Sheria ndogo za uratibu na usimamizi wa Wamachinga Flipbook PDF

Sheria ndogo za uratibu na usimamizi wa Wamachinga

29 downloads 119 Views 455KB Size

Recommend Stories


COMUNIDAD INDÍGENA U WA
COMUNIDAD INDÍGENA U’ WA En el territorio de Concepción están adscritas las comunidades de Aguablanca, localizada en las laderas que circulan la queb

WA, USA SECRETARÍA GENERAL
Conferencia Seattle, WA, USA SECRETARÍA GENERAL E-mail: [email protected] Secretaría General Antecedentes Impacts AL z z Confere

SONAX Podaci o proizvodima Proizvodi za vlasnike automobila Proizvodi i oprema za profesionalce Proizvodi za autopraonice
MADE IN GERMANY SONAX Podaci o proizvodima Proizvodi za vlasnike automobila Proizvodi i oprema za profesionalce Proizvodi za autopraonice Jahre GODI

PRECIOS ZA M2 MENUDEO
Hoja 1 ACTUALIZ: 20 de Julio 2015 LISTA DE PRECIOS PERIFERICO y BUSTAMANTE PERIFERICO TIPO MEDIDA PESO/P PZA/ ZA M2 PRECIOS MENUDEO VIGUETA Y

Story Transcript

TANGAZO LA SERIKALI NA ................... LA TAREHE .......................... SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA MIJI) (SURA YA 288) SHERIA NDOGO (Zimetungwa chini ya kifungu cha 62(1) (m) & 89) ---------------SHERIA NDOGO ZA (URATIBU NA USIMAMIZI WA WAMACHINGA) ZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA ZA MWAKA 2018 Jina na Mwanzo wa kuanza kutumika

1.

Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za (Uratibu na Usimamizi wa Machinga) za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala za Mwaka 2018 na zitaanza kutumika mara baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.

Matumizi

2.

Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote lilo chini ya Mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

3.

Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo:-

Tafsiri

“Afisa Muhidhiniwa” maana yake ni afisa yoyote wa Halmashauri au mtu yeyote atakayeteuliwa na Mkurugenzi kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi. “Afisa Mtendaji wa Kata” maana yake ni Afisa Mtendaji wa Kata iliyopo ndani ya eneo la Halmashauri. Afisa Mtendaji wa Mtaa” maana yake ni Afisa Mtendaji wa mtaa uliopo ndani ya Kata iliyopo katika Halmashauri. “Eneo la Wazi” maana yake ni eneo lolote la bustani, viwanja, barabara au kwenye hifadhi za barabara.

“Eneo la biashara” maana yake ni maeneo maalum ndani ya eneo la Halmashauri yaliyoainishwa na kutengwa mahususi kwa ajili ya kutumiwa na wafanyabiashara waliosajiliwa na kupewa kibali kufanyia biashara zao ndogondogo “ Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Manispaa ya Ilala “Kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashauri; “KAWAA” maana yake ni Kariakoo Wamachinga Association chama ambacho kinatambuliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala “Mtaa” maana yake ni eneo lolote lililopo ndani ya Halmashauri na inajumuisha maeneo yote ya barabara na hifadhi za barabara na njia ya waenda kwa miguu. “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. “Mkazi” maana yake ni mtu yeyote anayeishi na , au anayefanya shughuli yoyote ndani ya eneo la Halmashauri “machinga” maana yake ni Mfanyabiashara ndogondogo aliyesajiliwa kufanya biashara na kutambulika ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambaye anafanya biashara zake kwa njia ya kutembeza au kupanga katika maeneo maalumu yaliyoainishwa kwa shughuli za biashara. “Mfanyabiashara ndogondogo”maana yake ni mfanyabiashara yeyote au kikundi cha wafanyabiashara ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala aliyesajiliwa au kilichosajiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania inayotambuliwa kisheria na kuingizwa kwenye rejesta ya Halmashauri na inajumuisha wamachinga.

