ZENGO BUSALAMA (+255 787 745 222)

1

YALIYOMO 1. KAULI ZA VITENZI NA HALI ZAKE …………………………………………………………… 4 • Kauli kumi za vitenzi • Hali kumi za vitenzi 2. VIAMBISHI …………………………………………………………………………………………….…9 • Dhana ya viambishi • Kategoria za viambishi na dhima zake • Mzizi wa neno 3. VINYUME, UYAKINISHI NA UKANUSHI ……………………………………………………...13 • Aina za vinyume • Aina za ukanushi na ada zake 4. NGELI ZA NOMINO NA UPATANISHO WA KISARUFI ………………………….……….19 • Kategoria za ngeli za nomino • Upatanisho wa kisarufi 5. UHUSIANO WA WATU NA KAZI ZAO…………..………………………………………………24 • Uhusiano wa watu kifamilia • Watu na kazi/tabia zao 6. WANYAMA NA VIKEMBE VYAO …………………………………………………………………29 • Hali za wanyama • Vikembe vya wanyama na baadhi ya wadudu 7. VIPINDI VYA NYAKATI ……………………………………………………………………………..32 • Tofauti ya kipindi na wakati • Nyakati nane na vipindi vyake 8. AINA SABA ZA MANENO …………………………………………………………………………..35 • Nomino (N) • Viwakilishi (W) • Vivumishi (V) • Vitenzi (T, Ts, t) • Vielezi (E) • Viunganishi (U) • Vihisishi (H) 9. AINA NNE ZA SENTENSI (CASH) ……………………………………………………………53 • Changamano • Ambatano • Shurutia

2



Huru

10. KAULI HALISI NA KAULI TAARIFA …………………………………………………………….57 • Kauli halisi • Kauli taarifa 11. UANDISHI WA BARUA ………………………………………………………………………..…..60 • Barua ya kirafiki • Barua ya kiofisi 12. SAUTI ZA LUGHA YA KISWAHILI ……………………………………………………………..67 • Dhana ya Sauti za lugha • Kategoria za abjadi za Kiswahili • Silabi za kiswahili na miundo yake 13. ULEMAVU WA BINADAMU …………………………………………………………….………..71 • Jedwali na ulema na fasili zake 14. AKISAMI, MAJIRA YA MWAKA NA MISAMIATI YA MALIPO …………………………73 • Akisami • Majira manne ya mwaka • Misamiati wa malipo 15. NYONGEZA I. USHAIRI …………………………………………………………………………………….76 II.

VYAKULA ANUWAI ………………………………………………………………….…. 87

III.

ETIMOLOJIA YA BAADHI YA MANENO YA KISWAHILI …………………...87

IV.

VISAWE VYA BAADHI YA VIUNGO VYA MWILI …………………………….… 88

3

1 KAULI ZA VITENZI NA HALI ZAKE 1.1. Kauli za Vitenzi Dhana ya Kauli za vitenzi Kauli za vitenzi ni mnyumbuliko wa vitenzi kulingana na utendaji wake. Mnyumbuliko ni uundaji wa neno jipya kwa kuongeza viambishi baada ya mzizi wa kitenzi. Mfano; Ukinyumbulisha neno soma unaweza kupata maneno kama vile somwa, somewa, n.k Kauli kumi (10) za vitenzi Na Kauli Maelezo

Kiishio

Mfano

1

-a/ø

Soma, piga

-ea/ia

Somea, pigia

-ana

Somana, pigana

-eana/iana

Someana, pigiana

-wa

Somwa, pigwa

-ewa/iwa

Somewa, pigiwa

-eka/ika

Someka, pigika

-esha/isha

Somesha, pigisha

-eshana/ishana

Someshana, pigishana

2 3 4

5 6

7 8

9

10

Kutenda

Kitendo katika hali yake ya kawaida pasi na kunyambuliwa Kutendea Kufanya kitendo kwa niaba au kwa ajili ya mtu mwingine Kutendana Unamfanya mtu kitendo nay eye anakufanya vivyo hivyo Kutendeana Unafanya kitendo kwa niaba ya mtu nay eye anafanya kitendo hicho hicho kwa niaba yako Kutendwa Kuathirika moja kwa moja na kitendo Kutendewa Kitendo kufanywa na mtu mwingine kwa niaba au kwa ajili yako Kutendeka Kitendo kufanyika na kukamilika barabara Kutendesha Kumfanya mtu atende jambo fulani kwa niaba au kwa ajili yako Kutendeshana Mtu anakufanya utende jambo fulani na wewe unamfanya unamfanya atende jambo hilohilo Kutendesheana Kumfanya mtu atende jambo Fulani kwa ajili au kwa niaba ya mtu mwingine na yeye pia amfanye mtu mwingine atende jambo hilo hilo kwa ajili au kwa niaba yako

4

Somesheana, esheana/ishiana pigishiana

Kanuni inayotawala kauli za vitenzi:

Kauli = Mzizi + Kiishio

Chunguza jedwali hapa chini Na Kitenzi Kanuni 1 Pasha Pash+a 2 Sikia Siki+a 3 Tembea Tembe+a 4 Kimbia Kimbi+a 5 Andika Andik+a 6 Saili/jaribu Saili+ø/jarib+u 7 Elezea Elez+ea 8 Chekwa Chek+wa 9 Limwa Lim+wa 10 Lika L+ika

Kauli Kutenda Kutenda Kutenda Kutenda Kutenda Kutenda Kutendea Kutendwa Kutendwa Kutendeka

ZOEZI LA 1 A. Sentensi zifuatazo zipo katika kauli zipi za vitenzi? 1. Kamba yangu imeliwa na mchwa 2. Nyumba zile zilibomolewa na maafisa ardhi 3. Kingo za mto ule zilibomolewa vibaya 4. Mpunga uliliwa na ndege 5. Baba ameandika barua kwa mama 6. Mponeja alitupasha habari njema 7. Tunapaswa kusoma kwa bidii 8. Ukisikia jina lako nenda 9. Mimi ni fundi wa kuwamba ngoma 10. Watoto wote walimlilia yeye 11. Tulikula chakula chote 12. Tulichoshwa sana na safari ile 13. Walikanywa waache uzabizabina 14. Tuliwashauri wasipende vitu vya bure 15. Watoto walichokozana mpirani 16. Watumishi walicheleweshewa mishahara yao 17. Kahawa yote imetolewa shambani 18. Vifaranga wote walitotolewa siku hiyohiyo 19. Bibi alikuwa anakamia maziwa 20. Kikombe kile kilivunjika

5

B. Nyambulisha maneno yafuatayo katika kauli za vitenzi kwenye parandesi 1. Umiza (kutendeka) 2. Kemea (kutendwa) 3. Kurupushwa (kutenda) 4. Liwa (kutenda) 5. Lilia (kutendwa) 6. Zawadiwa (kutenda) 7. Chora (kutendeana) 8. Kulindwa (kutendana) C. Bainisha mtenda, mtendwa/kitendwa na mtendewa katika sentensi hizi 1. Zawadi alizawadiwa na Zawadi 2. Omari alipigiwa mpira na Oska 3. Kabaka alimwibia Kalunde simu yake 4. Ukuta ulibomolewa na Imran 5. Walimpiga sana kwa mijeledi 6. Tulimpandia mahindi yake yote 7. Mpira ule uligonga mwamba nusura goli liingie 8. Wote waliadhibiwa isipokuwa Tino 9. Mdukuzi kadukua taarifa zao 10. Walimbwende wote walitunzwa D. Elezea fasili nne za kila sentensi uliyopewa hapo chini 1. Mwajuma alipigiwa simu na mumewe 2. Hashimu alimpigia mpira dada yake E. Maneno yafuatayo yapo kwenye kauli gani? (1) Bomolewa (2) Liwa (3) Liliwa (4) Haribiwa (5) Ibiwa (6) Sikia (7) Umia (8) Sairi (9) Telekeza (10) Pewa

6

1.2. Hali za Vitenzi - Hali ya kitenzi ni namna au jinsi tendo linavyokuwa kulingana na muktadha au wakati. Yaani, tendo linaweza kuwa katika hali ya uyakinishi, hali ya ukanushi, hali ya kuendelea, n.k.

Jedwali hapa chini linaonyesha hali kumi (10) za vitenzi Na 1

Hali ya kitenzi Isiyodhihirika

Viambishi a-ka-la-wa-ya

Dhima Kutoonyesha wakati wowote

2

Ukanushi

Si-, Ha- na Hu-

Si- kuonyesha nafsi ya Iumoja

3

Kuendelea

-na-

4 5

Timilifu Mazoea/Desturi

-me-hu-

6

Masharti/Uwezekano

-ki-, -nge-, ngeli-, -ngali-

7

Iliyopita timilifu

-li- …. –me- …

8

Iliyopita inayoendelea

-li- ….. –na- …

9

Ijayo timilifu

-ta- .. –me- …

10

Ijayo inayoendelea

-ta- … -na- …

7

Mfano Ahukumiwa, kahukumiwa, Lahukumiwa, Wahukumiwa, Yahukumiwa Sitaki

Ha- kuonyesha nafsi ya Iwingi, II-wingi, III-umoja na wingi

Hatutaki, hamtaki, hataki

Hu- kuonyesha nafsi ya IIumoja

Hutaki

Tendo linaendelea kufanyika Tendo limefanyika kitambo Tendo kufanyika mara kwa mara (kujirudiarudia) -ki- kuonyesha masharti au uwezekano wa tendo kufanyika

Ninataka Nimetaka Hutaka Akitaka

–nge-, -ngeli- na –ngalihutumika wakati uliopita

Angetaka

Kuonyesha tendo lililokuwa limekamilika muda uliopita Kuonyesha tendo lililokuwa linaendelea wakati uliopita Kuonyesha tendo litakalokuwa limekamilika wakati ujao Kuonyesha tendo litakalokuwa linaendelea wakati ujao

Alikuwa amelala Alikuwa anakula Atakuwa amelala Atakuwa anakula

ZOEZI LA 2 1. Yakinisha vitenzi vifuatavyo (i) Haongei (ii) Siwezi (iii) Hawakuja (iv)Sikulima (v) Hajaja (vi)Sijala (vii) Hawatakuwepo (viii) Tusingelikuja 2. Sentensi zifuatazo zipo katika hali gani? (i) Walikula na kunywa (ii) Ninaimba (iii) Amerudi kwao Kenya (iv)Tulikuwa tunaimba (v) Watakuwa wamelala (vi)Hapendi utani (vii) Walikotoka kuna mvua (viii) Ukitaka kuruka agana na nyonga (ix)Usipoziba ufa utajenga ukuta (x) Aghalabu hututembelea 3. Bainisha viambishi vya hali katika vitenzi vifuatavyo (i) Wangelikuja (ii) Tunakula (iii) Wamelima (iv)Sikumkuta (v) Hawapatani (vi)Huwanasihi (vii) Ukija 4. Taja dhima ya mofimu zifuatazo (i) –Ki(ii) –Na(iii) Hu(iv) -Me(v) Ha-

8

2 VIAMBISHI 2.1. Dhana ya Viambishi - Kiambishi ni mofimu inayoambatanishwa aidha kabla au baada ya mzizi wa neno ili kuunda neno jipya linalohusiana na neno la msingi - Kuna aina kuu mbili (2) za viambishi, ambavyo ni viambishi awali na viambishi tamati Mofimu ni nini? Mofimu ni kipashio kidogo kabisa cha kimofolojia chenye maana kisarufi ambacho hakiwezi kugawika tena. Dhima kuu ya mofimu ni kuundia neno jipya Kuna aina kuu tatu (3) za mofimu, ambazo ni:-

(i) Mofimu huru Hii ni mofimu inayojisimamia na kujitegemea kimaana. Kimsingi ni neno huru. Mfano; ng’ombe, sahani, rangi, muwa, nk

(ii)

Mofimu funge

Hii ni mofimu isiyo na uwezo wa kujitegemea kimaana. Mofimu hii ikikaa pekee yake hukosa maana kileksika. Mfano wa mofimu funge ni –a katika neno chapa, -i katika neno safiri, a- katika neno analima, nk

(iii)

Mofimu kapa (ø)

Hii ni mofimu isiyowakilishwa na chochote. Aghalabu hutumika katika wingi wa maneno yenye silabi tatu yanayoanza na sauti u katika umoja.

Chunguza maneno haya Na 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10

Umoja (u+mzizi) U+nywele =unywele U+fito =ufito U+funguo =ufunguo U+kuta =ukuta U+lindi =ulindi U+lingo =ulingo U+kuti =ukuti U+kufi =ukufi U+kosi =ukosi U+kozi =ukozi

Wingi (ø+mzizi) Ø+Nywele =nywele Ø+Fito =fito Ø+Funguo =funguo Ø+Kuta =kuta Ø+Lindi =lindi Ø+Lingo =lingo Ø+Kuti =kuti Ø+Kufi =kufi Ø+Kosi =kosi Ø+Kozi =kozi

9

2.2. Kategoria za viambishi na Dhima zake 2.2.1. Kategoria za viambishi Viambishi vimegawanywa katika kategoria kuu mbili:(i) Viambishi awali Hivi ni viambishi ambavyo hupachikwa kabla ya mzizi wa neno. Vipo vya aina saba • Viambishi awali vya ngeli (pa-m-tu-ni-ku-wa-zi-a-u-li-ya-ki-i-vi) • Viambishi awali vya nafsi ya mtenda (nitu-um-awa) • Viambishi awali vya nafsi ya mtendwa au mtendewa (ni-ku-wa-m-tu) • Viambishi awali virejeshi vya ngeli (po-lo-ko-cho-ye-mo-o) • Viambishi awali vikanushi vya nafsi (sihahu) • Viambishi awali vya wakati na hali (njeo)-(nalitamehu) • Viambishi awali vikanushi vya wakati (kujai)

Viambishi tamati (viambishi kaditama) (ii) Hivi ni viambishi ambavyo huwekwa baada ya mzizi wa kitenzi ili kutuarifu kauli au mnyumbuliko wa kitenzi hicho. Mfano; -wa katika neno pigwa inaonyesha kauli ya kutendwa

Na 1

2

Dhima ya viambishi awali 2.2.2. Kiambishi Dhima Ngeli Kuonyesha umoja au wingi (pa-m-tu-ni-ku-wa-zi-a-uli-ya-ki-i-vi) Nafsi ya mtenda Kuonyesha mtenda wa tendo (nitu-um-awa)

3

Nafsi ya mtendewa/mtendwa (ni-ku-wa-m-tu-o-ye)

Kuonyesha nafsi ya mwathirika wa tendo. Aghalabu huwekwa nyuma ya mzizi wa neno

4

Virejeshi vya ngeli (po-lo-ko-cho-ye-mo-o) Vikanushi vya nafsi (sihahu)

Hurejelea ngeli ya mtendwa au mtendewa Kuonyesha hali ya ukanushi wa nafsi ya mtenda au mtendewa Si-nafsi ya I-umoja Ha-nafsi ya I-wingi, II-wingi na nafsi ya III-umoja na wingi

5

10

Mfano Ameapa (A-WA umoja) Kilipotea (KI-VI umoja Yalipotea (LI-YA wingi) Ninalima (mimi) Unalima (wewe) Analima (yeye) Tunalima (sisi) Mnalima (ninyi) Wanalima (wao) Zimekufikia (wewe) Ninawatuma (wao) Watanikoma (mimi) Nitamtuma (yeye) Watatutuma (sisi) Walipoenda Walikojificha Ninatak-sitaki Anataka-hataki Unataka-hutaki Wanataka-hawataki Tunataka-hatutaki

6

Njeo (wakati na hali) (na-li-ta-me-hu)

7

Vikanushi vya njeo (ku-ja-i)

Hu-nafsi ya II- umoja Kuonyesha lini kitendo chafanyika

Kukanusha kitenzi kulingana na wakati au hali

Mnataka-hamtaki Analima-sasa Alilima-jana Atalima-kesho Amelima-hivi punde Hulima-kila siku Alicheka-hakucheka Amecheka-hajacheka Nacheka-sicheki Hucheka-sicheki/hacheki

2.3. Mzizi wa neno - Mzizi ni mofimu ambayo si lazima iwe neno ambayo ndiyo kiini cha neno. AuMzizi ni sehemu ndogo ya neno ambayo haibadiliki ukiondoa viambishi vyote - Dhima kuu ya mzizi wa neno ni kuunda neno jipya kwa kuongeza au kupunguza viambishi awali au tamati Kuna aina kuu mbili za mizizi ya maneno

(i) Mzizi funge Mzizi wa aina hii huundwa na mofu moja. Mfano; -l- katika maneno kula, chakula, mlo au –f- katika maneno kifo, kufa, mfu, na –j- katika maneno ujio, njoo, uje, n.k

(ii) Mzizi huru -

Pia huitwa mzizi sahili. Mzizi wa aina hii huundwa na mofu zaidi ya moja. Mfano; -li- katika maneno kulia, lia, kilio; -lim- katika maneno lima, kulima, kilimo; -tembe- katika maneno matembezi, tembea, tembelewa; -kimbi- katika maneno kimbia, kimbiliwa, kimbilio, n.k

ZOEZI LA 3 1. Bainisha viambishi vya ngeli kisha taja dhima zake (i) Diengi amepata jiko (ii) Maputo yote yamepasuka (iii) Viti vyote vimekaliwa (iv) Pale ndipo palipobomoka (v) Mafya haya yamechakaa 2. Bainisha viambishi vya nafsi ya mtenda kisha andika dhima zake (i) Hatuwezi kutulia kabisa (ii) Unajiona sana siku hizi (iii) Mnacheka kwa sauti mno (iv)Tunasoma kwa bidii (v) Ananijua

11

3. Bainisha viambishi vya nafsi ya mtendwa/mtendewa (o-rejeshi) kisha andika dhima zake (i) Je, taarifa zilikufikia? (ii) Nitawatuma kesho (iii) Sikumkuta mtu yeyote pale (iv)Leo watanikoma (v) Walituombea sana 4. Bainisha viambishi vya wakati na hali kisha taja dhima zake (i) Baba analima Samata alicheza vizuri (ii) (iii) Zahera amelia sana leo (iv) Tino hucheza vizuri (v) Simfahamu mtu yeyote hapa 5. Andika dhima za viambishi vifuatavyo (i) –ku(ii) –ja(iii) –i (iv) –me(v) –na(vi) –li(vii) –ta(viii) Hu(ix) Si(x) Ha(xi) A(xii) -m(xiii) -wa(xiv) Ni(xv) –tu(xvi) U(xvii) –ki(xviii) Ya(xix) Ki(xx) Li

12

3 VINYUME, UYAKINISHI NA UKANUSHI 3.1. -

VINYUME Kinyume ni neno lenye maana inayopingana na neno lingine. Aghalabu huwa ni neno jipya lenye tahajia na maana tofauti na lile la awali

Aina za Vinyume vya maneno Kuna aina tano (5) za vinyume

(i) Vinyume vya nomino dhahania au hali Mfano: - Vita – amani - Furaha – huzuni - Nuru – giza - Mwanzo- mwisho - Shibe – njaa

(ii) Vinyume vya vivumishi vya sifa Mfano: - Tamu – chungu - Kubwa – ndogo - Nyeusi – nyeupe - Safi – chafu - Mbali – karibu

(iii) Vinyume vya jinsia Mfano: - Baba – mama - Mume – mke - Kaka – dada - Mvulana – msichana - Mjomba – shangazi - Babu – bibi

(iv)Vinyume vya uhusiano Mfano: - Mwalimu – mwanafunzi - Daktari – mgonjwa - Mzazi – mtoto - Kiongozi – mfuasi/maamuma - Mwanajeshi – raia