“Umbo la biashara” maana yake ni umbo maalum linalohamishika lililotengenezwa mahususi na kutambulika kwa kuzingatia viwango na vipimo vilivyowekwa na Halmashauri kwa ajili ya kuwekea na kurahisisha ufanyaji na upangaji wa biashara ndogondogo katika eneo la biashara. “Ushuru” maana yake ni tozo inayolipwa na mfanyabiashara ndogondogo au kutokana na kuuza au kununua bidhaa kwa lengo la biashara. “Vikundi” maana yake ni vikundi vya Ushirika, umoja wa vikundi vya wafanyabiashara vilivyosajiliwa kwa ajili ya kufanya bishara katika eneo la biashara “Wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, Kampuni au Shirika ambalo limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hizi.

Wajibu wa Halmashauri

4.

1

“Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa. Halmashauri itakuwa na jukumu la kutenga maeneo maalum ya wafanyabiashara ndogndogo kufanya biashara kulingana na aina ya biashara.

2

Halmashauri itakuwa na wajibu wa kusimamia shughuli za wafanyabiashara ndogondogo kwa utaratibu uliowekwa na Sheria Ndogo hizi.

3

Halmashauri kwa kushirikiana na wafanyabiashara itaratibu masuala ya ulinzi na usalama kwa kuzingatia Sheria ndogo (Ulinzi wa Umma) Halmashauri ya Manispaa ya Ilala za mwaka 2008 GN Na. 217 pamoja na marekebisho yake

4.

Kutoa Namba za Utambulisho kwa Wafanyabiashara Ndogondogo baada ya kusajiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania

Wajibu wa wafanyabiashara Ndogndogo

5 1

2 3 4 5

6

7

8

9 Msajili na Usajili wa Biashara Ndogondogo

6 1 2

3

Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutoza tozo au ushuru kwa kila mfanyabiashara ndogodogo kama ilivyoainishwa katika jedwali la pili la Sheria ndogo hizi Itakuwa wajibu wa kila mfanyabiashara Ndgondogo :kulipa tozo au ushuru wa kila siku wa kufanya biashara katika maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya biashara au mitaa anayotembeza biashara yake. kufanya usafi katika eneo na kuhifadhi taka hizo katika maeneo rasmi ya kutunza taka. kutojihusisha na vitendo vitakavyosababisha uvunjifu wa amani kujiunga katika kikundi kinachotambulika na kilichosajiliwa na Halmashauri Kutomzuia wakala au Afisa muidhiniwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ndogo hizi. Kufanya biashara katika maeneo yaliyotengwa na Halmashauri kwa mpangilio utakaowekwa kwa mujibu wa sheria ndogo hizi. Kutoa taarifa za kweli kuhusiana na biashara yake kwa Mamlaka na itakuwa ni kosa kwa mujibu wa Sheria ndogo hizi kutoa taarifa za uongo. Kuhakikisha anapata (umbo/ kasha) la kufanyia biashara. na kufanya biashara kkwenye umbo la biashara. Kusajili biashara yake na kufuata masharti ya Sheria Ndogo hizi Kutakuwa na Msajili wa Biashara ndogondogo ambaye atafanya kazi ya:kuratibu na kusimamia biashara ndgondogo Kutoa namba ya biashara ambao itaainisha eneo, mtaa na kibanda/ kasha au umbo la mfanyabiashara ndogondogo kuendesha shughuli zake . Kila usajili wa biashara ndogondogo utadumu kwa muda wa mwaka mmoja, baada ya hapo mfanyabiashara ndogondogo

atawajibika kuhuisha usajili wa biashara yake.

Vizimba/ Maeneo ya biashara.

7

Kibali cha biashara, ukomo wa 8 usajili na uhuishaji wa Kibali

4

Mfanyabiashara yeyote ambaye atachelewa kuhuisha usajili wa biashara yake atawajibika kulipa adhabu ya kuchelewa kusajili ambazo ni sawa na asilimia 50 ya gharama za ada, ushuru na kodi zikiwekwa pamoja.