13

(v) Vinyume vya vitenzi halisi au kauli ya kutenda Mfano: - Furahi- chukia/huzunika - Sifu – kashifu - Nyanyapaa – stahi - Simama – keti/kaa - Lia – cheka - Nuna – tabasamu - Tatiza – tanzua - Tandika – tandua - Injika – ipua/epua - Ezeka – ezua - Fuma – fumua - Fumba- fumbua - Tega – tegua - Choma – chomoa - Kata – unga Orodha ya misamiati teule na vinyume vyake Ifuatayo ni baadhi ya misamiati teule na vinyume vyake ambayo kwa hakika utakutana nayo katika mitihani anuwai ikiwemo ya utamilifu na ule wa utimilifu 1. Adili –uovu 2. Adimu – tele 3. Aghalabu – nadra 4. Ahirisha – tekeleza 5. Awali – tamati 6. Kaditama – mwanzo 7. Asubuhi – jioni 8. Mchana – usiku 9. Barubaru – banati 10. Bin –binti 11. Bwerere – aghali 12. Cheka – lia 13. Nuna – tabasamu 14. Chelewa – wahi 15. Kawia – wahi 16. Dhaifu – imara 17. Duni – bora 18. Elea – zama 19. Ezeka – ezua 20. Fuma – fumua 21. Gwiji – goigoi 22. Halali- haramu 23. Hila – uungwana

14

24. Hiari – shuruti, lazima, amri 25. Injika – ipua, epua 26. Ipua – injika 27. Karaha – amani 28. Kwea – shuka, teremka 29. Lazimisha – bembeleza 30. Mjomba – shangazi 31. Mwalimu – mwanafunzi 32. Mzalendo – haini 33. Gharibu – mwenyeji 34. Mzee – kijana 35. Mzoefu – maamuma 36. Ana elima – mjinga 37. Nuna – tabasamu 38. Nuru – giza 39. Nyanyapaa –stahi, jail 40. Okota – dondosha 41. Tekenya – finya 42. Paa- tua, sakafu 43. Panda – shuka, teremka, vuna 44. Rambirambi – nderemo, vifijo, furaha 45. Sahibu – adui 46. Shaibu – ajuza 47. Shujaa- goigoi, mwoga 48. Shuruti – hiyari 49. Tabibu – mgonjwa 50. Tandika – tandua 51. Tawanya – kusanya 52. Tapanya – kusanya 53. Tele – adimu 54. Ughaibuni – nchi jirani 55. Zama- ibuka 56. Ziba – zibua 57. Sifu – kashifu 58. Tatiza – tatua 59. Muumini – kasisi, mchungaji, shehe 60. Mwerevu – mjinga

15

ZOEZI LA 4 Andika vinyume vya maneno yafuatayo 1. Tandika 2. Fuma 3. Ezeka 4. Zama 5. Tatiza 6. Tabasamu 7. Sifu 8. Kiongozi 9. Nyanyapaa 10. Gharibu 11. Shababi 12. Njaa 13. Msiba 14. Eupe 15. Bin 16. Mtoto 17. Maamuma 18. Injika 19. Amani 20. Lia

3.2. UYAKINISHI NA UKANUSHI Uyakinishi ni nini? - Uyakinishi ni hali ya neno kuwa katika hakika na kweli yake. - Kwa hiyo kuyakinisha ni kitendo cha kukubaliana na kauli. Mfano; sitaki-nataka, hakufika-alifika, hawajala- wamelala, n.k Ukanushi ni nini? - Ukanushi ni hali ya kukataa kauli. Kwa hiyo kukanusha ni kitendo cha kukataa au kukana kauli - Ukanushi hufanyika kwa kuongeza kiambishi kikanushi nyuma ya neno husika ili kutengeneza neno linalokataa au kukanusha dhana ya neno linalokanushwa ilhali mzizi wake unabakia kuwa uleule. Mfano; njoo-usije, waende-wasiende, mtasema-hamtasema, n.k

16

Nini tofauti ya kinyume na ukanushi? Na Kigezo Kinyume 1 Fasili Ni neno lenye maana kinzani na lile ulilopewa 2 Tahajia Tahajia yake ni tofauti kabisa na ya lile neno linalopingwa 3 Dhana Dhana inayowakilishwa huwa kinyume na ya neno linalopingwa 4 Mzizi Mzizi hubadilika kabisa 5 Mifano - Vita – amani - Binti – bin - Peleka – leta - Shaibu- ajuza - Shababi- msichana

Ukanushi Ni neno linalokanusha neno jingine Tahajia hubadilika kidogo tu kutokana na ongezezeko la silabi kanushi Dhana ya msingi huwa haibadiliki

Mzizi -

haubadiliki kabisa Vuta – usivute Nendeni – msiende Njoo- usije Yeye – siye Mimi- si mimi

Aina za Ukanushi Kuna aina kuu mbili (2) za ukanushi

(a)

Ukanushi wa nafsi

Ukanushi wa nafsi ni ukanushi wa viambishi vya nafsi ya mtenda au mtendewa. Ukanushi wa nafsi hutumia viambishi vikanushi si-ha-hu

Chunguza mifano hii: Na Umoja Ukanushi 1 Sitaki 2 Hutaki 3 Hataki

(b)

Uyakinishi Ninataka Unataka Anataka

Wingi Ukanushi Hatutaki Hamtaki Hawataki

Nafsi Uyakinishi Tunataka Mnataka Wanataka

I II III

Ukanushi wa njeo

Ukanushi wa njeo ni ukanushi wa viambishi vya wakati na hali. Ukanushi wa njeo hutumia viambishi vikanushi ku-ja-i

Chunguza mifano hii: Na Umoja Ukanushi 1 Sikuja 2 Hukuja 3 Hakuja 4 Siji 5 Hujaja 6 Halimi

Uyakinishi Nilikuja Ulikuja Alikuja Ninakuja Umekuja Unalima

Wingi Ukanushi Hatukuja Hamkuja Hawakuja Hatuji Hamjaja Hawalimi

17

Nafsi Uyakinishi Tulikuja Mlikuja Walikuja Tunakuja Mmekuja Wanalima

I II III I II III

Ada za ukanushi - Ada ni kanuni zinazotawala dhana fulani. - Hivyo, ukanushi pia hutawaliwa na ada zake kulingana na aina ya ukanushi

Ukanushi wa nafsi Nafsi I II III

Mimi Sisi Wewe Ninyi Yeye Wao

Kiambishi cha Nafsi nituumawa-

Kanuni ya ukanushi

Mfano

Si+mzizi+i Ha+tu+mzizi+i Hu+mzizi+i Ha+m+mzizi+i Ha+njeo+kitenzi Ha+wa+njeo+kitenzi

Ninataka – sitaki Tunataka – hatutaki Unataka – hutaki Mtasema –hamtasema Alifika –hakufika Walifika – hawakufika

Ukanushi wa njeo Wakati Uliopo

Kiambishi cha njeo Uyakinishi Ukanushi -na-i

Ujao Uliopita Uliopo-timilifu Desturi/Mazoea Usiodhihirika

-ta-li-me-hua- /wa-

-ta-ku-ja-i -i

Kanuni ya ukanushi Ha+mzizi+i (si+mzizi+i) Ha+ta+kitenzi Ha+kitenzi Ha+ja+kitenzi Ha +mzizi+i Anipenda Wanipenda

Mfano Analima-halimi Nalima-silimi Atakuja –hatakuja Alikuja-hakuja Amelima – hajalima Hulima –halimi Hanipendi Hawatupendi

ZOEZI LA 5 1. Yakinisha sentensi zifuatazo (i) Hakumpiga kofi wala teke (ii) Kizuri hakijiuzi (iii)Sikupi heshima yako mkuu (iv)Usipeleke (v)Usipokuja sijishughulishi ng’o 2. Kanusha sentensi zifuatazo (i) Mosi alimpigia simu Pili (ii)Nimekuelewa (iii) Watasafiri mtondogoo (iv)Bei ikishuka nitanunua (v) Zinafanana 3. Andika kinyume cha maneno haya (i) Kaa (ii) Injika (iii) Aibu (iv) Lima (v) Tandika 4. Eleza tofauti uliopo kati ya “ukanushi na kinyume” 5. Taja viambishi vya ukanushi wa:- (i) Nafsi (ii) Njeo

18

4 NGELI ZA NOMINO NA UPATANISHO WA KISARUFI 4.1. NGELI ZA NOMINO Ngeli za nomino ni kundi la nomino lenye sifa zinazofanana kisarufi Dhima za Ngeli za nomino (i) Hutusaidia kujua upatanisho wa kisarufi, hivyo kuongea lugha fasaha (ii) Hutusaidia kujua maumbo ya umoja na wingi (iii) Hutusaidia kufahamu uhusiano uliopo baina ya Kiswahili na lugha zingine Kategoria za Ngeli za Nomino Kuna kategoria kadhaa za ngeli za nomino kama zilivyoainishwa katika jedwali Na Ngeli Maelezo Mifano 1 A-WA Hurejelea nomino za watu, wanyama, Mbuzi-mbuzi wadudu, ndege na samaki Ng’ombe-ng’ombe Sato- sato Mchwa-mchwa Mtoto-mtoto 2 KI-VI Hurejela nomino zinazoanza na sauti /ki/ Cherehani-vyerehani au /ch/ katika umoja na /vi/ au /vy/ katika Chuma –vyuma wingi Kijiko-vijiko Kiti-viti Kikapu-vikapu 3 LI-YA Aghalabu hurejelea nomino zenye mianzo Jiko-meko/majiko ya sauti /ji/ au /j/ katika umoja na /ma/ au Jicho-macho /me/ Jino-meno Ua-maua Aidha ngeli hii husimamia nomino zenye Bati-mabati miundo anuwai lakini zile ambazo Figa –mafiga huchukua viambishi vya ngeli /li/ katika Jifya -mafya umoja na /ya/ katika wingi 4 U-I Aghalabu huwakilisha nomino zenye Mti-miti mianzo ya sauti /m/ katika umoja na /mi/ Mfupa-mifupa katika wingi Mtambo-mitambo Mfuko-mifuko, nk 5 U-ZI Hurejelea majina ambayo huanza kwa Ukuta-kuta, sauti /u/ katika umoja na huchukua Upepo-pepo kiambishi cha ngeli /zi/ katika wingi Ufukwe-fukwe Unywele-nywele Ukucha-kucha

19

6

I-ZI

Hurejelea majina ya vitu visivyobadilika katika umoja wala wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi /i/ katika umoja na /zi/ katika wingi

7

U-YA

8

Ø- YA

9

U- ø

10

PA-MU-KU (Hurejelea vielezi vya mahali, k.v shuleni,nk)

Aidha majina yenye mianzo ya sauti /ny/, /mb/ na /ng/ yapo katika ngeli hii Hurejelea nomino ambazo huchukua kiambishi awali /u/ katika umoja na /ma/ katika wingi Hurejelea nomino za wingi (vitu visivyohesabika). Mengi ya majina haya huanaza kwa sauti /m/ Hurejelea nomino za wingi ambazo huanza kwa sauti /u/ PA-Hurejelea mahali maalumu pa wazi MU-Hurejelea mahali fulani ndani KU-Hurejelea mahali fulani kwa ujumla

Ufunguo-funguo Ufa-nyufa Uma-nyuma Ungo-nyungo, n.k Sukari, chumvi,chai, mbegu, nguo, nyumba,nyama, nk

Unyoya-manyoya Ugonjwa-magonjwa Majaribu, majivuno, majazi, majisifu, maji, maziwa, n.k Ulafi, upendo, ulevi, usafi, n.k

4.2. UPATANISHO WA KISARUFI Upatanisho wa kisarufi ni nini? Upatanisho wa kisarufi ni kukubaliana kisarufi baina ya nomino, kivumishi na kitenzi katika sentensi. Aidha upatanisho wa kisarufi ni utaratibu wa kimuundo ambao nomino inawakilishwa na mofimu katika maumbo mengine yanayohusiana nayo katika sntensi. Chunguza majedwali yafuatayo hili Jedwali A: Uhusiano wa Nomino na Vivumishi na Vitenzi Na Ngeli Kivumishi Kivumishi kionyeshi kishirikishi Umoja Wingi Umoja Wingi 1 A-WA Huyu Hawa Wangu Wetu 2 3 4 5

KI-VI LI-YA U-I U-ZI

Hiki Hili Huu Huu

Hivi Haya Hii Hizi

Changu Langu Wangu Wangu

20

Vyetu Yetu Yetu Zetu

Kitenzi kishirikishi cha ndiUmoja Wingi Ndiye Ndio /ndiwo Ndicho Ndivyo Ndilo Ndiyo Ndio Ndiyo Ndio Ndizo

6 7 8 9 10

I-ZI U-YA YA U PA-MUKU

Hii Huu Haya Huu Hapa

Hizi Haya Haya Huu Hapa

Yangu Wangu Yangu Wangu Pangu

Zetu Yetu Yetu Wetu Petu

Ndiyo Ndio Ndiyo Ndiyo Ndipo

Ndizo Ndiyo Ndiyo Ndiyo Ndipo

Humu

Humu

Mwangu

Mwetu

Ndimo

Ndimo

Huku

Huku

Kwangu

Kwetu

Ndiko

Ndiko

Jedwali B: Sentensi zenye upatanisho sahihi wa kisarufi Na Umoja Wingi 1 Mbuzi huyu aliyeumia ndiye wangu Mbuzi hawa walioumia ndio wetu 2 Kiti hiki kilichopambwa ndicho chako Viti hivi vilivyopamba ndivyo vyenu 3 Bati hili lililochakaa ndilo lake Mabati haya yaliyochakaa ndiyo yao 4 Mfupa huu uliooza ndio wake Mifupa hii iliyooza ndiyo yao 5 Uzi ule uliokatika ndio wangu Nyuzi zile zilizokatika ndizo zetu 6 Chai ile iliyomwagika ndiyo yake Chai zile zilizomwagika ndizo zao 7 Ugonjwa huo uliomshika ndio wake Magonjwa hayo yaliyowashika ndiyo yao 8 Maziwa yale yaliyomwagika ndiyo yangu Maziwa yale yaliyomwagika ndiyo yetu 9 Uyoga huu ulioiva ndio wako Uyoga huu ulioiva ndio wenu 10 Pale ndipo penye agano lake Pale ndipo penye maagano yao 11 Humo ndimo mlimomwagwa uchafu Humo ndimo mlimomwagwa uchafu wenu wako 12 Huku ndiko kwangu Huku ndiko kwetu Dhima za vitenzi vishirikishi vya ndi- kingeli Kitenzi Maana Dhima Ndisi Ndiyo sisi au ni sisi Nafsi ya 1-wingi (A-WA) Ndimi Ndiyo mimi au ni mimi Nafsi ya 1-umoja (A-WA) Ndiwe Ndiyo wewe au ni wewe Nafsi ya 2-umoja (A-WA) Ndinyi Ndiyo nyinyi au ni nyinyi Nafsi ya 2-wingi (A-WA) Ndiye Ndiyo yeye au ni yeye Nafsi ya 3-umoja (A-WA) Ndio Ndiyo hao au ni hao Nafsi ya 3-wingi (A-WA). Pia ni kiwakilishi cha ngeli ya U-I umoja na U-ZI umoja Ndiyo Ndiyo hiyo au ni hiyo Kiwakilishi cha ngeli ya I-ZI umoja, LI-YA wingi, U-I wingi, U-YA wingi, ngeli ya YA na ngeli ya U Ndiko Ndiyo huko au ni huko Kiwakilishi cha ngeli ya PA-MU-KU kurejelea mahali fulani kwa ujumla Ndilo Ndiyo hilo au ni hilo Kiwakilishi cha ngeli ya LI-YA umoja Ndipo Ndiyo hapo au ni hapo Kiwakilishi cha ngeli ya PA-MU-KU kurejelea mahali maalumu pa wazi

21

Ndimo

Ndiyo humo au ni humo

Ndicho Ndivyo Ndizo

Ndiyo hicho au ni hicho Ndiyo hivyo au ni hivyo Ndiyo hizo au ni hizo

Kiwakilishi cha ngeli ya PA-MU-KU kurejelea mahali maalumu ndani Kiwakilishi cha ngeli ya KI-VI umoja Kiwakilishi cha ngeli ya KI-VI wingi Kiwakilishi cha ngeli U-ZI wingi na I-ZI wingi

Nafsi za vivumishi vya kumiliki kingeli (-ngu-tu, -ko-nu, -ke-o)

1 Nafsi 1 2 3

Umoja -angu (yangu, langu, n.k) -ko (yako, lako, n.k) -ke (yake, lake, n.k)

2

Wingi -tu (yetu, letu, n.k) -nu (yenu, lenu, n.k) -o (yao, lao, n.k)

ZOEZI LA 6 1. Andika ngeli za nomino zifuatazo: (i) Mchwa (ii) Mbuzi (iii) Kifaranga (iv) Kinda (v) Kibwagara (vi) Ua (vii) Paa (viii) Kifaru (ix) Ufa (x) Uma (xi) Mtoto (xii) Cherehani (xiii) Chai (xiv) Magonjwa (xv) Maradhi 2. Andika sentensi zifuatazo katiak wingi (i) Jiko langu ni zuri (ii) Uyoga huu umeoza (iii) Ua huu ni mchafu (iv)Ukuta huu umebomoka (v) Chai hii haina sukari (vi)Ufa huu ni lazima uzibwe (vii) Mtoto anayelima ni mjukuu wangu (viii) Kilichoibwa ni chake (ix)Jitu lililokuwa likinisumbua limeuawa (x) Aliyanywa vizuri tu

22

3

3. Andika ngeli mbili (2) kwa kila nomino (i) Koo (ii) Paa (iii) Kaa (iv) Mbuzi (v) Ua 4. Maneno yaliyokolezwa wimo yapo katika nafsi gani? (i) Watu wangu wa nguvu nawapenda sana Mle ndimo mlimokuwa mnaburudika (ii) (iii) Wao ndio mahasimu wetu wakubwa (iv) Peke yetu hatuwezi (v) Pao hapafai Wale siku hizi hawapikiki katika chungu kimoja (vi) (vii) Anacheza kikwao (viii) Mwalimu Malecha ni gwiji la Hisabati (ix) Mtoto wa Nuru amekuwa gofu la mtu (x) Aishi na aisha wameoana 5. Sentensi hizi zipo katika ngeli gani? (i) Kiti cha dhahabu hakikaliwi na mtu (ii) Ajenga ingawa hana mikono (iii) Kwetu kuzuri (iv) Dengue ni ugonjwa huu ni hatari (v) Yai hili ni viza (vi) Chai hii haina sukari ya kutosha (vii) Uji wa mtoto umemwagika (viii) Mbao zetu zimeoza (ix) Ukuta wa bibi umenakshiwa (x) Maziwa ya mtoto yamenywewa na paka

23

5 UHUSIANO WA WATU NA KAZI ZAO 5.1. Uhusiano wa Watu kifamilia Uhusiano ni namna watu wawili au zaidi wanavyounganishwa ama kwa kuzaliwa au kwa ndoa. (i) Uhusiano wa kuzaliwa huitwa unasaba au uhusianishi - Uhusianishi ni hali ya viumbe aghalabu wanyama na binadamu kuhusiana kijeni au kichembeuzi kwa sababu ya kuwa na mbari, ukoo, jadi, nasaba au uzao mmoja. - Kundi la watu wenye nasaba moja, familia, uzawa au ukoo huitwa ayali (ii) Uhusiano wa kuoana huitwa uhusiano wa ndoa. Uhusiano wa ndoa ni muunganiko wa familia mbili au au zaidi zenye nasaba tofauti kwa njia ya kuoana Yafuatayo ni majina anuwai ya kimahusiano katika familia 1. Mama au nina- mzazi wa kike 2. Baba – mzazi wa kiume 3. Kaka – ndugu wa kiume 4. Dada – ndugu wa kike 5. Bibi au nyanya- mama wa baba au mama 6. Babu – baba wa baba au mama 7. Mjukuu – mtoto wa mwana 8. Kitukuu – mwana wa mjukuu 9. Kilembwe – mwana wa kitukuu 10. Kilembwekeza au kining’ina – mwana wa kilembwe 11. Ami au amu – kaka wa baba awe mdogo au mkubwa 12. Shangazi – dada wa baba awe mdogo au mkubwa 13. Mjomba au hau – kaka wa mama awe mdogo au mkubwa 14. Halati au hale – dada wa mama awe mdogo au mkubwa 15. Mkazahau au mkazamjomba- mke wa mjomba 16. Mkazamwana – mke wa mwana au mke wa mtoto wako 17. Mavyaa – mzazi wa kike wa mume 18. Bavyaa – mzazi wa kiume wa mume 19. Mamamkwe – mzazi wa kike wa mume au mke wako, mamkwe 20. Babamkwe – mzazi wa kiume wa mume au mke wako, bamkwe 21. Mcheja – mzazi wa mke au mume (mkwe) 22. Kivyere – jina la wazazi wa mume na wazazi wa mke hutumia kuitana 23. Mkoi – mtoto wa shangazi, mjomba, halati

24

24. Binamu – mwana wa kiume wa ami au amu 25. Bintiamu – mwana wa kike wa amu 26. Shemeji – ndugu wa mke au wa mume 27. Mama wa kambo – mama asiyekuzaa lakini anakulea 28. Umbu – jina waitanalo kaka na dada ikiwa wamezaliwa na mzazi mmoja 29. Ndugu mlungizi au mnuna– ndugu anayekufuata kuzaliwa 30. Wifi – mke wa kaka au dada wa mume 31. Mwamu au mlamu – kaka wa mke au mume wa dada 32. Mwanyumba – mume mwenzako aliyeooa kutoka boma moja na wewe au mume wa dada wa mke wako 33. Mkemwenza au mitara – jina wanalotumia wanawake walioolewa na mwanamume mmoja 34. Mtoto wa kwanza kuzaliwa – kifungua mimba, kichinja mimba, mwanambee, chudere, chaudere 35. Mtoto wa mwisho kuzaliwa – kitinda mimba, kifunga mimba, mziwanda, mwanamjukuu 36. Nyanyamkuu- mama wa nyanya 37. Babamkuu- baba wa babu 38. Maharimu – mtu usiyeweza kumwoa au kuolewa naye kwa sababu ya uhusiano wa nasaba 39. Baba mkubwa – ndugu wa kiume mkubwa wa baba yako 40. Baba mdogo – ndugu wa kiume mdogo wa baba yako 41. Mamachanja – jina litumiwalo na mume kumwita mke wake 5.2. Watu na Kazi /Tabia zao Kazi ni shughuli halali anayofanya mtu kwa lengo la kujipatia kipato, pia huitwa wajibu, dhima au jukumu. Hata hivyo nimetaja baadhi ya kazi au tabia ambazo si halali kwa lengo la kujifunza 1. Abidi ni mtumwa wa kiume 2. Baharia ni mtu anayefanya kazi kwenye chombo cha majini; mwanapwa 3. Bawabu ni mtu anayelinda mlangoni; gadi , mlinzi 4. Boharia ni mtu anayetunza stoo, bohari au ghala 5. Boi ni mfanyakazi wa ndani wa kiume 6. Bucha ni mtu anayechinja wanyama; mchinjaji. 7. Chokora au chokra ni mtumishi wa kazi za nyumbani 8. Chura ni mtu anayezibua vyoo au anayefagia barabara; topasi 9. Dalali ni mtu anayeuza vitu kwa kunadi katika mnada; mnadi 10. Dereva ni mtu anayeendesha gari, treni, pikiki au baiskeli 11. Dobi ni mtu anayefua na kupasi nguo 12. Fanani ni mtu anayesimulia hadithi; msimulizi 13. Hakimu ni mtu anayeamua kesi baina ya mshitaki na mshitakiwa; kadhi, jaji 14. Haramia ni mwizi wa vyombo vya majini au baharini 15. Jangili ni mwindaji haramu, mkaa 16. Kachero ni mtu anayepeleleza na kuchunguza matukio, askari kanzu, mpelelezi

25

17. Kibaka ni mtu anayepora vitu vya watu; mporaji 18. Kijakazi ni mfanyakazi wa ndani wa kike; kisonoko, ama 19. Kiranja ni kiongozi wa wanafunzi 20. Kiroboto ni askari wa kukodiwa, wamluki 21. Kocha ni mtu anayefundisha michezo 22. Kondakta ni mtu anayekatisha tikiti za wasafiri au abiria 23. Korokoroni ni mlinzi wa gereza au ghala la jeshi 24. Kuli ni mtu anayepakia na kupakua mizigo au shehena melini 25. Kungwi ni mtu anayefunda mwari unyagoni; somo 26. Kuruta ni askari ambaye hajahitimu mafunzo 27. Kwezi ni mtua anayekwea na kuangua matunda kwenye mti 28. Lomba ni mpiga ngoma katika kikundi cha wanawake 29. Maamuma ni mfuasi wa dini 30. Machinga ni mtu anayeuza vitu kwa kutembeza 31. Makanika ni fundi wa kutengeneza magari mabovu 32. Malenga ni mtu anayetunga na kuandika mashairi 33. Manju ni stadi wa kutunga na kuimba nyimbo 34. Mchokozi ni mvuvi wa pweza 35. Mchuuzi ni mtu anayeuza bidhaa kwa rejareja 36. Mesenja ni mtu anayesambaza barua maofisini; katikiro, tarishi 37. Mfinyanzi ni mtu anayefinyanga vyungu 38. Mfuanazi ni mtu anayeondoa kumbi la nazi 39. Mgema ni mtu anayetengeneza pombe kutokana na miti au matunda 40. Mghani ni mtu nayeghani au imba mashairi 41. Mhadhiri ni mwalimu wa chuo kikuu 42. Mhagizi ni tabibu wa mifupa 43. Mhandisi ni mtu anayebuni na kusanifu miundombinu mbalimbali kama vile barabara, majengo, nk; injinia 44. Mhariri ni mtu nayesoma na kusahihisha maandishi; edita 45. Mhasibu ni mtu anayetunza kumbukumbu za fedha, mtunzafedha 46. Mhunzi ni mtu anayefua vyuma; msana 47. Mkaa ni mtu nayewinda wanyama; msasi, mwindaji au mrumba 48. Mkadamu ni msimamizi mkuu wa shamba 49. Mkalimani ni mtu anayetafsiri lugha, mtafsiri 50. Mkunga ni mtu anayezalisha wajawazito 51. Mkutubi ni mwangalizi na mtunzaji wa maktaba 52. Mlanguzi ni mtu anayenunua vitu kwa bei ya chini na kuviuza kwa bei ya juu. 53. Mlipi ni mtu anayelipa wafanyakazi fedha, mlipaji 54. Mnadhiri ni mtu aliyewka nadhiri 55. Mnajimu ni mtaalamu wa elimu ya nyota 56. Mndime ni kibarua anayelima shamba; mpande 57. Mnyapara ni kiongozi wa msafara wa miguu; mtu anayeangalia utekelezaji wa kazi bila ya yeye mwenyewe kushiriki; msimamizi 58. Mpagazi ni mtu anayebeba mizigo begani au rukwamani/mkokotenini; hamali

26

59. Mpishi ni mtu anayeandaa maakuli au chakula 60. Mrina ni mtu anayerina au kupakua asali; mpakua asali 61. Msanii ni mtu anayefanya kazi ya sanaa kama vile muziki, maigizo, kuchonga vinyago, nk 62. Mshenga ni mtu anayepeleka posa na mahari 63. Mshitiri ni mtu anayenunua bidhaa, mnunuzi 64. Msonzi ni mtu anayesuka nywele au mikeka; msusi 65. Mtambaji ni mtu anayetamba ngonjera au tenzi 66. Mtozi ni mwajiriwa mtaalamu na mbobezi wa jambo fulani 67. Mumiani ni mtu anayenyonya damu za watu na kuziuza 68. Mutribu ni msanii wa taarab 69. Muwani ni mtaalamu wa kupigana mieleka 70. Mvuvi ni mtu anayevua samaki 71. Mwalimu ni mtu anayefundisha darasani; mdarisi, ustaadhi 72. Mwanagenzi ni mtu anayejifunza stadi fulani chini ya mwalimu 73. Mwashi ni fundi ujenzi 74. Nahodha ni mtu anayeongoza meli, kiongozi wa timu ya soka; kapteni 75. Nesi ni mtu anayeangalia wagonjwa; muuguzi, mwalisaji 76. Ngariba ni mtaalamu wa kutahiri jandoni 77. Ngoi ni kiongozi wa nyimbo 78. Nokoa ni mlinzi na msimamizi msaidizi wa shamba 79. Nyakanga ni kungwi mkuu, mwalimu wa makungwi 80. Raisi ni kiongozi wa ngazi ya juu kabisa wa nchi iliyo jamhuri 81. Refa ni mtu anayechezesha mchezo; mwamuzi 82. Rubani ni mtu anayeongoza ndege; mwanahewa 83. Saisi ni mtu anayechunga punda au wanyama wengine na kuangalia waliopandwa na kuwatenga 84. Sekretari ni mtu anayetunza nyaraka ofisini, mhazili 85. Serehangi ni kiongozi wa wafanyakazi wa meli au ndege, naibu nahodha 86. Seremala ni mtu anayetengeneza samani; fundimbao 87. Shaha ni mwalimu wa malenga, malenga mkuu 88. Shehe ni mtu anayeswalisha msikitini 89. Sherasi ni kiongozi wa kikundi cha ngoma 90. Sinzia ni mwizi wa mifukoni 91. Sogora ni stadi wa kupiga ngoma 92. Sonara ni mtu anayetengeneza mapambo kama vile hereni, pete, bangili, nk 93. Spanaboi ni msaidizi wa makanika 94. Spika ni kiongozi wa vikao vya bunge; mutakalamu 95. Tabibu ni mtu anayetibu wagonjwa; daktari, mganga 96. Utingo ni msaidizi wa dereva; taniboi 97. Wakili ni mtu ambaye hutetea washitakiwa au washitaki mahakamani; mwanasheria 98. Yaya ni mlezi wa watoto

27

ZOEZI LA 7 1. Andika majina ya watu hawa kutokana na kazi zao (i) Mvulana aliyeajiliwa kufanya kazi za ndani …………………….. (ii) Msichana aliyeajiliwa kufanya kazi za ndani …………………….. (iii) Msichana aliyeajiliwa maalumu kwa kazi ya kulea watoto …………………….. (iv) Mtu anayesoma aghalabu muswada na kusahihisha, kupanga hoja na matumizi ya alama za uakifishaji ……………………………. (v) Mtu anayetengeneza vifaa vya chuma kama vile mapanga, mashoka na mundu ……. 2. Andika kazi za watu hawa (i) Seremala (ii) Mwashi (iii) Mnajimu (iv) Nokoa (v) Bawabu (vi) Kinyozi 3. Jaza nafasi zilizowazi kwa kutumia maneno uliyopewa kwenye kisanduku hapo chini …………………………. aliwafulia maharusi pete za dhahabu (i) (ii) Mzee Maneno ni fundi wa kutengeneza vitanda vya chuma na samani mbalimbal za nyumbani, hivyo huitwa …………………………… Dada Asha anafanya kazi ya kutunza na kuazimisha vitabu maktaba kwani (iii) yeye ni ……………………………….. (iv) Tulitia nanga salama kwani ……………………… wetu alikuwa mzoefu (v) Baba yangu anafundisha chuo cha ualimu, hivyo baba yangu ni ……… Sonara, mkufunzi, mhadhiri, utingo, nahodha, mkutubi, mhazili, seremala, mhunzi, 4. Jaza nafasi zilizo wazi (i) Kisawe cha kilembwekeza ni ………………………… (ii) Amina ni mtoto wa mjukuu wangu, hivyo amina ni nani kwangu? ……… (iii) Andrea na Anna ni watoto wa mama mmoja. Andrea ataamwita nani mme wa Anna? Mtoto wa kaka yako ikiwa wewe ni msichana atakuitaje? …………… (iv) (v) Masanja na Masunga ni marafiki. Je, mke wa Masanja atamuita nani Masunga? … 5. Taja majina ya watu wanaofanya kazi zifuatazo (i)Kutunga mashairi (ii) kutafsiri lugha moja hadi nyingine (iii) kutahiri (iv) kurekebisha mashine na mitambo (v) kutengeneza vyombo vya udongo (vi) kufundisha dini ya kiislamu (vii) kuamua kesi kortini (viii)kutengeneza vitu vya chuma (ix) kujenga nyumba kwa mawe (x) kufunda wari

28

6 WANYAMA NA VIKEMBE VYAO 6.1. Hali za wanyama Hali ya mnyama kuwa wa kike au kiume huitwa jinsi. Kwa kawaida kuna aina mbili za wanyama kulingana na hali au jinsi zao • Wanyama madume na • Wanyama majike. Kwa asili, wanyama madume wana jukumu la kupanda majike ili majike wabebe mimba na kuzaa ili kuendeleza kizazi. Wafuatao ni baadhi ya wanyama na hali zao Na Jina Hali /Dhima Kisawe 1 Ayala Mnyama pori dume wa jamii ya mbawala, swala, Ayale paa au pongo 2 Barare Dume la panzi lililokomaa 3

Denge

Dume la mbuzi lililokomaa

Beberu

4

Dorome

Dume la kondoo lililokomaa

Ng’ondi, vulata

5

Fahali

Dume la ng’ombe lililokomaa

Nzao

6 7 8 9 10

Galimu Gegedu Jogoo Koo Kuchi

11

Maksai

12 13

Mbuguma Mtamba

Dume la ngamia Dume la bata Dume la kuku lililokomaa Kuku jike anayetaga Jogoo mkubwa mwekundu ambaye ni hodari wa kupigana Ng’ombe dume aliyehasiwa ambaye hutumika kwa kazi mbalimbali Mnyama jike ambaye amezaa na anaendelea kuzaa Mnyama jike ambaye bado hajaanza kuzaa

14 15

Mtetea Njeku

16 17 18 19 20

Ndenge Pora Gendaeka Kishingo Zebu

21

Korwa

Kuku anayekaribia kutaga kwa mara ya kwanza Ng’ombe dume ambaye bado hajafikia umri wa fahali Mbuzi dume ambaye bado hajafikia umri wa beberu Kuku dume ambaye bado hajafikia umri wa jogoo Dume la nyani Kanga, bata au kuku asiye na manyoya shingoni Ng’ombe mwenye umbile kubwa pembe ndefu na nundu kubwa Kima dume

29

Jimbi, kikwara

Mbugome Mfarika, mbarika, mori, dachia Tembe

Koyogwe

6.2. Vikembe vya Wanyama na Wadudu Kikembe ni kizalia cha mtu, mdudu au mnyama. wanyama na wadudu Na Mnyama/ Kisawe mdudu 1 Bata 2 Binadamu Mja/mtu/mahuluku/insane /mlimwengu/insi 3 Chui 4 Chura 5 Farasi 6 Fisi Shumndwa/shundwa/baka ya/kingugwa 7 Kima Mbega/tumbili/ngedere 8 Kondoo Ng’onzi 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35

Kuku Mamba Mbu Mbuzi Mbwa Mbweha Ndege Njiwa/Hua Nyoka Ndovu Ng’ombe Nyati Ngamia Nguruwe Nyangumi Nyani Nyuki Nzi Nzige Paka Samaki Simba Sungura Punda Papa Kwanga Kima

Ngwena

Kelbu, kilabu

Tembo Bakari/bakara Mbogo/ng’ombe pori Bairi/jamali Hinziri/mbago/ngiri/gwase

Nyau Nsi/nswi/somba Asadi Kitungule Ndogwe Wibari Tumbili/ngedere

30

Vifuatavyo ni vikembe vya baadhi ya Kikembe

Kisawe

Kiyoyo Mtoto

Mwana/nyandu

Kisui Kiluwilulwi Mwanafarasi Bakaya Kichachuli Katama Kifaranga Kigwena Kiluwiliwi Mwanambuzi Kilebu Nyamawa Kinda Kipura Kinyemere Kidanga Ndama Ndama Nirihi Kibwagara Kinyangunya Kigunge Jana Buu Kimatu Kipusi Kichengo Shibili /shibli Kitungule Kihongwe Kinengwe Kitungule Kichachuli

Chongole Kitekli

Mwanakondoo/ngwisha/ kimeme

Kibui/kibuli Kibwa/kidue/papi

Nirigi Kidisi/kivinimbi

Funza Maige, tunutu, matumatu Kinyaunyau Chengo Kibwayi Kituju Kiongwe/mwanapunda

ZOEZI LA 8 1. Andika majina ya madume ya wanyama wafuatao (i)Ng’ombe (ii) Kondoo (iii) Mbuzi (iv) Bata (v) Kuku (vi) Swala (vii) Panzi (viii) Paa (ix) Ngamia (x) Nyani 2. Elezea wanyama wafuatao (i)Mtamba (ii) Koo (iii) Mbuguma (iv) Njeku (v) Pora (vi) Ndenge (vii) Mtetea (viii) Maksai (ix) Ayala (x) Barare (xi) Denge (xii) Fahali 3. Andika visawe vya viumbe hawa (i)ng’ombe (ii) simba (iii) beberu (iv) fahali (v) kondoo (vi)mtamba (vii)mbwa (vii) tembo (viii) nyumbu (ix)ngamia (x) kima (xi) mamba (xii)nyati 4. Andika maana mbili kwa kila neno hapo chini (i)tembe (ii) mbarika (iii) koo (iv)kima (v) mtetea 5. Andika majina ya vizalia viumbe wafuatao (i)Kuku (ii) Nzi (iii) Nguruwe (iv) Sungura (v) Simba (vi) Chui (vii) Nyuki (viii) Mbwa (ix) Ndege (x)Chura (xi) bata (xii) fisi (xiii) ng’ombe (xiv)mbu (xv) kondoo

31

7 VIPINDI VYA NYAKATI 7.1. Tofauti ya kipindi na wakati (i) Kipindi ni muda maalumu wa kukamilika wakati, pia huitwa mwia. (ii) Wakati ni msimu unaojumuisha vipindi kadhaa kukamilika. Pia huitwa majira, wakaa, muhula au awamu 7.2. Nyakati nane na vipindi vyake N Wakati Maelezo a 1 Saa Ni muda wa dakika 60 au sekunde 3600 2 Siku Ni muda wa saa 24 kuanzia asubuhi hadi asubuhi nyingine

3

Juma au wiki

Ni muda wa siku 7

4 5

Mwezi Mwaka

Ni muda wa majuma manne Ni muda wa miezi 12 au majuma 52

32

Vipindi • Sekunde 3600 • Dakika 60 • Asubuhi • Mchana • Adhuhuri • Alasiri • Jioni • Isha • Usiku • Usiku wa manane • Majogoo • Alfajiri • Mafungianyama • Mafunguliang’ombe • Jumatatu • Jumanne • Jumatano • Alhamisi • Ijumaa • Jumamosi • Jumapili Siku 28, 29, 30 au 31 • Januari (siku 31) • Februari (siku 28/29) • Machi (31) • Aprili (30) • Mei (31) • Juni (30) • Julai (31) • Agosti (31) • Septemba (30)

• • • 6 7 8

Muongo au mwongo Karne Milenia

Oktoba (31) Novemba (30) Desemba (31)