5

Mmiliki wa eneo la biashara ndogondogo atakayeshindwa kuhuisha usajili wa biashara yake baada ya muda kuisha au asipokuwepo kwenye eneo lake la biashara kwa miezi sita atafutiwa usajili wake.

6

Ni marufuku kwa mfanyabiashara ndogondogo ambaye hajasajiliwa kufanya biashara katika eneo lolote la Halmashauri ikibanika ametenda kosa hilo atatozwa faini ya shilingi Elfu Hamsini.

1

Ni wajibu wa kila mfanyabiashara ndogondogo kusajiliwa yeye mwenyewe na eneo lake a biashara/kizimba katika Kata anayofanyia biashara ndogondogo.

2.

Ni marufuku kwa mfanyabiashara ndogongodo yeyote kufanya biashara ndogongodo katika eneo lolote la Halmashauri pasipo kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria ndogo hizi.

3.

Kila mfanyabiashara atawajibika kulipa ushuru ulizowekwa kwa mujibu wa sheria ndogo hizi. Bila kuathiri matakwa ya Leseni ya Biashara, Mfanya biashara Ndogondogo atawajibika kumba Kibali cha kufanya biashara ndogondgo ndani ya eneo la Halmashuri na kibali kitalipiwa ada kama ilivyoelekezwa katika jedwali la kwanza la sheria ndogo hizi na kitadumu kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe ya kutolewa kwake. s

1

2

3

Kufuta kibali

9

1

Kibali kilichotolewa kitatumiwa na muhusika kwa ajili ya biashara na muda ulioainishwa katika kibali husika na si vinginevyo. Kibali kitatolewa na Halmashauri baada ya kupokea maombi ya maandishi kutoka kwa mwombaji yakiainisha aina ya biashara na eneo linaloombwa kwa ajili ya biashara. Halmashauri inaweza kufuta kibali kilichotolewa chini ya Sheria Ndogo hizi endapo mwenye kibali hicho:a) Atakuwa na malimbikizo ya madeni ya kodi/ada au ushuru; b) Atakuwa amesimamisha shughuli zake kwa muda wa miezi mitatu bila ya taarifa na sababu za msingi. c) Atakuwa amekiuka masharti ya Sheria Ndogo hizi hata baada ya kuonywa; au d) Atawashawishi wafanyabiashara wengine kutofuata Sheria ndogo hizi, kusababisha uvunjaji wa amani au atashiriki katika vitendo vya wazi vya uvunjifu wa amani katika eneo lililotengwa kwa ajili ya biashara ndogondogo. e) Atakodisha au kumpatia mtu mwingine kibali/leseni yake ya biashara.

Saa za Kazi

10

(1)

(2)

Eneo la biashara litakuwa wazi siku zote za juma kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni; isipokuwa jumamosi ya kila mwisho wa mwezi ambayo ni siku ya usafi ambapo eneo la biashara litafunguliwa kuanzia saa 4.00 asubuhi. Bial kuathiri kifungu cha 10(1) Halmashauri inaweza kuruhusu baadhi ya maeneo biashara kufanyika zaidi ya muda uliyoainishwa hapo juu kulingana na mahitaji na mazingira yatakayojitokeza kwa wakati huo.

(3)

Udhibiti wa nidhamu

11

Halmashauri kwa kushirikiana na viongozi wa wafanyabiashara ndogondogo wanaweza kufunga maeneo ya biashara yaliyotengwa kwa ajili ya matengenezo au sababu nyingine yeyote ya dharura pale itakapoonekana inafaa ili mradi watoe taarifa kwa wafanyabiashara ndogondogo. Itakuwa ni marufuku kwa mtu au mfanyabiashara ndogondogo yeyote:a) Kubandika tangazo au kubandua tangazo lolote ndani ya eneo la biashara bila ya idhini ya Mkurugenzi. b) Kuweka bendera ya chama chochote cha siasa ndani ya eneo la biashara. c) Kufanya shughuli za kisiasa ndani ya eneo la biashara; d) Kuharibu miundombinu ya biashara iliyowekwa. e) Kutumia lugha ya matusi ndani ya eneo la biashara; f) Kufanya shughuli yoyote kwenye eneo ambalo haliruhusiwi au halijajengwa kama eneo la biashara; g) Kupangisha kizimba au eneo la biashara kwa mfanyabiashara ambaye hajasajiliwa au kupewa eneo husika; h) Kufanya biashara nje ya eneo la biasharana kizimba chake; i) Kutupa taka ovyo, kutiririsha maji machafu ndani ya eneo la biashara. j) Kuwasha moto maeneo yasiyohusika ndani ya eneo la biashara.