Ni muda wa miaka 10 Ni muda wa miaka 100 Ni muda wa miaka 1,000

TANBIHI: 1. Asubuhi ni mwanzo wa siku jua linapochomoza, bukrata 2. Mchana ni kipindi cha siku kati ya adhuhuri na alasiri. Au ni kipindi chote cha siku kati ya mawio na machweo. Pia huitwa kutwa 3. Adhuhuri ni kipindi cha siku kuanzia saa sita na nusu mchana hadi saa tisa mchana. Ni muda wa siku kati ya asubuhi na alasiri 4. Alasiri ni kipindi cha siku kati ya saa tisa mchana hadi saa kumi na moja na nusu jioni. Pia huitwa laasiri 5. Jioni ni kipindi kutoka alasiri hadi machweo, ni mwisho wa siku jua linapozama 6. Usiku ni kipindi cha siku baada ya kutua jua hadi alfajiri. Pia huitwa kucha 7. Isha ni kipindi kati ya saa mbili usiku na usiku wa manane 8. Usiku wa manane ni kipindi kati ya saa sita usiku hadi saa tisa 9. Majogoo ni kipindi kati ya saa 8 usiku hadi saa 11 alfajili 10. Alfajiri ni kipindi cha kati ya saa kumi na saa kumi na moja asubuhi. Pia huitwa liamba, mapambazuko, au asubuhi na mapema 11. Mafungianyama ni wakati wa jioni mifugo inaporejeshwa zizini baada ya kuwa malishoni mchana kutwa 12. Mafunguliang’ombe ni muda wa asubuhi mifugo inapofunguliwa kwenda kwenye malisho 13. Juzi ni siku ya pili kabla ya leo, siku moja kabla ya jana 14. Jana ni siku ya kwanza kabla ya leo 15. Leo ni siku iliyopo sasa, siku baada ya jana na kabla ya kesho 16. Kesho ni siku ya kwanza baada ya leo 17. Keshokutwa ya pili baada ya leo 18. Mtondo ni siku ya tatu baada ya leo 19. Mtondogoo ni siku ya nne baada ya leo 20. Jubilii ni sherehe maalumu za kuadhimisha tukio muhimu katika maisha ya mtu, asasi, shirika, nk, ambayo hufanywa kila baada ya kipindi fulani, mfano: Miaka 25 -ya fedha, 30-ya chaza, 50-ya dhahabu, 60-ya almasi, nk

33

ZOEZI LA 9 1. Siku ya nne baada ya leo huitwaje? 2. Kipindi cha kuanzia saa sita mchana hadi saa tisa mchana huitwaje? 3. Kipindi cha kuanzia saa tisa hadi saa kumi na moja huitwaje? 4. Siku ya tatu baada ya juzi huitwaje? 5. Kisawe cha neno juma ni kipi? 6. Wiki moja ina siku ngapi? 7. Mwezi mmoja una wiki majuma mangapi? 8. Mwaka mmoja una majuma mangapi? 9. Siku ya tatu baada ya Jumanne huitwaje? 10. Mwezi wa nne baada ya Julai huitwaje? 11. Kipindi cha miaka kumi huitwaje? 12. Kipindi cha miongo kumi huitwaje? 13. Kipindi cha miongo mia moja huitwaje? 14. Kisawe cha milenia ni nini? 15. Kipindi cha miezi mia moja na ishirini ni sawa na miongo mingapi? 16. Sherehe maalumu za kuadhimisha tukio muhimu katika maisha ya mtu, asasi, shirika, nk, ambayo hufanywa kila baada ya kipindi fulani, kv. miaka 25 au 50 huitwa je? 17. Jubilii ya dhahabu ni maadhimisho ya miaka ………………………. ya tukio 18. Jubili ya fedha ni maadhimisho ya miaka …………………….. ya tukio 19. Jubilii ya almasi ni maadhimisho ya miaka ……………………. ya tukio 20. Mntondogoo ni siku gani?

34

8 -

AINA SABA ZA MANENO Uainishaji wa maneno ni utaratibu wa kuyagawa maneno katika kategoria mbalimbali kulingana na kazi na sifa zake katika lugha. Katika lugha ya Kiswahili kuna kategoria au aina kuu saba (7) za maneno:(i) Nomino au majina (N) (ii) Viwakilishi (W) (iii) Vivumishi (V) (iv) Vitenzi (T, Ts, t) (v) Vielezi (E) (vi) Viunganishi (U) (vii) Vihisishi (H)

8.1. Nomino (N) - Nomino ni neno linalotaja jina la kitu, mtu, mahali, hali, mnyama, mdudu, samaki, ndege, siku, mwezi, namba, mwaka, nk. - Alama inayowakilisha nomino ni (N), na kisawe cha nomino ni Jina Aina za Nomino Kuna aina kuu tano (5) za Nomino, kwa kifupi tunaita PE-KA-JA-WI-DHA

PE=pekee KA=kawaida JA=jamii WI=wingi DHA-dhahania (i) Nomino za pekee - Haya ni majina ya watu, mahali, kampuni, nchi, milima, mito, siku za juma, masomo, miezi, namba, miaka, nk. - Mfano wa majina ya pekee ni:(i) Majina ya watu, mfano: Zengo, Brighton, Aneth, Heavenlight, Mboje, Omari, n.k (ii) Majina ya siku za juma, mfano; Jumatatu, Jumanne, n.k (iii) Majina ya miezi, mfano; Januari, Februari, Machi, n.k (iv)Majina ya mahali kama vile kijiji, wilaya, mtaa, mkoa, nchi, bara, nk. Mfano; Mapinga, Kilomo, Mapinduzi, Kunduchi, Mbezi, Ubungo, nk (v) Majina ya masomo. Mfano; Sayansi, Jiografia, Hisabati, nk

35

Sifa kuu za nomino za pekee ni kwamba; - Haziwezi kunyumbulishika - Hazina wingi - Huanza kuandikwa kwa herufi kubwa (ii) Nomino za kawaida - Haya ni majina ya kawaida yanayorejelea vitu mbalimbali, watu, wanyama, mahali, n.k. - Nomino hizi zinaweza kuwa katika umoja na wingi kulingana na ngeli yake. - Mfano; nyumba-nyumba, mbuzi-mbuzi, daktari-madaktari, mwalimu-walimu, soko - masoko, kalamu-kalamu, n.k Tanbihi: Nomino za kawaida zinapotumika kutambulisha au kurejelea nomino za pekee moja kwa moja, herufi ya kwanza huandikwa kwa herufi kubwa. Mfano; Mlima Kilimanjaro, Waziri Mwakyembe, Chifu Dadu, Mwalimu Mafuru, Daktari Malewa, n.k

(iii) Nomino za jamii - Nomino hizi hurejelea kundi la vitu, wanyama au watu kwa ujumla wake. - Aghalabu vitu hivi huwa katika kundi la vitu viwili au zaidi. - Nomino za jamii pia huitwa nomino za jumla au nomino za mafungu. Mifano; jozi ya viatu, doti ya khanga, umati wa watu, kundi la nyani, bustani ya maua, mbuga ya wanyama, kikosi cha askari, jeshi, bunge, timu, dazani, katoni, chama, halmashauri, tume, genge, baraza, kamati, mkutano, korija, n.k

(iv) Nomino za wingi Nomino hizi hurejelea vitu ambavyo kwa asili vipo katika wingi na haviwezi kuhesabika. Vitu kama hivyo tunatumia vipimo maalumu kujua kiasi chake. Nomino hizi kwa kawaida hazina umoja. Mfano wa nomino za wingi ni; maji, maziwa, mchanga, changarawe, pesa, nywele, ndevu, chumvi, sukari, n.k (v)Nomino za dhahania Haya ni majina ya hali au vitu ambavyo havionekani wala havishikiki. Tunaamini tu kuwa vipo na vinaishi. Mfano; upendo, hasira, ugonjwa, njaa, mapepo, malaika, umaskini, utajiri, uelewa, furaha, bahati, joto, uchovu, shetani, jinni, usingizi, upendo, n.k

36

ZOEZI LA 10 A. Jibu maswali kulingana na maelekezo 1. Uelewa wake ni mdogo. Neno uelewa ni aina gani ya nomino? 2. Baba yangu ni mwenyekiti wa mtaa. Neno mwenyekiti ni aina gani ya nomino? 3. Upele humwota asiye na kucha. Sentensi hii ina nomino ngapi? 4. Hasira za mkisi furaha za mvuvi. Neno lililopigiwa mstari ni aina gani ya nomino? 5. Tume ya taifa ya uchaguzi imevunjwa. Neno tume ni aina gani ya nomino? B. Pigia mstari nomino zote 1. Mungu hamtupi mja wake 2. Shetani ameuteka ulimwengu 3. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu 4. Alinunua sharubati 5. Chama chetu ni kikongwe 6. Mafuta ya alizeti ni aghali sana siku hizi 7. Ziwa Tanganyika lina kina kirefu 8. Mbu na dumizi ni wadudu hatari 9. Kamati imeongezewa siku 10. Alinunua korija mbili C. Taja aina kuu tano za nomino, kisha andika mifano miwili kwa kila aina uliyotaja D. Nini tofauti ya nomino pekee na nomino za kawaida?

8.2. Viwakilishi (W) - Viwakilishi ni maneno yanayosimama badala ya nomino katika sentensi - Alama inayowakilisha kiwakilishi ni (W). - Dhima kuu ya viwakilisha ni kusimama badala ya nomino katika sentensi. - Viwakilishi pia huitwa vibadala Aina za Viwakilishi Kuna aina kumi (10) za Viwakilishi. Kwa kifupi tunaita NASUSIA-PAM; yaani;-

N=nafsi, A=a-unganifu, S=sifa, U=ulizi, S=sisitizi, I=idadi, A=ashiria (onyeshi) P=pekee, A=amba-, M=milikishi (i) Kiwakilishi cha nafsi - Viwakilishi vya nafsi hutumika kuwakilisha nafsi katika umoja au wingi. - Viwakilishi vya nafsi vipo sita, kwa kifupi tunaita MIWEYE-SINYIWA; yaani:-

MI=mimi, WE=wewe, YE = yeye, SI = sisi, NYI = nyinyi, WA = wao

37

(ii) Kiwakilishi cha a-unganifu - Kiwakilishi cha a-unganifu huwakilisha nomino kwa kutaja kinachomiliki nomino hiyo. - Huundwa na mwambatano wa kiambishi cha nafsi au cha ngeli na mofimu a, kisha nomino nyingine yaani –a +N V Mfano:- Cha mlevi huliwa na mgema - Za watoto zimeiva - Cha mtu ni mavi - Ya mama imemwagika - Vya mwalimu vimeisha, n.k

(iii) Kiwakilishi cha sifa - Viwakilishi vya sifa hurejelea sifa ya nomino bila kuitaja. Kwa mfano; - Mzuri amewasili - Mtanashati ametuaga - Vyekundu vimeisha

(iv) Kiwakilishi kiulizi - Viwakilishi viulizi hutumika kuuliza nomino inayorejelewa. Mfano; (i) Vingapi vinatakiwa? (ii) Zipi zimepotea? (iii) Nani amekuja? (iv)Wapi hapana majimaji? (v) Yule kijana alikupatia nini?

(v)Kiwakilishi kisisitizi - Viwakilishi visisitizi hutumika kuonyesha msisitizo. Mfano; - Huyuhuyu ndiye aliyetukana - Haohao ndio waliokutukana - Hapahapa ndipo walipohitilafiana

(vi) Kiwakilishi cha idadi - Kiwakilishi cha idadi hutaja idadi ya nomino zinazorejelewa. - Mfano; wawili, wachache, wengi, n.k. - Kuna aina mbili za viwakilishi vya idadi

38

(a) Viwakilishi vya idadi dhahiri, mfano; wawili, mmoja watano, ishirini, n.k (b) Viwakilishi vya idadi isiyo dhahiri, mfano; wachache, wengi, kadhaa, nk

(vii) Kiwakilishi kiashiria (onyeshi) - Hudokeza umbali wa kitu au mtu toka kwa mzungumzaji. - Aidha hurejelea nomino bila kuitaja. Mfano; hiki, kile, huku, yule, pale, hapa, humo, kule, hao, mle, wale n.k

(viii) Kiwakilishi cha pekee - Kiwakilishi cha pekee hurejelea nomino isiyotajwa. - Viwakilishi vya pekee vipo katika makundi manne yafuatayo:(a) Vya –ote. Mfano; Yeyote aje (b) Vya –enye. Mfano; Wenye vitabu wamekuja (c) Vya –enyewe. Mfano; Mwenyewe hataki (d) Vya –ingine au engine. Mfano; Kingine kimepatikana, wengine wameondoka

(ix) Kiwakilishi kirejeshi (amba-) Kiwakilishi cha amba hurejelea nomino isiyotajwa kwa kutumia maumbo ya amba-. Mfano; - Ambalo limepotea - Ambaye hajaoa - Ambacho kinakufaa - Ambamo ameingia

(x) Kiwakilishi kimilikishi Kiwakilishi cha kumiliki huonyesha nomino inamiliki nini kulingana na ngeli yake. Kwa mfano; - Kwetu hakuna longolongo - Zao zimeharibika - Kwao kunaudhi - Chetu ni kizuri - Letu limeharibika

39

ZOEZI LA 11 1. Maneno huyu, wale, ambao, mfupi na zile yakitumika pamoja na vivumishi hufanya kazi gani? 2. La mgambo likilia kuna jambo. “La mgambo” ni aina gani ya kiwakilishi? 3. Yeyote atakayekuja anione. Yeyote ni aina gani ya kiwakilishi? 4. Changu ni cheusi, chake ni cheupe. Sentensi hii ina viwakilishi vingapi? 5. Alisema yeye hana ubaya na mtu. Kiwakilishi katika sentensi hii ni kipi? 6. Chetu kinaongoza. Chetu ni aina gani ya kiwakilishi? 7. Nani atakuwepo? Kiwakilishi ni nini? 8. Mamia walimlaki Rais. Neno gani ni kiwakilishi? 9. Neno linalosimama badala ya nomino katika sentensi huitwaje? 10. Mimi na wewe ni maadui. Sentensi hii ina viwakilishi vingapi?

8.3. Vivumishi (V) - Vivumishi ni maneno yanayoelezea zaidi juu ya nomino, kiwakilishi au kivumishi kingine. Pia huitwa visifa - Kivumishi huwakilishwa na herufi (V)

Aina za vivumishi Kuna aina kumi (11) za vivumishi. Kwa kifupi KASUSIA-PAMJI; yaani:-

K=kimfanano, A=a-unganifu, S=sifa, U=ulizi, S=sisitizi, I=idadi, A=ashiria (onyeshi) P=pekee, A=amba-, M=milikishi, JI=jina kwa jina (nomino kwa nomino) (i) Vivumishi vya kimfanano Hutumika kulinganisha sifa ya nomino na hali au tabia nyingine. Vivumishi hivi hutanguliwa na nomino au kiunganishi cha a-unganifu na huchukua mofimu ki-. Yaani; N + (-a + ki + N) V Mifano; - Anaishi maisha ya kimaskini T N (-a ki +N) V - Amevaa mavazi ya kifalme T N (-a ki+N) V -

Anapenda mziki wa kizungu T N (-a ki +N) V

40

-

Ana sauti ya kitoto t N (-a ki+N) V

(ii) Vivumishi vya a-unganifu Vivumishi hivi hueleza zaidi kuhusu nomino kwa kuonyesha kitu kinachomiliki nomino hiyo. Huundwa kwa kuambatisha kiambishi cha nafsi au ngeli pamoja na kiambishi –a cha a-unganifu, kisha nomino. Yaani; (-a + N) V Mfano; - Watoto wa mama wana tabia nzuri N (-a N) t N V V -

Chai ya mwalimu imemwagika N (-a N) T V

-

Mtoto wa marehemu anaumwa N (-a N) T V

(iii) Vivumishi vya sifa Vivumishi vya sifa hutoa sifa ya nomino. Mfano; - Yule mama mweusi - Mvulana mkorofi - Tabia mbaya - Suti nzuri

(iv) Vivumishi vya kuuliza Hutumika kuuliza swali kuhusu nomino inayoandamana nayo. Mfano; - Watoto wangapi? - Wanafunzi wangapi wameshindwa? - Umefika eneo gani? - Watoto wangapi wanaumwa?

41

(v)Vivumishi vya kusisitiza Husisitiza nomino fulani kwa kurudia rudia. Kwa mfano; - Jahazi hilihili - Mtoto huyuhuyu - Vijana hawahawa - Wembe uleule - Ng’ombe wale wale

(vi) Vivumishi vya idadi Hutueleza zaidi kuhusu kiasi au idadi ya nomino. Kuna aina mbili za vivumishi vya idadi - Idadi dhahiri, mfano; Mtoto mmoja, kumi, watatu, n.k - Idadi isiyo dhahiri, mfano; wachache, nyingi, kidogo, n.k

(vii) Vivumishi vya kuonyesha Hutumika kuonyesha nomino kulingana na mahali toka mzungumzaji hadi nomino hiyo ilipo. Maneno kama; hapa, huyu, hili, huku, haya, ule, wale, pale, hapo, huyo, hiyo, hicho, pale, lile, kile, n.k ni vivumishi vya kuonesha Mfano;- Mtoto huyu ni mtundu - Jani hili linawasha - Tupa mpira huo

(viii) Vivumishi vya pekee Vivumishi vya pekee vipo vya aina nne (4) ikiwa ni pamoja neno pekee lenyewe

(a) Vya –ote. Mfano: Kitabu chochote kinafaa Kalamu yoyote inafaa Mtu yeyote aje hapa Jambo lolote linawezekana Mahali popote tutaenda

(b) Vya –enye. Mfano: Kopo lenye maziwa Kitabu chenye picha Watu wenye ulemavu Mahali penye unyevunyevu

42

(c) Vya –enyewe Mfano: Mtu mwenyewe haeleweki Kitabu chenyewe ni aghali mno Mahali penyewe panatisha

(d) Vya –ingine au -engine Mfano: Mgonjwa mwingine amelazwa Chakula kingine kimepikwa Yule mwingine alitoroka Watu wengine hawana ubinadamu Vitu vingine havifai

(ix) Vivumishi vya ambaHurejelea nomino kwa kutumia mofimu rejeshi aghalabu zenye umbo amba-. Mfano: - Msichana ambaye amekuja ni dada yangu - Mzee ambaye amefariki - Pipa ambalo umelileta jana - Mti ambao umeanguka ni wetu

(x) Vivumishi vya kumiliki Huonyesha nomino inamiliki nini kwa kutumia viungo vimilikishi kama vile-angu, -ako, ake, -etu, -enu, -ao, n.k Mifano: Tumia talanta yako vizuri Gauni lako zuri Sanduku langu limechakaa Maisha yetu yako hatarini (xi) Vivumishi vya jina kwa jina au nomino kwa nomino Mfano: - Mbwa mwitu ni wakali - Mama ntilie nitilie mboga kidogo - Mama lishe amepika ubwabwa mtamu - Askari kanzu wawili walikuja

43

ZOEZI LA 12 1. Maneno huyu, mpole, mwembamba, mweusi, mkali, zile na hiki yakitumika pamoja na nomino hufanya kazi gani? 2. Juma ni mtoto pekee kwa wazazi wake. Neno pekee ni aina gani ya kivumishi? 3. Watu wote wa Mungu wamwabudu yeye. neno wote ni aina gani ya kivumishi? 4. Mtoto wa mama analia. Kivumishi katika sentensi hii ni ……………………. 5. Musa alivalia vazi la kifalme. Kivumishi ni ………………………… 6. Suti yangu ilishonwa na fundi mzoefu. Neno mzoefu ni kivumishi gani? 7. Mtoto ambaye anaumwa aje hapa. Kivumishi katika sentensi hii ni ………………….. 8. Watu wengi hawapendi uchafu. Wengi ni aina gani ya kivumishi? 9. Sitaki nione mtu yeyote hapa. Neno yeyote ni aina gani ya kivumishi? 10. Wanafunzi wangapi wameripoti?. Wangapi ni aina gani ya kivumishi? 11. Andika aina nya kivumishi kilichokolezwa wino (i) Chai ya mwalimu imemwagika (ii) Mtoto mzuri analia (iii) Kibatara ni wakili mahiri (iv) Mtoto huyu anaumwa (v) Walevi walewale walikuwepo (vi) Ng’ombe mwenye tume ndiye achinjwaye (vii) Maisha yetu ya hatarini (viii) Alivaa vazi la kihuni (ix) Walimu sita wameajiriwa (x) Watu wengine wanaudhi mno

8.4. Vitenzi (T) Vitenzi ni neno linaloeleza tendo ama lililofanyika, linalofanyika au litakalofanyika. Aina za vitenzi Kuna aina kuu tatu (3) za vitenzi. (a) Vitenzi vikuu (T) (b) Vitenzi visaidizi (Ts) (c) Vitenzi vishirikishi

(i) Vitenzi vikuu (T) Hivi ni vitenzi vinavyorejelea kitendo moja kwa moja. Mfano; - Waziri Aneth aliwasili jana - Kasimu anatapika - Funga mlango

44

(ii) Vitenzi visaidizi (Ts) Vitenzi visaidizi hutumika kusaidia vitenzi vikuu katika sentensi ili kuleta maana iliyokusudiwa kulingana na wakati au hali. Vitenzi visaidizi haviwezi kukaa pekee yake katika sentensi ni lazima viandamane na kitenzi kikuu. Mwandamano wa vitenzi viwili au zaidi katika sentensi; kwa mfano Ts+Ts+T huitwa vitenzi sambamba Mifano; (i) Baba anapenda kulima N Ts T (ii) Hajaanza kufanya kazi Ts T (iii) Maliza kufyeka nyasi zote Ts T N V (iv)Anataka kuanza kulima Ts Ts T (v) Angali analima mpunga Ts T N (iii) Vitenzi vishirikishi (t) Vitenzi vishirikishi hutumika kuelezea hali au mazingira yaliyopo au yasiyokuwepo kwa nomino, kiwakilishi au hali Kuna aina kuu mbili za vitenzi vishirikishi navyo ni (a) vitenzi vishirikishi vikamilifu (b) vitenzi vishirikishi vipungufu

Vitenzi vishirikishi vikamilifu Mfano: (i) Wewe u mtundu (ii) Sara yuko Morogoro kikazi (iii) Hassan yu kipofu (iv)Baba ana gari zuri (v) Ilikuwa baridi mno (vi)Maji yamo mtungini (vii) Huyu siye tuliyempendekeza (viii) Kalamu hii i mpya (ix)Shule yetu haikuwa chafu (x) Mimi ni mtoto

45

Vitenzi vishirikishi vipungufu (pia huitwa vitenzi vya ndi-) Mfano: (i) Aneth ndiye Mkurugenzi wa Kampuni ya BriAn (ii) Huku ndiko kulikoibiwa (iii) Huyu siye mhusika (iv)Hicho ndicho chenyewe (v) Pale ndipo penyewe (vi)Wewe ndiwe mziwanda wanhu (vii) Wao ndio waliotutukana (viii) Hivi ndivyo tutakavyowafanya (ix)Hilo ndilo lililotokea (x) Hizi ndizo kanuni zetu

ZOEZI LA 13 1. Taja aina kuu tatu za vitenzi na alama zake 2. Pigia mstari vitenzi vyote (i) Baba anasoma gazeti (ii) Mama anapika (iii) Mimi nilikuwa ninasoma (iv) Mjomba alikuwa mgonjwa (v) Wewe u hodari sana (vi) Amina yu buge (vii) Yeye ndiye mkuu wetu (viii) Musa angali usingizini (ix) Issa alikuwa anajisomea chumbani mwake (x) Shule yetu haikuwa chafu 3. Andika aina ya kitenzi kilichokolezwa wino (i) Wewe u mpole (ii) Mimi ndimi mkurugenzi hapa (iii) Amina yuko Arusha kikazi (iv) Yule siye tuliyempendekeza (v) Chai imo birikani (vi) Kule ndiko kuliko na viwanda vingi (vii) Mbuzi hulia mee mee (viii) Mwalimu alitufundisha kunyamaza (ix) Si busara kuwa waropokaji (x) Kaka ana mke 4. Changanua sentensi zifuatazo (i) Mimi ni hodari wa vita (ii) Jasiri haachi asili (iii) Mkataa kwao ni mtumwa (iv) Wewe hustahili kuonewa kabisa (v) Baada ya dhiki faraja

46

8.5. Vielezi (E) - Vielezi ni maneno yanayoelezea zaidi juu ya vitenzi, vivumishi, hali na vielezi vingine - Alama inayowakilisha vielezi ni herufi kubwa (E) Aina za vielezi - Kuna aina kuu NNE (4) za vielezi. (a) Vielezi vya wakati au muda (b) Vielezi vya idadi au kiasi (c) Vielezi vya namna au jinsi (d) Vielezi vya mahali - Kwa kifupi WA-I-NA-MA; yaani:-WA-wakati, I-idadi, NA-namna, MA-mahali

(i) Vielezi vya wakati - Vielezi vya wakati huelezea zaidi kuhusu lini tendo lilifanyika au litafanyika. - Hujibu swali lini? Mfano; asubuhi, jioni, mchana, mwakani, wiki ijayo, juzi, jana, usiku, kesho, leo, kutwa, Chunguza sentensi hizi: - Nitarejea Ijumaa ijayo - Ilinyesha kutwa - Walipigana usiku kucha

(ii) Vielezi vya idadi - Vielezi vya idadi hutuelezea kitendo kinafanyika, kilifanyika, kimefanyika, au kitafanyika mara ngapi. - Hujibu swali mara ngapi? Kuna aina mbili za vielezi vya idadi

(i)

Vya idadi kamili/halisi/dhahiri

Hivi hutaja dhahiri ni mara ngapi tendo lafanyika, litafanyika au limefanyika. Mfano; (a) Mathayo alinizaba kofi mara tatu (b) Meza vidonge viwili mara mbili kwa siku (c) Rejea hospitali siku tatu baada ya dozi

(ii)

Vya idadi isiyodhihirika

Hivi havitaji idadi dhahiri. Mfano; mara kadhaa, mara kwa mara, kadha wa kadha, aghalabu, mara chache, mara nyingi, nadra, nk

47

Chunguza sentensi hizi:(a) Huja mara kwa mara (b) Aghalabu hutembeleana (c) Ni nadra sana kuonekana

-

(iii) Vielezi vya namna Vielezi vya namna huelezea namna kitendo kinavyofanyika, kilivyofanyika, kitakavyofanyika au jinsi ambavyo hufanyika. Vielezi vya namna au jinsi hujibu swali; jinsi gani? au namna gani?

Mfano: (a) Anacheza kitoto (b) Anaandika vizuri (c) Aliongea vibaya (d) Alikuwa anatembea harakaharaka (e) Anatembea kwa madaha (f) Alinguka puu! (g) Lilitumbukia chubwi! (h) Alilia mee! (i) Yalimwagika pwaa!

(iv) Vielezi vya mahali - Vielezi hivi hutoa habari kuhusu mahali ambapo tendo linafanyika lilifanyika, litafanyika au hufanyika. - Hujibu swali; wapi? Mfano; (i) Alitoka Arusha (ii) Amepitia sokoni (iii) Anaenda Kigoma, n.k.

Miundo ya vielezi vya mahali Kuna miundo miwili (a) Nomino pekee ya mahali. Mfano: Alikwenda Arusha, Tulizuru Marekani (b) Nomino ya kawaida + ni. Mfano: shule +ni = shuleni, nyumba+ni = nyumbani

Chunguza sentensi hizi: (i) Msipitie sokoni (ii) Tutakutana kanisani (iii) Amekula hotelini (iv)Tutaenda mbinguni (v) Walikutana Ulaya

48

ZOEZI LA 14 A. Vielezi ni nini? B. Pigia mstari maneno yote ambayo ni vielezi 1. Aghalabu hututembea kwetu 2. Mwalimu atafika kesho 3. Ilinyesha kutwa nzima 4. Nimefarijika mno 5. Amerejea kwao Canada 6. Anacheza kitoto 7. Alijificha shimoni 8. Nenda shule haraka 9. Mwaju huchelewa mara kwa mara 10. Yamejaa pomoni. 11. Ilikuwa baridi kupindukia 12. Upupu ulimwagwa pote 13. Alisoma vizuri mno 14. Fimbo ile nyeusi imevunjika vipandevipande 15. Waliingia darasani mmoja mmoja

8.6. Viunganishi (U) - Viunganishi ni maneno yanayotumika kuunganisha, kujumuisha, kulinganisha, kutofautisha, kuonyesha sababu, matokeo, masharti, uwezekano na kuhusianisha dhana mbili au zaidi. - Pia huitwa viungo

Dhima za viunganishi Viunganishi vina dhima au kazi zifuatazo:1. Kuonyesha umiliki wa mahali, sababu, ala, mbinu n.k. Mfano; - Uwanja wa nyumbani - Amekata kwa kisu, nk - Wamekuja kwa basi 2. Kujumuisha. Mfano; - Licha ya umaskini ana ukoma - Kivumishi hutokea baada ya kivumishi kingine 3. Kuhusianisha Mfano; - Kutokana na ujinga wako utakiona cha mtema kuni - Nipo hapa kwa minajili ya mwanangu

49

4. Kuonyesha tofauti (jambo kufanyika kinyume cha matarajio) Mfano; - Juma anaimba ingawa anaumwa - Nomino ni jina ilhali kivumishi ni kisifa 5. Kuonyesha sababu Mfano; - Nimefika ili nikusaidie - Madhali upo hapa nisaidie 6. Kuonyesha matokeo Mfano; - Ndiposa ikawa hivyo - Hivyo wakatawanyika 7. Kuonyesha kitu kimoja kama sehemu ya kingine Mfano; - Miongoni mwao yupo Asheri - Baadhi ya majina ya dhahania ni njaa, upole na amani 8. Kuonyesha kitendo kufanyika baada ya kingine Mfano; - Fagia halafu usome - Kusanya matunda haya kisha uyaoshe 9. Kuonyesha kitu kufanyika badala ya kingine. Mfano; - Amekuja kwa niaba ya bosi wake - Umeleta pilipili mbuzi badala ya hoho? 10. Kulinganisha Mfano; - Kile kisu ni kama chetu - Wewe na yule ni sawa tu 11. Kuonyesha uwezekano Mfano: - Pengine ungempigia angekuelewa - Ungewahi huenda ungemkuta 12. Kuonyesha masharti Mfano; - Usifanye mambo al-muradi unafanya, zingatia vigezo - Ikiwa utakuja saa mbili utanikuta

50

ZOEZI LA 15 Pigia mstari viunganishi vyote 1. Anatambaa huku akitaga 2. Baba na mama wanalima 3. Napita njia hii kwa sababu ni salama 4. Nimekuja hapa ili nikusaidie 5. Aliwahi ingawa alikuwa anaumwa 6. Nomino ni jina ilhali kitenzi ni tendo 7. Amekula lakini hajashiba 8. Hawakuiba ila walisingiziwa tu 9. Hakula wala kunywa 10. Walikula chakula kisha wakanywa sharubati 11. Ikiwa utakuja saa mbili utanikuta 12. Pika halafu usome 13. Miongoni mwao yupo Iskanda 14. Baadhi ya majina ya dhahania ni upepo, njaa na hasira 15. Hivyo wakatawanyika

8.7. Vihisishi (H) - Kihisishi ni neno linaloonyesha hisia za mzungumzaji mathalani furaha, huzuni, uchungu, hasira, mshangao, nk. - Aghalabu vihisishi huambatana na alama ya hisi (!) - Vihisishi pia huitwa viingizi - Baadhi ya maneno ambayo ni vihisishi ni pamoja na Lo! Salaale! Kumbe! Ng’o! Akh! Aka! Ah! Ala! Haha! Mmh! Haya! Enhee! Ebo! Wee! La! Hoyee! Huraa! Oh! Naam! Masikini! Jamani!, nk

ZOEZI LA 16 1. Changanua sentensi zifuatazo (i) Abdallah na Aman wanakimbizana (ii) Aneth ni mtoto mzuri sana (iii) Licha ya kumiliki bajaji anafuga nyuki (iv)Darasa letu halikuwa chafu (v) Oh! Umekuja? (vi)Aliyekupa wewe kiti ndiye aliyenipa mimi kumbi (vii) Mama, dada na mimi tunaenda Moscow (viii) Alisema yeye hana ubaya wowote na mtu yeyote (ix)Watoto wa mfalme ni wepesi kujificha (x) Nzi hatui katika damu ya simba

51

2. Andika alama inayowakilisha aina ya neno lililokolezwa wino (i) Hairuhusiwi mtu yeyote kuingia humu pasi na ruhusa yangu (ii) Sweta lake lilishonwa na fundi mzoefu (iii) Nenda shule haraka (iv)Anarose ni mpole sana (v) Brighton na mama yake wamependeza (vi)Shule yetu ni maarufu sana (vii) Ng’ombe mwenye tume aliyeletwa juzi asubuhi amechinjwa (viii) Simba mwenda pole ndiye mla nyama (ix)Duh! Haya mambo ni hatari sana (x) Kamwe sitokusamehe 3. Changanua sentensi zifuatazo (a) Cha mlevi huliwa na mgema (b) Miriamu amevaa vazi la kijeshi (c) Kadogoo anacheza kitoto (d) Wewe na Musa hamkuwepo (e) Mtu mwenyewe chambega yule 4. Ainisha maneno yaliyokolezwa wino (a) Mvumilivu hula mbivu (b) Upendo alipendwa na watu kwa sababu ya upendo wake (c) Hasira hasara (d) Shetani ameuteka ulimwengu (e) Maji yakimwagika hayazoleki (f) Musa yupo pale anacheza (g) Wewe u msumbufu sana (h) Baba hakuwa na kipingamizi (i) Upele humwota asiye na kucha (j) Kubali yaishe 5. Jibu maswali yafuatayo (a) Ng’ombe mwenye tume ndiye achinjwaye. Neno lipi ni kivumishi? (b) Mtoto wa samaki ni kichengo. Changanua sentensi hii (c) Ambacho kimefubaa ni chake. Neno chake limetumika kama aina gani ya neno? (d) Mamia walimlaki rais. Kiwakilishi ni neno gani? (e) Kule hapakuwa na mtu yeyote. Changanua sentensi hii

52

9 AINA NNE ZA SENTENSI Sentensi ni nini? Sentensi ni kipashio cha juu kabisa katika tungo chenye muundo wa kiima na kiarifu ambacho hutoa taarifa kamili. Sehemu kuu mbili za Sentensi Sentensi za Kiswahili huundwa na sehemu kuu mbili ambazo ni KIIMA (K) na KIARIFU (A) Kiima (K) ni nini? Kiima (K) ni kifungu cha maneno katika sentensi ambacho hutangulia kitenzi, aghalabu huonyesha mtenda wa tendo. Mfano; Baba yangu katika sentensi Baba yangu analima Kiarifu (A) ni nini? Kiarifu (A) ni sehemu ya sentensi yenye kitenzi pamoja na vijalizo vyake kama shamirisho au chagizo. Mfano; analima katika Baba yangu analima Shamirisho ni nini? Shamirisho ni neno linaloashiria kitendwa au yambwa katika sentensi. Mfano; Katika sentensi “Kibaka amemwibia Ali nauli yake”. (i) Yambwa/Kitendwa au shamirisho: nauli (ii) Yambiwa/Mtendewa: Ali (iii) Mtenda: Kibaka Kumbuka kuwa; • Yambiwa ni kipashio cha sentensi kinachofanyiwa au kinachotendewa tendo. Au ni nomino ambayo kwayo tendo linafanyika. Yambiwa pia huitwa Mtendewa (Indirect Object) •

Yambwa ni kipashio cha sentensi kinachopokea tendo. Ni nomino inayotendwa. Yambwa pia huitwa Kitendwa au Mtendwa (Direct Object)

Chagizo ni nini? Chagizo ni neno linalochukua nafasi ya kielezi katika sentensi. Mfano; Jeni aliibiwa nauli yake kizembe sana

53

Aina za Sentensi Kuainisha sentensi ni kutaja aina za sentensi. Uanishaji wa Sentensi ni uwekaji wa sentensi katika makundi kulingana na mikabala anuwai. Kimuundo, kuna aina kuu nne (4) za sentensi - Sentensi Sahili - Sentensi Changamano - Sentensi Ambatano - Sentensi Shurutia

9.1. Sentensi Sahili - Neno sahili maana yake rahisi, nyepesi, isiyo na ugumu. Kwa hiyo sentensi sahili ni sentensi ambayo inatoa ujumbe rahisi unaoeleweka. - Sentensi sahili pia huitwa sentensi huru au huria - Sentensi sahili huundwa na kishazi huru kimoja na huelezea tendo moja tu. Mfano; Wanafunzi wanafanya mtihani

Muundo wa Sentensi Sahili (i) Kitenzi kikuu (T) peke yake. Mfano; Gari limeanguka (ii) Kitenzi kikuu (T)+kitenzi kisaidizi (TS) Mfano; Masanja hakutaka nipate utajiri (iii) Kitenzi shirikishi (t). Mfano; Kiswahili ni tunu ya Taifa

Sifa za Sentensi Sahili -

Ina kiima na kiarifu Haifungamani na sentensi nyingine, inajitosheleza kimuundo na kimaana

Mifano ya sentensi sahili 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7.