Usafi wa eneo la Biashara

12.

Ukusanyaji wa Ada na Ushuru.

13.

Huduma ya usafi, ulinzi, maji na umeme

14.

Kamati ya Wafanyabiashara katika eneo la biashara

15.

1

Kila mfanyabiashara anayefanya shughuli za biashara katika eneo la biashara atawajibika kuweka eneo lake katika hali ya usafi wakati wote.

2

Mkurugenzi au afisa Muidhiniwa kwa kushirikiana na viongozi wa wafanyabiashara ndogondogo watapanga siku, namna na muda maalum mara moja kwa mwezi kwa ajili ya kufanya usafi wa jumla katika eneo lote la biashara.

3

Kila mfanyabiashara katika eneo la biashara atatakiwa kushiriki katika usafi wa jumla wa eneo la biashara bila kukosa pamoja na kufuata kanuni za afya Halmashauri au wakala atatoza Ada au Ushuru kwa wafanyabiashara ndogondogo wafanyao biashara kwenye eneo la Halmashauri kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hizi. Kila mfanyabiashara katika eneo la biashara atawajibika kugharamia huduma ya ulinzi, usafi, Maji, na umeme kulingana na mahitaji yake kila mwezi kufuatana na utaratibu utakaowekwa na kamati ya wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la biashara.

1

Kutakuwa na Kamati ya Wafanyabiashara katika eneo la biashara ambayo itaundwa na Wafanyabiashara waliosajiliwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi ambao watafanya kazi katika kipindi cha mwaka mmoja.

2

Wajumbe wa Kamati ya Wafanyabiashara katika eneo la biashara watakuwa ni Mwenyekiti na Katibu kutoka kila kundi la wafanyabiashara wa aina ya biashara inayofanana waliosajiliwa kufanya biashara katika eneo la biashara.

3

Uchaguzi wa wajumbe wa kamati ya wafanyabishara katika eneo la biashara utazingatia misingi ya na demokrasia usawa wa kijinsia.

Mkutano wa wafanyabiashara ndogondogo pamoja na vikao vya kamati ya wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la biashara

16..

Kazi za Mkutano wa 17. wafanyabiashara ndogondogo pamoja na Kamati ya Wafanyabiashara ndogondogo

1

Kutakuwa na mkutano wa wafanyabiashara Ndogondogo katika eneo la biashara utakaofanyika mara moja katika kila robo ya mwaka ambapo afisa biashara wa Manispaa atakuwa katibu wa mkutano huo na mwenyekiti atachaguliwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya wafanyabiashara katika eneo la biashara.

2

Kamati ya wafanyabisahara ndogondogo inaweza kukutana na kufanya vikao kwa jinsi itakavyoona inafaa kila baada ya mkutano wa wafanyabishara kwa ajili ya kutekeleza yaliyoainishwa na kuazimiwa katika mkutano wa wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la biashara na katibu wa vikao vyote vya kamati ya wafanyabiashara atakuwa ni afisa biashara wa Manispaa.

1

Mkutano wa wafanyabiashara ndogondogo utafanya kazi zifuatazo;

a) Kuhakikisha biashara inayoendeshwa katika eneo la biashara imesajiliwa na kulipiwa ada, ushuru na kodi ya biashara. b) Kuboresha ustawi wa biashara katika eneo la biashara kwa kuanzisha ushirika imara miongoni mwa wafanyabishara c) Kuhakiki uwepo wa nidhamu katika shughuli zinazofanyika katika eneo la biashara. d) Kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa wafanyabishara katika eneo la biashara. e) Kukuza na kuendeleza mfumo wa biashara;na f) Kutekeleza

kazi

zingine

watakazoelekezwa na Mkurugenzi kulingana na Sheria Ndogo hizi. g) Kuhakikisha eneo lote la biashara linakuwa safi muda wote. 2

Makosa na adhabu

Uwezo wa Kufifilisha

18.