Mama anapika ubwabwa Mimi ninacheza rede Wambura anafundisha darasani Amina atakuwa anaimba kwaya Yeye alikuwa mgonjwa Kuku ametaga amayai manne Mwalimu anafundisha vizuri

9.2. Sentensi Ambatani - Hii ni sentensi inayojengwa na sentensi mbili au zaidi zilizounganishwa kwa kutumia viunganishi kama vile lakini, wala, au, na, japokuwa, ingawa, ilhali, n.k. - Kimsingi sentensi hii ina matendo mawili (vitenzi vikuu viwili)

54

Muundo wa Sentensi Ambatani (i) Sentensi sahili tu. Mfano; Mwalimu anafundisha wakati wanafunzi wanapiga kelele (ii) Sentensi sahili na changamano. Mfano; Walinzi waliposhindwa polisi waliwasaidia lakini hawakuweza kuwakamata majambazi (iii) Sentensi changamano tu. Mfano: Barabara zilizojengwa na wakoloni zimedumu hadi leo wakati zile zinazojengwa na Wachina hata mwezi hazifikishi

9.3. Sentensi Changamani - Sentensi Changamani ni sentensi yenye kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au zaidi - Kishazi ni miongoni mwa aina 4 za tungo; zingine ni neno, sentensi na kirai. - Kirai ni tungo yenye kitenzi, kitenzi ambacho chaweza kuwa kinajitosheleza au hakijitoshelezi kimaana. Kuna aina kuu mbili (2) za vishazi; kishazi huru (k/hr) na kishazi tegemezi (k/tg) (a) Kishazi huru ni tungo inayotawaliwa na kitenzi kikuu, ambacho kwa kawaida hutoa ujumbe unaojitosheleza. Mfano; Mzee analima (b) Kishazi tegemezi ni tungo ambayo inatawaliwa na kitenzi kisaidizi, ambacho kwa kawaida hutoa ujumbe usiojitosheleza kimaana. Mfano: Mbuzi aliyevunjika mguu. KUMBUKA: - Kishazi tegemezi pia huitwa sentensi tegemezi au tungo tegemezi - Kwa hiyo, sentensi changamani ni muungano wa kishazi tegemezi na kishazi huru (K/Tg+K/Hr) Chunguza sentensi hizi (i) Gari lililopinduka jana jioni/ halikuharibika hata kidogo k/tg k/hr (ii) Watoto walioletwa juzi /wamepatikana k/tg k/hr (iii) Nyumbu aliyepigwa risasi /amekufa k/tg k/hr (iv)Aliwaarifu /aje hapa k/tg k/hr

55

(v) Mtoto ambaye anaumwa /aende hospitali k/tg k/hr

9.4. Sentensi Shurutia Sentensi shurutia ni sentensi ambayo inaundwa kwa mofimu za masharti ki, nge, ngeli na ngali Mfano: (i) Ukija utanikuta (ii) Angemsikiliza mwalimu asingeumia (iii) Usipoziba ufa utajenga ukuta (iv)Ukitaka kuruka agana na nyonga (v) Angelijua ukweli wa mambo mapema asingeteseka (vi)Ukimuona kimbia (vii) Angalilima shamba kubwa angalipata mavuno mengi

ZOEZI LA 17 1. Kipashio cha juu kabisa katika tungo chenye kiima na kiarifu huitwaje? 2. Bainisha mtenda, mtendwa na mtendwa katika sentensi hii; “Hassan amempigia Hamis mpira” 3. Andika maana nne za sentensi hii; “Baba amempigia simu kaka” 4. Taja aina nne za sentensi kimuundo 5. Ainisha tungo zifuatazo:(i) Kiti kilichovunjika (ii) Simutamba yangu ni mbovu, yake ni mpya (iii) Ingawa anaumwa anatembea harakaharaka (iv) Wanafunzi waliotoroka waliadhibiwa na kutakiwa kuja na wazazi (v) Ukitaka kuruka agana na nyonga (vi) Usipoziba ufa utajenga ukuta (vii) Aliokota nazi chini ya mtende (viii) Aliyempiga aje hapa (ix) Anataga huku anatembea (x) Baba na mama wamesafiri (xi) Nimenunua bamia na njegere (xii) Ninasoma 6. Bainisha kishazi tegemezi na kishazi huru katika sentensi zifuatazo (i) Ndiposa wale walioshinda alitunuku zawadi njema (ii) Mtu ambaye hapendi ushirikiano simtaki hapa (iii) Kuku yule mweusi mwenye kilema aliyeletwa na kaka jana ameuzwa (iv) Viti vyote vilivyopambwa vimeuzwa (v) Palipobomoka pamezibwa

56

10 KAULI HALISI NA KAULI TAARIFA Kauli ni nini? Kauli ni maneno yanayotamkwa; usemi, tamko, kalmia au tamshi. Kuna aina mbili za kauli (a) Kauli halisi (b) Kauli taarifa 10.1. Kauli halisi - Kauli halisi ni kauli au maneno halisi ambayo msemaji mwenyewe huyatamka. - Kauli halisi pia huitwa usemi wa moja kwa moja. Mfano;• Kitabu hiki ni changu • Je, umemwona Hamisi? • Lo! Humwogopi hata nyoka? • “Nitaenda Morogoro kesho”, Aneth alisema Sifa bainifu za kauli halisi Kauli halisi inajipambanua na kujibainisha kwa kuwa na sifa zifuatazo (i) Hutumia alama za nukuu (“……”) Mfano; “Kitabu hiki ni kizuri”, Amina alisema (ii) Hutumia alama ulizi (?) Mfano; “Je, umemwona Ingramu?”, Asha aliuliza (iii) Hutumia alama ya hisi (!) Mfano; “Lo! Humwogopi hata nyoka?”, Shekhan alishangaa (iv)Njeo yoyote huweza kutumika Mfano; - “Nitaenda Singida kesho”, Zengo alisema (wakati ujao) (v) Hutumia nafsi ya kwanza zaidi Mfano;-ninaimba, tunaimba

57

Kanuni za matumizi ya alama za uakifishaji katika tungo za kauli halisi • Iwapo sentensi inaanza na maelezo ya mnenaji, koma hufuata maelezo hayo nacho kituo huwekwa mwishoni mwa maneno yanayonukuliwa. Mfano; Mwalimu aliniambia, “Kiweke kitabu chako mezani.” •

Iwapo sentensi inaanza na maneno yanayonukuliwa, koma huwekwa mwishoni mwa maneno hayo nacho kituo huwekwa mwishoni mwa maelezo ya mnenaji. Mfano; “Kiweke kitabu chako mezani,” mwalimu aliniambia.



Maelezo yanayofuata maneno yanayonukuliwa huanza kwa herufi ndogo. Mfano; “Mkate huu ni mtamu,” mtoto alisema.



Unapomnukuu mzungumzaji, alama za nukuu huwekwa baada ya kuweka koma, kituo, kihisi, kiulizi, n.k

ZOEZI LA 18 1. Kauli halisi ni nini? 2. Taja sifa bainifu za kauli halisi 3. Andika sentensi tano (5) zilizo katika kauli halisi 4. Badili sentensi zifuatazo ziwe katika kauli halisi i) Alisema kuwa kitabu chake kilikuwa kipya ii) Aliuliza sababu ya yeye kuchelewa iii) Alishangaa kuwa yule alikuwa mtoto iv) Alisema kuwa wangecheza siku hiyo uwanjani v) Alisema kuwa angeondoka siku iliyofuata 10.2. Kauli taarifa Kauli taarifa ni maelezo tu yanayoripoti yaliyosemwa na mtu mwingine hapo awali. Kauli taarifa pia huitwa usemi ripoti au usemi usio wa moja kwa moja Tofauti na kauli halisi, katika kauli taarifa alama za hisi, ulizi na nukuu hazitumiki kabisa. Aidha, aghalabu wakati uliopita hutumika zaidi Sifa linganifu za kauli halisi na kauli taarifa Kauli Halisi /Moja kwa moja Kauli Taarifa/Ripoti (i) Nafsi ya I na ya II hutumika Mimi Huwa nafsi ya III (yeye, wao) + kimbishi (ni-), wewe (u-), sisi (tu-) na ninyi cha njeo –li(m-) Mf; alilima, walilima Mf; ninalima, unalima, tunalima, mnalima (ii) Viashiria vya kwanza hutumika Huwa vya pili au tatu Mf; huyu, hiki, hapa, n.k Mf; huyo/yule, kile, pale, kule, n.k (iii) Vimiliki vya kwanza hutumika Huwa vya pili au tatu Mf; changu, chako, pangu, kwetu, petu, Mf; chake, pake, pao, n.k

58

n.k (iv) Mofimu ya masharti –ki- hutumika Mf; ukisoma, ukija, n.k (v) Kitenzi kishirikishi ni hutumika Mf; huyu ni kiduko, hiki ni kipya

Hubadilika na kuwa –ngeMf; angesoma, angekuja Hubadilika na kuwa katika muundo wa –

kuwa Mf; yule alikuwa kiduko, kile kilikuwa kipya Hubadilika na kuwa –ngeMf; angeimba, angeenda Wakati ule, siku ile, siku iliyofuata,

(vi) Mofimu ya njeo –ta- hutumika Mf; nitaimba, nitaenda (vii) Sasa, leo, kesho, jana

Sifa bainifu za kauli taarifa - Hutumia nafsi ya tatu - Hutumia wakati uliopita au mtimilifu - Haina alama za nukuu - Haina alama za hisi na ulizi ZOEZI LA 19 1. Andika kauli halisi zifuatazo katika kauli taarifa (ii) Kitabu hiki ni changu (iii) Je, umemwona Aisha? (iv)Lo! Humwogopi nyoka? (v) “Nitaenda Ulaya”, baba alisema (vi)Mama alisema, “Leta kikombe” (vii) “Leta mkate”, dada aliniambia. (viii) Mkate huu ni mtamu (ix)Naitwa profesa Ntale Nnoyi (x) “Nitaenda Nairobi”, shangazi aliniambia (xi)Jamani! Kumbe ni mtoto? 2. Andika sentensi zifuatazo katika kauli halisi (i) Brighton alisema kuwa yeye alikuwa anasoma kwa bidii (ii) Alimshauri mwanawe kuwa angesoma kwa bidii angefaulu mtihani (iii) Aneth alisema kuwa kitabu chake kilikuwa kipya (iv)Shangazi alisema kuwa angeondoka kuelekea ughaibuni siku iliyofuata (v) Mama Busalama alimwahidi mwanawe kuwa iwapo angefaulu mtihani angemtunza (vi)Mgeni alisema kuwa angeondoka siku ile (vii) Wanafunzi walisema kuwa wangecheza siku iliyofuata (viii) Kijakazi alisema kuwa angeenda sokoni siku hiyo (ix)Mama alishangaa kuwa huyo alikuwa ni mtoto (x) Alisema kuwa angeondoka siku iliyofuata 3. Lo! Humwogopi hata nyoka? Shekhan alishangaa na kuhoji. Andika katika kauli taarifa 4. Sinywi dawa tena. Kauli taarifa ya sentensi hii ni ipi?

59

11 UANDISHI WA BARUA Barua ni nini? Barua ni ujumbe wa maandishi unaoandikwa na kutumwa kwa mtu mwingine kwa njia ya posta, mtandao wa intaneti (barua pepe), simu, nukushi au kwa njia ya tarishi. Aina za Barua Kuna aina kuu mbili za barua. Nazo ni:(i) Barua ya kiofisi (ii) Barua ya kirafiki 11.1. Barua ya kirafiki - Barua ya kirafiki ni barua tunayoandika kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa madhumuni ya kuwasabahi, kuomba msaada, kuwapongeza, kuwashukuru, kuwatakia heri au kuwajulisha juu ya mambo kadha wa kadha - Barua ya kirafiki pia huitwa barua ya kindugu au barua isiyo rasmi Vipengele muhimu vya kuzingatia katika uandishi wa barua ya kirafiki 1. Anwani ya mwandishi 2. Tarehe 3. Mwanzo wa barua 4. Salamu au maamukizi 5. Madhumuni ya barua 6. Mwisho wa barua 7. Jina la mwandishi Muundo wa barua ya kirafiki Anwani ya Mwandishi Tarehe Mwanzo wa barua Salamu Madhumuni ya waraka Mwisho wa barua Jina la mwandishi

60

11.2. Barua ya kiofisi - Barua ya kiofisi pia huitwa barua rasmi au ya kikazi. - Kwa kawaida barua rasmi huandikwa kwa makusudi mbalimbali kama vile, kutoa taarifa za tukio fulani, kuomba kazi, kuagiza vifaa au vitu, kumwalika kiongozi katika shughuli maalumu, kutoa taarifa ya kushindwa kufika mkutanoni, n.k. Aina za barua za kikazi Barua za kikazi zipo za aina nyingi sana, kwa mfano: - Barua za kuomba kazi - Barua za maonyo - Barua za kupandishwa vyeo - Barua za kufukuzwa kazi - Barua za kuongezewa mshahara - Barua za kutoa taarifa - Barua za kibiashara (za kuagiza na kupokea bidhaa) - Barua za magazetini Muundo wa barua za kikazi Barua za kikazi huwa na vipengele kumi (10) vifuatavyo;-

(i) -

Anuani ya mwandishi

Anwani hii huandikwa pembe ya juu kulia ili kutambulisha maskani ya mwandishi Pia hutumiwa na mwandikiwa wakati wa kuijibu barua husika inapobidi.

(ii) Tarehe -

-

Tarehe ya siku ambayo barua imeandikwa. Tarehe huandikwa chini ya anuani ya mwandishi ili kumjulisha mwandikiwa kama barua hiyo imefika mapema au imechelewa. (iii) Kumbukumbu namba Barua rasmi huwa na kumbukumbu namba. Huu ni utambulisho maalumu wa barua husika. Kumbukumbu namba aghalabu huwa ni kifupi cha jina la taasisi inakotoka barua hiyo, kule inakokwenda, hiyo ni barua ya ngapi na mwaka husika. Mf: MBSS/CRDB/02/17

(iv)Anuani ya mwandikiwa -

Anwani hii hutanguliwa na cheo cha mwandikiwa na huwekwa upande wa kushoto chini ya kumbukumbu namba. Nafasi ya mstari mmoja au zaidi huweza kurukwa baina ya kumbukumbu namba na anuani ya mwandikiwa.

61

-

-

(v) Mwanzo wa barua Sehemu hii huandikwa chini ya anuani ya mwandikiwa. Ni heshima kutaja cheo cha mwandikiwa mwanzoni mwa barua ya namna hii, kwa mfano Ndugu Katibu, Ndugu Ofisa Mifugo, n.k. (vi)Kichwa cha barua Kichwa cha barua hutaja kwa ufupi jambo linalohusu barua hiyo. Kichwa cha barua huandikwa waziwazi katikati ya barua mara baada ya mwanzo wa barua. Ni muhimu kiwe kifupi na chenye kueleweka waziwazi. Hufaa zaidi kikiandikwa kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari. Hakipaswi kuzidi maneno matano.

(vii) Barua yenyewe -

Sehemu hii huandikwa mambo yote muhimu kuhusu barua yenyewe. Barua yenyewe iwe fupi na yenye taarifa za lazima tu. Uanzaji wa barua yenyewe umrejeshe msomaji kwenye mada ili kufupisha maelezo mengi kama vile kwa kusema: Mada tajwa hapo juu inahusika, Rejea barua yako ya tarehe…..yenye Kumb. Na…., Husiana na mada tajwa hapo juu, n.k.

(viii) Mwisho wa barua - Mwisho wa barua huwa ni tamko la heshima la kumalizia barua. - Mara nyingi mwisho unaotumika katika barua rasmi ni kama vile: Wako mtiifu, Wako katika ujenzi wa taifa, Wako katika kazi, n.k.

(ix)Saini na jina la mwandishi Mwisho wa barua mwandishi hupaswa kutia saini na jina lake kama utambulisho wake juu ya kilichoandikwa. Saini hupaswa kutiwa kwa mkono.

(x) Cheo cha mwandishi Baada ya jina mwandishi hupaswa kuandika cheo chake. Cheo kinaweza kuwa: Mwanakijiji, Muombaji, Mwalimu Mkuu, Afisa Mtendaji, n.k

62

11.3. Barua za kibiashara Barua ya kibiashara ni barua inayoandikwa kwa lengo la kuagiza bidhaa au kukiri kupokea bidhaa zilizotumwa. Muundo wa barua ya kibiashara Muundo wa barua ya kibiashara ni sawa kabisa na barua yoyote rasmi. Ina vipengele kumi (10) na hutumia lugha rasmi kama zilivyo barua zingine rasmi

Mfano wa barua ya kuomba kazi: KIJIJI CHA MTO WA MBU, S.L.P 124, ARUSHA-TANZANIA. KUMB NA: HWK/KMM/OKU/1/18

12-5-2018

MENEJA WA KIWANDA, KIWANDA CHA KUSINDIKA MATUNDA, S.L.P 717, IRINGA. Ndugu Meneja, YAH: OMBI LA KAZI YA UKARANI Husika na kichwa tajwa hapo juu. Ninayo heshima kuomba kazi ya ukarani katika kiwanda chako kama ilivyotangazwa kupitia gazeti la “Sanifu” Uk. 3 la tarehe 20/6/2017. Nilisoma katika kituo cha Elimu ya Watu Wazima huko Mufindi. Baadaye nilijiunga na masomo kwa njia ya posta na kuhitimu kwa ufaulu wa masomo ya Kiswahili, Siasa na Kiingereza. Nina umri wa miaka 45, nimeoa na nina watoto wanne. Mimi ni mwanakijiji wa kijiji cha Magadini. Napendelea michezo na kazi za mikono. Ninaweza kusoma na kuandika vizuri na ninayo hati nzuri. Mkuu wa Kituo cha Elimu ya Watu Wazima cha Mufindi na msimamizi wa masomo kwa njia ya posta anaweza kutoa taarifa zaidi juu ya uwezo wangu. Nitashukuru sana iwapo ombi langu litafikiriwa na kupokelewa vema. Wako mtiifu, MH MATATIZO HAYAISHI

MWOMBAJI

63

Mfano wa barua ya kutoa taarifa KIJIJI CHA JANGWANI, S.L.P 104 MONDULI-ARUSHA. KUMB NA: HWM/KJ/TSK/137/13

10/7/2017

AFISA WANYAMAPORI WA WILAYA, WILAYA YA MONDULI, S.L.P 1045, ARUSHA. Ndugu Afisa Wanyamapori, YAH: TATIZO LA SIMBA KIJIJINI KWETU Husika na mada tajwa hapo juu. Ninasikitika kukutaarifu kuwa, hapa kijijini kwetu amezuka simba anayewinda watu. Ni simba jike na watoto watatu na ameonekana mara tatu hapa kijijini. Simba huyo huingia hapa kijijini kutoka katika msitu wa hifadhi ya taifa ambapo si ruhusa kuweka mitego. Nitashukuru ikiwa utatushauri haraka jambo la kufanya mara upatapo barua hii. Wako katika kazi, MM MASANJA MASUNGA

MTENDAJI WA KIJIJI Mfano wa barua ya mwaliko SHULE YA SEKONDARI AHMES S.L.P 376, BAGAMOYO-PWANI KUMB NA: SSA/MKV/132/18

12.8.2017

MKUU WA WILAYA, WILAYA YA BAGAMOYO, S.L.P 1, BAGAMOYO. Ndugu Mkuu wa Wilaya,

64

YAH: MWALIKO WA KUKABIDHI VYETI Husika na kichwa cha barua hapo juu. Ninakualika uwe mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita yatakayofanyika hapa shuleni siku ya tarehe 20/7/2017 kuanzia saa saba za mchana hadi saa 12 jioni. Pia utatunuku vyeti vya kuhitimu kwa wahitimu 600 katika sherehe hiyo. Nitashukuru sana iwapo ombi letu litakubaliwa. Wako katika ujenzi wa taifa, EG EMMANUEL GWIMILE MKUU WA SHULE

Mfano wa barua ya kibiashara KIJIJI CHA MWAGWILA, S.L.P 109, MEATU- SIMIYU KUMB NA: HWM/KM/XIX/16

4-11-2016

MENEJA WA KIWANDA, KIWANDA CHA ZANA ZA KILIMO MBEYA, S.L.P 44, MBEYA. Ndugu Meneja, YAH: AGIZO LA ZANA ZA KILIMO Husika na kichwa cha barua hapo juu. Tunaomba ututumie zana za kilimo, kwani tunakusudia kuanzisha mradi wa kilimo cha mahindi hapa kijijini. Zana tunazohitaji kwa ajili ya mradi huu ni : 1. Majembe – 6 2. Mapanga – 10 Tunaomba utume kwa basi la NTALENDO TRANS linalofanya safari zake kila siku hapa Meatu. Kabla ya kutuma, tuandikie kutuarifu tarehe utakayotuma. Malipo yatalipwa kwa hundi. Wako katika ujenzi wa taifa, NK NYAMIZI KILOBOTO

MRATIBU WA MRADI

65

ZOEZI LA 20 1. Wewe ni Meneja Mradi wa Kilimo cha Mbogamboga wa Kikundi cha Hapa Kazi Tu cha S.L.P 86 Bariadi. Mwandikie Bw Matuja Ng’olo wa SLP 8 Meatu ambaye ni mfanyabiashara wa pembejeo za kilimo umuombe akupatie bei za bidhaa zifuatazo: mbegu za mchicha, mbegu za kabeji, mbegu za nyanya, mbegu za pilipili hoho, mbegu za karoti na mbegu za pilipili 2. Jifanye wewe ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Inonelwa ya S.L.P 74 Makomangwa, mwandikie Mkuu wa Wilaya yako ya Makomangwa umualike kuwa mgeni rasmi kwenye Sherehe ya Mahafali ya kuhitimu Elimu ya Msingi kwa vijana wako Desemba 3, mwaka huu. Katika shughuli hiyo, pamoja na mambo mengine atagawa vyeti kwa wahitimu 207. Jina lako ni Ngosha Adalemelagwa 3. Andika barua ya kuomba kazi ya ulinzi katika Taasisi ya Uhasibu tawi la Singida kama ilivyotangazwa katika gazeti Mwananchi la tarehe 7 Januari 2018. Elimu yako ni darasa la 7. Anwani yako ni Kijiji cha Mwabalebi S.L.P 56 Meatu na anwani ya Taasisi ni Meneja wa Tawi, Taasisi ya Uhasibu Tanzania, S.L.P 201 SINGIDA 4. Chora muundo wa barua rasmi ukionyesha vipengele vyake muhimu. 5. Bainisha toafuti baina ya barua rasmi na barua isiyo rasmi/kirafiki 6. Mwandikie baba barua yako umjulishe kuwa mtafunga shule tarehe 3 Desemba saa 4:00 asubuhi. Hivyo awahi kuja kukuchukua 7. Chora muundo wa barua ya kirafiki 8. Soma barua ifuatayo, kisha andika mambo matano yanayokosekana HOSPITALI YA MWAGWILA, S.L.P 901, MWANHUZI B…………………………… A…………………… MGANGA MKUU WA WILAYA, WILAYA YA MEATU, S.L.P 44, MWANHUZI Ndugu, C………………………………………………… Nasikitika kukujulisha kuwa ugonjwa wa kipundupindu umelipuka katika kata ya Mwanyahina. Tayari watu sita wamefariki kwa ugonjwa huo. Wataalamu wa afya wa Zahanati ya kata wameelemewa na wagonjwa. Pia, kuna uhaba mkubwa wa vifaa kama dawa, glavu na magodoro ili kukabili tatizo hilo. Tunaomba waganga sita na wauguzi kumi ili kuokoa maisha ya watu. D………………………………………… E………………… Dkt Nyalige Mganga Mkuu

66

12 SAUTI ZA LUGHA YA KISWAHILI 12.1. Dhana ya sauti za lugha Sauti ni ukemi unaosikika kutokana na mtetemo wa mkondo wa hewa unaofanywa na ala za matamshi kama vile mdomo, ulimi, nk Aidha, sauti za lugha ni herufi zinazotumika katika maandishi ya lugha husika Kila lugha ina mfumo wake wa uwasilishaji wa sauti kwa njia ya maandishi ujulikanao kama othografia. Kwa sababu hiyo, abjadi ya lugha ya Kiswahili ni seti ya herufi thelathini na moja (31) ambazo ndizo hutumika katika maandishi ya Kiswahili. Abjadi pia huitwa alfabeti au abtathi Abjadi ya Kiswahili iliyozoeleka na inayotumika hadi sasa ina asili yake ya kiuainisho kutoka kwa Ludwig Krapf na Edward Steere Zifuatazo ni herufi za abjadi zinazotumika katika maandishi ya maneno ya lugha ya Kiswahili zikihusishwa na sauti za lugha ya kiswahili Na Herufi Jina la herufi 1 A A 2 B Be 3 Che Che 4 D De 5 Dh Dha 6 E E 7 F Fe 8 G Ge 9 Gh Ghe 10 H He 11 I I 12 J Je 13 K Ke 14 Kh Khe 15 L Le 16 M Me 17 N Ne 18 Ny Nya 19 ng’ ng’a 20 O O 21 P Pe

67

22 23 24 25 26 27 28 29 30 31

R S Sh T Th U V W Y Z

Re Se Sha Te The U Ve We Ye Ze

Tanbihi: Kutokana na jedwali hapo juu utagundua kuwa kuna baadhi ya sauti ambazo kimaandishi huwakilishwa na herufi mbili (2). Herufi hizo ni ch, dh, gh, kh, ng’,ny, sh na th Hata hivyo, kimsingi herufi hizo mbili huwakilisha sauti moja (1) tu kimatamshi na SIYO sauti mbili kama maandishi yanavyoonesha. Aidha ni muhimu ifahamike kuwa lugha ya Kiswahili haina herufi Q na X kama ilivyo katika baadhi ya abjadi za lugha nyingine 12.2. Kategoria za Abjadi za Kiswahili Abjadi ya Kiswahili ipo katika makundi mawili; irabu na konsonanti 12.2.1. Irabu Irabu ni sauti ya lugha inayotamkwa bila kuwepo kizuizi chochote kwenye mkondo wa hewa kutoka mapafuni kupitia kinywani na puani. Pia huitwa vokali Kuna aina tano (5) za vokali au irabu; A, E, I, O, U 12.2.2. Konsonanti Konsonanti ni sauti ya lugha ambayo hutamkwa kwa kubana au kuzuia mkondohewa kutoka mapafuni kwenda nje kupitia ama chemba ya kinywa au ya pua. Katika lugha ya Kiswahili kuna konsonanti ishirini na sita (26) nazo ni ; B, CH, D, DH, F, G, GH, H, J, K, KH, L, M, N, NY, NG’, P, R, S, SH, T, TH, V, W, Y, Z. Konsonanti nane (8) ambazo ni ch, dh, gh, kh, ny, ng’, sh na th zinaundwa na herufi mbili ingawa huwakilisha sauti moja 12.3. Silabi za Kiswahili na Muundo wake Silabi ni kipashio kidogo cha kifonolojia ambacho hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Kwa mantiki hiyo, maneno ya lugha hutamkwa kwa kufuata utaratibu wa silabi. Kwa maneno mengine, silabi ni kitamkwa.

68

Kuna aina kuu mbili za silabi (ii) Silabi funge Silabi funge ni silabi ambayo huishia na konsonanti ambayo kilele cha mvumo wa sauti. Mfano; mkulima = m+ku+li+ma, abadan = a+ba+da+n, kemkem = ke+m+ke+m, nk (iii) Silabi huru Silabi huru ni silabi ambayo aghalabu huishia na irabu. Mfano: baba =ba+ba, ua = u+a, staftahi= sta+fta+hi, nk Muundo wa silabi za Kiswahili Ipo miundo kadhaa ya silabi za Kiswahili (i) Irabu pekee yake (I). Mfano; a katika neno asali =a+sa+li (ii) Konsonanti peke yake (K). Mfano; m katika neno mtu = m+tu (iii) Konsonanti na irabu (KI). Mfano; sa na li katika neno asali (iv) Konsonanti, Konsonati na Irabu (KKI). Mfano; kta na dha katika neno muktadha=mu+kta+dha, fta katika neno daftari=da+fta+ri na staftahi=sta+fta+hi, sta katika neno staftahi (v) Konsonati, konsonanti, konsonanti na irabu (KKKI). Mfano; spri katika neno springi = spri+ngi

ZOEZI LA 21 1. Andika idadi ya silabi katika maneno haya (i) Mbarika (ii) Ng’ombe (iii) Mhunzi (iv) Mchwa (v) Stakabadhi 2. Andika idadi ya aina za irabu katika maneno haya (i) Cherekochereko (ii) Morogoro (iii) Mlalahoi (iv) Afanaleki (v) Fistula 3. Andika idadi ya aina za konsonanti katika maneno haya (i) Mchakamchata (ii) Cherekochereko (iii) Msonobari (iv) Ng’ambo (v) Mchakato 4. Andika idadi ya konsonanti katika maneno haya (i) Muktadha (ii) Mpwapwa (iii) Mpingo

69

(iv) (v) 5. (i) (ii) (iii) (iv) (v) 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20.

Cherehani Fyatua Andika idadi ya aina za silabi katika maneno haya Cherekochereko Mchakamchaka Mtoto Mwandambo Kibibi Herufi hizi zinaitwaje? a, e, i, o, u ……………………………….. Herufi hizi zinaitwaje? b, ch, d, f, g, ………………………………. Herufi hizi zinaitwaje? a, b, ch, d, e, f, g ……………………………………. Ba, be, bi, bo, bu huitwa …………………………. Muunganiko wa silabi na silabi huunda …………………………………… Meza, dada, shule, kilimo huitwa ………………………………………….. Baba na mama ni marafiki huitwa …………………………………… Neno MCHWA lina konsonanti ngapi? ……………………………….. Neno CHOROKO lina aina ngapi za irabu? Neno MTOTO lina aina ngapi za konsonanti? Herufi zipi ambazo hapo katika kamusi ya Kiswahili? Konsonanti inayoundwa na mofu mbili huitwa …………………….. Irabu pia huitwa …………………………… Kisawe cha alfabeti ni ……………………… Andika idadi ya konsonanti katika maneno yafuatayo (i)Kinywa (ii) Skrubu (iii)Staftahi (iv) Mchwa (v) Muktadha (vi) Gharama (vii) Shule (viii) Nyanya (ix) Mbarika (x) Ngariba (xi) Chovya (xii) Fyeka (xii) Mwanhuzi (xiii) Dhanio (xiv) Thamani (xv) Dhamana (xvi) Ng’ombe (xvii) Tembo (xviii)Mfwangavo (xix) Kyabakari (xx) Khamisi

70

13 ULEMAVU WA BINADAMU 13.1. Dhana ya ulemavu a) Ulemavu ni hali ya kuwa na hitilafu au kasoro katika kiungo cha mwili. Pia huitwa ulema b) Mlemavu ni mtu ambaye ana matatizo au hitilafu katika viungo vya mwili wake c) Kumbuka kuwa si vizuri kuwacheka vilema kwa vyovyote vile kwani hujafa hujaumbika, huwezi jua ya kesho. Kila mtu ni mlemavu mtarajiwa 13.2. Jedwali la ulema Na Mlema Maelezo 1 Albino Mlemavu wa ngozi 2 Bubu Hawezi kuongea 3 Buge Hana kidole au vidole vya mguu au mkono 4 Chongo Hana jicho moja 5 Kengeza Mboni ya jicho lake imeelekea upandeupande 6 Kibogoyo Hana meno 7 Kigego Aliyezaliwa akiwa na meno au aliyeanza kuota meno ya juu kabla ya chini 8 Kikono Mlemavu wa mkono 9 Kikwekwe Mtu mfupi mno

10 11

Kipofu Kipooza

12 13 14 15 16 17 18 19

Kishingo Kitange Kiwete Kiziwi Masito Ndondo Ngwagu Nunge

20

Papachi

21

Toinyo

Haoni kabisa Mlemavu wa neva za fahamu (sehemu ya mwili wake imepooza, hapati hisia) Shingo yake imepinda Mlemavu wa mdomo (umepasuka) Mlemavu wa miguu yote Hasikii kabisa Hasikii vizuri (anasikia kwa shida) Mlemavu wa akili Mwathirika wa mihadarati Ana gutu ya vidole kwa sababu ya ukoma Meno yake yamepandiana au yamebebana Hana pua

71

Kisawe Zeruzeru Bubwi Kigutu Gere

Mhangi

Kibwiko Mbilikimo, kikwikwi, kidunavi, kibete, kishubuti, kidurango, kisaka

Mdomo sungura Kilema Kiduko, duko Kiruu, punguani, mzuzu Teja Mkoma Ngerekanya

22 23 24 25 26 27 28 29 30

Kibunye Kibyongo Kiguru Kipara Kithembe Kigugumizi Matege Dadawi Matungamavi

31

Chuji

Aliyekatika sikio Aliye na nundu mgongoni Aliyelemaa mguu mmoja Asiye na nywele Anayeongea kwa ncha ya ulimi Anayeongea kwa kusitasita Miguu kupinda kwa nje au kwa ndani Mtu mwenye kigugumizi/kitanga Miguu imepinda kuelekea ndani na kusababisha magoti kugusana Mtu asyeona vizuri

Kibiongo, kijongo Kinyonyoke

Mgegezi, mgugumi

ZOEZI LA 22 1. Andika visawe vya maneno yafuatayo i) Buda ii) Mhangi iii) Kipara iv) Papachi v) Kiziwi vi) Kitange vii) Buge viii) Albino ix) Kibiongo x) Kiwete 2. Andika jina la mtu mwenye ulemavu tajwa hapo chini (i) Asiye na macho (ii) Asiye ongea (iii) Mwenye jicho moja (iv)Asiye na meno (v) Asiye na pua (vi)Asiye na masikio (vii) Asiye na miguuu (viii) Asiye na mikono (ix)Asiyesikia kabisa (x) Anayesikia kwa shida 3. Mtoto wa kwanza kutahiriwa miongoni watoto waliopelekwa jando huitwaje? (chando, chalo, chudere) 4. Kitata ni nini? 5. Mtu asiyeona vizuri huitwaje?

72

14 AKISAMI, MAJIRA YA MWAKA NA MISAMIATI YA MALIPO 14.1. Akisami Akisami ni sehemu ya kitu, umbo au tarakimu kama vile robo, nusu, theluthi, n.k Chunguza jedwali hili Na Akisami Maelezo 1 ½ Moja ya mbili 1 2 /3 Moja ya tatu 3 ¼ Moja ya nne 1 4 /5 Moja ya tano 1 5 /6 Moja ya sita 1 6 /7 Moja ya saba 1 7 /8 Moja ya nane 1 8 /9 Moja ya tisa 1 9 /10 Moja ya kumi

Jina Nusu Theluthi Robo Humusi Sudusi Subui Thumni Tusui Ushuri

14.2. Majira manne ya mwaka Majira ni nini? Majira ni msimu fulani kulingana na hali ya hewa. Kisawe cha majira ni msimu Yafuatayo ni majira manne ya mwaka hapa kwetu Na Msimu Maelezo 1 Kiangazi Majira ya jua kali 2 Masika Majira ya mvua nyingi 3 Kipupwe Majira ya baridi kali 4 Vuli Majira ya mvua za rasharasha

Tanzania Kisawe Kifuku Mawaga/manyunyu/manyonyota

14.3. Misamiati ya Malipo mbalimbali Malipo ni gharama aghalabu ya fedha anayoitoa mtu anapohitaji huduma au kununua kitu. Aidha, malipo ni kitu chochote anachopewa mtu baada ya kufanya kazi fulani. Pia huitwa mshahara Chunguza jedwali hili Na Malipo Maelezo Kisawe 1 Mahari Mali anayotoa mwanamume na kuwapa Pamvu wazazi wa mwanamke anayetarajia kumwoa 2 Kodi Fedha inayotolewa kwa ajili ya nyumba Ada, ushuru iliyopangwa au kitu kilichoazimwa ili kutumiwa

73

3

Deni

4

Masurufu

5

Marupurupu

6

Posho

7

Mshahara

8

Pensheni

9 10

Kiinua mgongo Fungule

11

Fidia

12

Ushuru

13

Kiingilio

14

Karo

15

Utotole

16 17

Fola Koto

kwa muda Au ni fedha inayotozwa na serikali kutoka kwenye mshahara wa mtu, pato la biashara Madai ya kitu kilichokopwa kwa makubaliano ya kukirejesha baadaye Fedha au huduma nyingine anayopewa mfanyakazi aghalabu na ofisi yake kwa ajili ya kumwezesha kukidhi mahitaji yake anapokuwa safarini Kiasi cha fedha anachopata mfanyakazi nje ya mshahara wake wa kawaida kwa ajili ya kukidhi mahitaji kama vile nyumba, usafiri, umeme na maji Malipo nje ya mshahara anayolipwa mtu baada ya kufanya kazi maalumu aghalabu ya kitaalamu Ujira anaolipwa mtu na mwajiri wake kila baada ya kipindi fulani kwa kazi aliyoitumikia Malipo yanayotolewa kwa kipindi maalumu kwa mtu aliyestaafu kutokana na mfuko wa uwekezaji ambao mtu huyo pamoja na mwajiri wake walikuwa wanachangia wakati wa ufanyaji kazi wake Malipo anayopewa mwajiriwa mwishoni mwa kipindi cha ajira yake Asante apewayo mganga wa kienyeji baada ya kuhitimisha uganga wake Malipo yanayofanywa baada ya kusababisha hasara, usumbufu au maumivu fulani kwa mtu Kiasi cha fedha au ada inayotozwa na serikali kwa bidhaa zinazoingizwa au kusafirishwa nje ya nchi Malipo kwa ajili ya kuingia katika shughuli ya burudani kama vile mchezo, mziki au kujiandikisha katika chama Malipo ya fedha yanayotolewa na mwanafunzi kama gharama za masomo Zawadi ambayo mtu hupewa baada ya kufanikiwa kukiona kitu kilichokuwa kikitafutwa baada ya kupotea Malipo ya kumshika mtoto mchanga Karo alipayo mzazi kwa mhadhiri wakati mwanaye anapodahiliwa chuoni

74

Mkopo, mkugo, karadha

Masurufu

Ijara, janguo,posho Mafao

Bahashishi, bonsai, tunzo, dafina, zawadi Kifunguamkoba, kiingiaporini, kanda

Kodi

Karo, ada

Ada Kiangazamacho

Ada

18

Hongo

Fedha au kitu cha thamani anachotoa mtu ili apate huduma asiyostahili

19

Fichuo

20

Dhamana

21

Kishika mkono

Tunu aitoayo bwana harusi ili amuone bibi harusi kwa mara ya kwanza Au ni tuzo apewayo mvulana au msichana baada ya kufundwa Fedha au mali ambayo hutolewa ili kumwezesha mtu kupata mkopo au huduma fulani au kumwezesha mtu anayeshitakiwa kuachiliwa kwa muda Zawadi anayotoa bwana harusi kwa bibi harusi mara baada ya kufungishwa ndoa Au ni fedha zinazotolewa kama kitangulizi unapotaka kununua kitu

Rushwa, mrungura, chai, chauchau, chichili, kadhongo, kiinikizo Zawadi

ZOEZI LA 23 1. Ili kuokoa nchi kutokana na ufisadi si budi kila mmoja wetu akatae ………….. 2. Mashala alipoenda kwa sangoma alitoa ……………………. kama ada ya kumuona 3. Mwalimu Mipawa akistaafu atapewa ………………………………… 4. Makoye alifurumushwa nyumba ile kwa sababu hakuwa amelipa ………………….. 5. Ni vigumu kwa mwanafunzi kutoka familia masikini kulipa …………………….. 6. Ili uingie kwenye ukumbi was enema yakupasa ulipe ……………………… 7. Atakayegundua dawa ya ukimwi atalipwa …………………….. 8. Wafanyakazi wa umma hulipwa ……………………. kila mwisho wa mwezi 9. Bidhaa yoyote inapoingizwa nchini ni lazima ilipiwe ………………………. 10. Ngika alipotoka jandoni alipewa ………………………… 11. Japo alivunjiwa nyumba yake hakudai …………………. yoyote 12. Kama Isa asingwekewa ………………… na Musa angeeydelea kuwa korokoroni 13. Rais alisisitiza kuwa kila mtu anapaswa kulipa ……… ili nchi ijenge uchumi wake 14. …………………….. inanunua utu wa mwanamke 15. Mwalimu Juma alipewa ………………………….. aliposafiri kikazi Mwanza 16. Siku hizi wanafunzi hawalipi ……………………… shuleni kwani elimu ni bure 17. Mkataba wangu wa ajira ukifika ukomo nitapewa …………………… 18. Walimu wanaosimamia mitihihani ya taifa hulipwa ………………….. zao mapema 19. Elezea majira manne ya mwaka 20. Moja ya tatu ya kitu kizima huitwaje kwa jina moja?

75

NYONGEZA I.

USHAIRI

Ushairi ni nini? - Ushairi ni utungo wa kisanaa unaotumia lugha teule na mpangilio maalumu wa maneno badala ya kutumia lugha nathari. Aidha ushairi ni sanaa ya utunzi wa mashairi, tenzi na ngonjera. - Kwa hiyo ushairi ni tanzu ya fasihi yenye vipera vitatu ambavyo ni Mashairi,

Ngonjera na Tenzi SHAIRI Shairi ni utungo unaotumia mapigo ya silabi kwa utaratibu maalumu wa kimuziki kwa kutumia lugha teule (mkato, picha na tamathali za semi). Aidha, shairi ni utungo wa kisanaa wenye mpangilio maalumu wa beti, vina na mizani Mfano;

Vita usije hamahaki, Makonda kusimamia, Vijana wakosa haki, unga kuubwia, Ni vibaya kuhamaki, pasi na kufikiria, Taifa lateketea, Makonda we mbele songa. Aliyeanza Nyerere, ukoloni kuondoa, Mwinyi Mkapa Mkwere, Magufuli hana doa, Wasikuchezee shere, bangi viroba ondoa, Kaka Makonda shujaa, kikuli si kitu kwako Maana ya baadhi ya istilahi za kishairi (1) Maghani ni mashairi yanayoghanwa (2) Mghani ni mtaalamu wa kughani mashairi (3) Malenga ni mtunzi na mwandishi wa mashairi (4) Shaha ni mwalimu wa malenga (5) Mutribu ni msanii wa taarabu (6) Manju ni mtaalamu wa kutunga na kuimba nyimbo katika ngoma (7) Sherasi ni kiongozi wa kikundi cha ngoma (8) Ngoi ni mtu mwenye ustadi wa kuongoza katika uimbaji nyimbo (9) Sogora ni mtaalamu wa kupiga ngoma (10) Diwani ni kitabu cha mashairi (11) Urari ni ulinganifu wa silabi (mizani) katika mshororo wa shairi (12) Muwala ni uwiano uliopo baina ya vipengele vya fani na maudhui katika ushairi

76

Aina za mashairi Kuna aina kuu mbili za mashairi kwa ujumla

1. Mashairi ya Kimapokeo Haya ni mashairi yanayozingatia kanuni za muwala na urari wa mizani, vina na mishororo katika ubeti wa shairi. Pia huitwa mashairi ya kizamani au mashairi funge

2. Mashairi ya Kimamboleo Haya ni mashairi yasiyozingatia kanuni za muwala na urari . Mashairi haya pia huitwa

mashairi huru, mashairi ghuni, mapingiti au masivina Sifa za Shairi 1. Huwa na vina, mizani, mishororo na beti 2. Hutumia lugha teule 3. Hufupisha au kurefusha maneno ili kutosheleza idadi ya mizani 4. Hayazingatii kanuni za kisarufi 5. Hutumia mbinu za lugha

Vipengele muhimu vya shairi 1. Mizani Mizani ni ulinganifu wa idadi ya silabi katika kila kipande au mstari wa shairi. Aghalabu mashairi ya kimapokeo huwa na mizani 8 kwa kila kipande na mizani 16 kwa kila mstari Mfano; Ka-zi zo-te du-ni-a-ni, na mba -wa-ni m-ku-li-ma,= 16 A-na-pi-ta ki-la fa-ni, ha-ta ka-ma ha-ku-so-ma, =16 Ku-la ha-e-ndi so-ko-ni, a-u ku-o-mba kwa Ju-ma, =16 Zu-ngu-ka du-ni-a nzi-ma, ka-zi bo-ra ni ki-li-mo. =16

2. Vina Vina ni silabi zenye sauti ya namna moja zinazotokea katikati au mwishoni wa kila mshororo wa ubeti. Kuna vina vya kati (vya ndani) na vya mwisho (vya nje) Mfano; Kilimo ni mkombozi, kinga ya umasikini, Humpa mtu makazi, mavazi na burudani, Pato lake si la mwezi, posho haikosi ndani, Zunguka dunia nzima, kazi bora ni kilimo

77

3. Ubeti Ubeti ni fungu la mistari kadhaa aghalabu minne lenye maana kamili. Mfano; Kilimo ni mkombozi, kinga ya umasikini, Humpa mtu makazi, mavazi na burudani, Pato lake si la mwezi, posho haikosi ndani, Zunguka dunia nzima, kazi bora ni kilimo

Ubeti

4. Kituo Kituo ni mstari wa mwisho katika kila ubeti wa shairi ambao huonesha msisitizo wa ubeti mzima au shairi zima. Majina mengine ya kituo cha shairi ni kibwagizo, mkarara, kiitikio, korasi, bahari,

kitoshelezi, kimalizio, mfuniko, uradidi, takriri, kitembo, kipokeo, nk Mfano; Orodhesha toka pwani, hadi mikoa ya bara, Shughuli za ofisini, na za kufunga minara, Weka katika medani, kilimo hushinda kura,

Zunguka dunia nzima, kazi bora ni kilimo = kituo 5. Mshororo ni mstari mmoja wa ubeti. Kila mshororo wa ubeti wa shairi la tarbia una jina lake kama inavyoonekana katika mfano hapo chini Mfano; Orodhesha toka pwani, hadi mikoa ya bara,=mwanzo Shughuli za ofisini, na za kufunga minara, = mloto Weka katika medani, kilimo hushinda kura, = mleo

Zunguka dunia nzima, kazi bora ni kilimo = kituo Aidha ♣ ♣ ♣

kila mstari au mshororo una vipande viwili; ukwapi na utao Kipande ni nusu mstari, aghalabu huwa na mizani nane Ukwapi ni kipande cha kwanza (kushoto) katika mshororo Utao ni kipande cha pili (kulia) katika mshororo

Mfano; Kilimo ni mkombozi, /kinga ya umasikini, Ukwapi Utao (mizani 8) (mizani 8)

78

Aina za Vituo vya shairi Kuna aina kuu tatu (3) za Vituo 1. Kituo bahari Kituo bahari ni kituo kisichobadilika mwanzo hadi mwisho wa shairi. Mfano;

Ungeyatoa machozi, kuliko kutabasamu, Unadhani ni azizi, kuweka kando elimu? Kijana wacha ubozi, usomesome kwa hamu, Maisha huwa magumu, kukaa bila elimu. Henezi utamaizi, nikwambiayo ghulamu, Leo ndiyo upuuzi, kuna siku ni muhimu, Umefanya uamuzi, mwisho utajilaumu, Maisha huwa magumu kukaa bila elimu 2. Kituo kimalizio au kituo kiishio Kituo kimalizio ni kituo kinachobadilika katika kila ubeti, yaani kinabadilika kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho Mfano;

Tulopeleka bungeni, wamegeuka nyang’au Mafisadi kama nini, baradhuli mabahau Wameuvunja mpini, konde wamelisahau, Zamani na siku hizi, mambo sivyo yavyokuwa. Mwalimu mwana elimu, asiyekujua ni nani? Kwake ilete elimu, liyopewa na manani, Watu wote wafahamu, haipingiki hasilani, Adharauye mwalimu, kapungua akilini 3. Kituo nusu Kituo Nusu ambacho nusu ya maneno yake hubadilika na nusu hubaki yale yale kutoka ubeti wa kwanza hadi ubeti wa mwisho Mfano;

Baragumu napuliza, lipo jambo linakera, Nyote mnasikiliza, wazee na makapera, Kwa makini sikiliza, hali hii siyo bora, Jambo lenyewe ugonjwa, UKIMWI hasa ni kifo

79

Dunia yatikisika, ugonjwa umeingia, Tena wavuka mipaka, Ulaya hata Asia, Huu UKIMWI hakika, tiba haujasikia, Ndugu zangu jihadhari, UKIMWI hasa ni kifo Mitindo anuwai ya mashairi Uainishaji wa mitindo ya mashairi unategemea zaidi idadi ya mishororo

Chunguza jedwali hili Idadi ya mishororo 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10

Jina Tamonitha Tathnia Tathlitha Tarbia Takhmisa Tasdisa Sabilia Tathmina Utisa Ukumi

ZOEZI LA 24 1. Utungo wa kisanaa unaotumia lugha teule na mpangilio maalumu wa maneno huitwaje? 2. Taja tanzu tatu za ushairi 3. Eleza maana za istilahi zifuatazo: (i) Mghani (ii) Malenga (iii) Mutribu (iv) Diwani (v) Manju 4. Elezea vipengele vikuu vitano vya shairi 5. Shairi lenye mishororo minne katika kila ubeti huitwaje? 6. Jumla ya silabi katika mshororo mmoja wa shairi huitwaje? 7. Silabi zinazofanana katikati na mwishoni mwa kila mshororo wa shairi huitwaje? 8. Ili kupata idadi ya mizani katika mshororo wa shairi tunahesabu nini? 9. Nusu mshororo wa shairi huitwaje? 10. Aghalabu kila kipande cha mshororo wa shairi huwa na mizani ngapi? 11. Kipande cha kwanza cha mshororo wa shairi huitwa ……………………………… na kile cha pili huitwa …………………….. 12. Mstari wa mwisho katika kila ubeti wa shairi huitwaje?

80

13. Taja aina tatu za vituo vya shairi 14. Andika majina ya kila mshororo wa shairi tarbia 15. Andika majina mengine kumi ya kituo cha shairi 16. Kwa kawaida, kichwa cha shairi hupatikana katika mstari ujulikanao kwa jina gani? 17. Andika majina ya mashairi haya kulingana na idadi ya mistari yake (vi) 3 (vii) 4 (viii) 5 18. Soma shairi hili kisha jibu maswali yafuatayo Kazi zote duniani, namba wani mkulima, Anapita kila fani, hata kama hakusoma, Kula haendi sokoni, au kuomba kwa Juma, Zunguka dunia nzima, kazi bora ni kilimo. Kilimo ni mkombozi, kinga ya umasikini, Humpa mtu makazi, mavazi na burudani, Pato lake si la mwezi, posho haikosi ndani, Zunguka dunia nzima, kazi bora ni kilimo Orodhesha toka pwani, hadi mikoa ya bara, Shughuli za ofisini, na za kufunga minara, Weka katika medani, kilimo hushinda kura, Zunguka dunia nzima, kazi bora ni kilimo Maswali: (i) Shairi hili lina beti ngapi? (ii) Andika vina vya kati na vya mwisho vya ubeti wa mwisho wa shairi hili (iii) Kila mshororo wa shairi una mizani ngapi? (iv)Shairi hili lina mishororo mingapi? (v) Nakili kituo cha shairi hili (vi)Kituo cha shairi hili ni cha aina gani? (vii) Kichwa kinachofaa kwa shairi hili ni kipi? (viii) Nakili utao wa mshororo wa kwanza wa ubeti wa pili wa shairi hili (ix)Kipande kimoja cha shairi hii kina mizani ngapi? (x) Shairi hili ni la aina gani kulingana na idadi ya mishororo?

81

UTENZI Utenzi ni utungo mrefu wa ushairi unaoelezea juu ya tukio fulani. Mfano;

Leo nataka binti, Ukae juu ya kiti, Ili uandike hati, Ndogo ya waja. Mimi kwako ni baba, Hati hii ya huba, Andika iwe haiba, Asaa itakufa

Sifa za Utenzi - Huwa na mistari minne - Huwa na mizani nane - Huwa na vina bahari (vinavyofanana) - Mstari wa mwisho wa kila ubeti huitwa bahari Vipengele muhimu vya utenzi - Vina - Mizani - Ubeti - Mishororo/mistari - Bahari Kumbuka kuwa misingi ya utenzi ni sawa kabisa na ile ya mashairi, isipokuwa;- Utenzi hauna vina vya kati kwenye mstari au mshororo - Huwa na mizani nane

82

ZOEZI LA 25 Soma utenzi ufuatao kisha jibu maswali kuuhusu

1. Tunaye paka nyumbani, Hachoki kukaa ndani, Analala sebuleni, Mchana hadi jioni 2. Nyama mtupieni chini, Utadhani haioni, Hapeleki mdomoni, Kiwekwacho sakafuni 3. Uchafu hana machoni, Wala upele mwilini, Mwangalie kifuani, Anapendeza machoni. 4. Hutamwona bafuni, Wala kule kisimani, Mate yake mdomoni, Hujisafisha mwilini. 5. Hana haja na sabuni, Ya kunawa miguuni, Wala mafuta laini, Ya kupakaa usoni 6. Haendi haja chooni, Wala pale sebuleni, Kinyesiche hukioni, Hukifukia shimoni 7. Ana mengi akilini, Hakufundishwa shuleni, Akienda mawindoni, Utafurahi moyoni. 8. Panya akija nyumbani, Wakikutana uani, Huyo yuko hatarini, Hauwezi ushindani.

83

9. Nyoka atambaa chini, Paka yeye ni makini, Ataruka kichwani, Na kwenda naye hewani. 10. Atapombwaga chini, Nyoka hana tumaini, Daima ni mshindani, Paka wetu wa nyumbani Maswali 1. Utenzi huu una beti ngapi? 2. Kila ubeti una mistari mingapi? 3. Kila mstari una mizani ngapi? 4. Andika vina vya utenzi huu 5. Paka anayezungumziwa katika utenzi huu hushinda wapi? 6. Kutokana na utenzi, paka hutumia nini kujisafisha? 7. Paka wa utenzi huu haonji chakula gani? 8. Paka akitaka kujisaidia hufanya nini? 9. Kichwa kinachofaa kwa utenzi huu ni kipi? 10. Mshairi ametumia neno “kinyesiche”, nini kirefu cha neno hili?

NGONJERA Ngonjera ni aina ya mashairi ya majibizano baina ya pande mbili au watu wawili au zaidi. Aghalabu katika mazungumzo hayo huwa mna mijadala ya malumbano yenye shabaha ya kutoa ujumbe maalumu kwa hadhira. Tofauti yake na shairi la kawaida ni kwamba, ngonjera inatambwa na watu wawili au makundi mawili ambapo ubeti wa kwanza huibua hoja na ule wa pili hujibu hoja. Malumbano hayo ya hoja huendelea vivyo hivyo hata mwafaka kupatikana. Mfano:

Mwalimu: Hilo si maalumu, kuokoa maishani, Tena unajidhulumu, waingia kufuruni, Hiyo kazi ya Karimu, ndiye mwenye nusurani, Kazi njema ya walimu, kutoa watu gizani. Daktari: Daktari ni muhimu, kukutoa ujingani, Mtu amekula sumu, maisha ya hatarini, Budi atajilazimu, afike kwangu nyumbani, Daktari ni muhimu, kwa kuokoa maisha.

84

Mwalimu: Asili ya binadamu, yatokana na manani, Narudi kutakalamu, nililosema mwanzoni, Asipopenda Karimu, bidiizo zifaeni? Kazi njema ya walimu, kutoa watu gizani. Daktari: Hilo nalifahamu, silipingi abadani, Amri ni ya Karimu, najua toka zamani, Japo mtu hana damu, asubiri kwa Manani, Daktari ni muhimu, kwa kuokoa maisha. Mwalimu: Kidogo natabasamu, na kicheko mdomoni, Wa tele wendawazimu, moja ni wewe fulani, Hivyo wale marehemu, hawakwenda ugangani? Kazi njema ya walimu, kutoa watu gizani. Daktari: Hilo mimi sikubali, nitafanya ushindani, Bora kuomba Jalali, si lazima ugangani. Unapopata ajali, mbona hukai nyumbani? Daktari ni muhimu, kwa kuokoa maisha. Mwalimu: Hayo yako sikubali, na wala siyaamini, Tokea enzi azali, hako Daktari nchini, Watu hupata thakili, hutibiwa majumbani, Kazi njema ya walimu, kutoa watu gizani. Sifa za ngonjera 1. Ni dayalojia, yaani majibizano baina ya pande mbili 2. Huwa na vipengele vyote vya shairi; beti, vina, mizani na idadi ya mishororo 3. Kituo huweza kufanana (aina za vituo)

Muundo wa Ngonjera Muundo wa ngonjera ni sawa kabisa na muundo wa mashairi ya kawaida. Kwa hiyo vipengele vya ngonjera ni vile vile vya shairi, ambavyo ni ubeti, mizani, vina, mishororo na kituo. Aidha mitindo ya ngonjera ni sawa na ile ya mashairi

85

ZOEZI LA 26 Tamba ngonjera ifuatayo kisha jibu maswali kuihusu

1. Leo kanijia jumbe, ujumbe wake kusema, Kwangu mimi Mwanalimbe, msifika wa kulima, Ati huyu Mwanafumbe, aenda shule kusoma, Chembe ipi ya faida, kwa msichana kusoma 2. Uko ulimwengu gani, msifika wa kulima? Wataraji niamini, usemalo la hekima? Ati faida huoni, ya msichana kusoma? Yapo mengi ya faida, kwa msichana kusoma. 3. Mtoto una hekima, kunijuza nilotaka, Ila bado hujasema, sikio nikazibuka, Maneno umeyauma, niambie ya uhakika, Chembe ipi ya faida, kwa msichana kusoma? 4. Kwanza kufuta ujinga, wa kutojua kusoma, Na herufi utaunga, neno lake mtasoma, Namba hazitamchenga, hawezi lipwa dhuluma, Yapo mengi ya faida, kwa msichana kusoma Maswali 1. Ngonjera hii ina beti ngapi? 2. Andika vina vya ndani na vya nje vya ubeti wa mwisho wa ngonjera hii 3. Jumla ya mistari minne katika ngonjera hii huitwaje? 4. Mstari mmoja wa ubeti wa ngonjera hii una mizani ngapi? 5. Kichwa kinachofaa kwa ajili ya ngonjera hii ni kipi? 6. Funzo gani unalipata kutokana na ngonjera hii? 7. Taja sifa inayotofautisha ngonjera na shairi funge 8. Mwanalimbe anasema, “Maneno umeyameza” Anamaanisha nini? 9. Andika kisawe cha neno dhuluma kama lilivyotumika katika ubeti wa nne 10. Taja stadi tatu ambazo msichana atazipata kwa kwenda shule Andika tofauti ya maneno haya 1. Nyakanga na shaha 2. Kungwi na ngariba 3. Ngoi na sherasi 4. Sogora na mutribu 5. Manju na malenga

86

Na 1 2 3

II. VYAKULA ANUWAI (a) Aina za milo kulingana na muda Muda Jina la mlo Asubuhi Staftahi, kiamshakinywa, kifunguakinywa, kisebeho, kisabeho Mchana Chamcha Usiku Chajio

6 7 8 9 10

(b) Aina za vyakula kimapishi Aina ya chakula Maelezo Gagazi Samaki wa kuchoma Paya Supu ya miguu ya mbuzi Kongoro Supu ya miguu ya ng’ombe Chachandu Supu ya pweza Saladi Mchanganyiko wa mbogamboga na matunda unaoliwa bila kupikwa Mseto Mchanganyiko wa nafaka anuwai Mchanyato Mchanganyiko wa muhugo, ndizi na viazi Kimboya Mchanyato wa muhogo na kunde, choroko au maharage Hangale Ndizi za kukausha; kologwe Ndovi Ndizi zilizopikwa; izu

Na 1

III. ETIMOLOJIA YA BAADHI YA MANENO YA KISWAHILI MANENO ASILI/ETIMOLOJIA Shamba, divai Kifaransa

2

Laki, bima, gati, duka, korija

Kihindi

3

Bandari, kodi, pilau, dirisha

Kiajemi

4

Shule, hela

Kijerumani

5

Meza, nanasi, bendera, pera, viazi, karanga, muhogo, mahindi, papai, pesa, jeneza, gereza, mvinyo, leso, sukari

Kireno

6

Ripoti, shati, picha, beseni, trekta, waya, namba

Kiingereza

7

Rehema, wakili, shukrani, dhaifu, salamu, sharubati, sharafa, sharti

Kiarabu

Na 1 2 3 4 5

87

IV. Na 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18

Kiungo Jicho Mdomo Uso Ulimi Kidakatonge Uchengele Kiganja Kidole Mkono Kiwiko Bega Kifua Titi Tumbo Goti Paja Makalio Unyayo

VISAWE VYA BAADHI YA VIUNGO VYA MWILI Kisawe Ozi Kinywa Wajihi Lisami Kilimi, kimio Uchango Kitanga, kitengele Chanda Dhiraa Kivi Fuzi Kidari, sadiri Ziwa, tombo Uzao, undani Ondo Ango, koro, kiweo, kiga Matako Uwayo

88

Get in touch

Social

© Copyright 2013 - 2024 MYDOKUMENT.COM - All rights reserved.