22.

1

2

Ili kutekeleza majukumu yake sawasawa kamati ya wafanyabiashara ngondogo inaweza kuunda kamati ndogo zifuatazo ambazo zitakuwa na wajumbe watano kila mojakutoka miongoni mwa wajumbe wa kamati ya wafanyabiashara: (a) Kamati ndogo ya miundo mbinu na usafi. (b) Kamati ndogo ya fedha, biashara na utawala; na (c) Kamati ndogo ya Ulinzi na Usalama. Mtu yeyote atakaye kwenda kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa, na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingi laki mbili (Tsh.200, 000/=) na isiyozidi shilingi milioni moja (1,000,000/=) au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote mbili kwa pamoja. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza faini mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria hizi, kiasi kisichopungua shilingi laki mbili (Tsh.200,000/=) na kisichozidi shilingi laki tano (500,000/=) iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoambatishwa kwenye Jedwali la tatu la Sheria Ndogo hizi, na atatakiwa kulipa Ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi. Mtu aliyefanya kosa kwa mujibu wa wa Sheria Ndogo hizi atakiri kosa hilo kwa kujaza fomu maalum na atapewa stakabadhi mara baada ya kulipa faini.

JEDWALI LA KWANZA KIBALI KUFANYA BIASHARA KWENYE ENEO LA BIASHARA

1. Jina la Mwombaji ……………………………………………………………….. 2. Anuani ya mwombaji …………………………………………………………… 3. Kibali cha …………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………… 4. Eneo ambalo kibali hicho kitatumika ……………………………………….. ………………………………………………………………………………………… 5. Namba ya Usajili ya Mfanyabiashara…………………………………………………………………… 6. Malipo ya Ada/ushuru Tshs…………………………………… Stakabadhi Na………………………………………. 7. Malipo ya Kodi ya biashara Tshs…………………………………………… Stakabadhi Na……………………………………….. 8. Muda wa Kibali ni kuanzia tarehe……………………hadi tarehe………… 9. Masharti ya kutumia kibali hicho…………………………………………….. a) ……………………………………………… b) ……………………………………………… c) ……………………………………………… d) ……………………………………………… e) ……………………………………………… 10. Imesajiliwa na: Jina ……………………………………… Saini…………………………………….. Mkuu wa Soko Tarehe …………………………………. Mhuri……………………………………

JEDWALI LA PILI

ADA, USHURU NA KODI YA BIASHARA KWA KILA BIASHARA INAYOFANYIKA KWENYE ENEO LA BIASHARA

Na

Aina ya biashara

Ushuru kwa mwezi

Ada kwa

Kodi ya

kwa kila biashara.

mwezi

Biashara kwa mwaka

JEDWALI LA TATU KUFIFILISHA KOSA

(Chini ya kifungu cha 22)

Mimi ………………………………………………wa S.L.P……………….……….. nakiri KWA HIYARI YANGU MWENYEWE mbele ya……………………………………..ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya ………………………………. kwamba mnamo tarehe……ya Mwezi….Mwaka………nilitenda kosa la kukiri masharti ya kifungu cha …………..cha Sheria Ndogo za (Ada na Ushuru) za Halmashauri ya Manispaa Ilala za mwaka 2018.

Kwa mamlaka aliyopewa na Mkurugenzi wa Halmashauri. Niko tayari kulipa kiasi cha Ada na Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini.

NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIYARI YANGU KWA KADIRI YA UFAHAMU WANGU

Leo tarehe……………..ya mwezi……………mwaka……………………

Jina……………………………..…………………………...Saini……………………........

Mbele ya: Jina……………………………..………………. Saini…………………………………….…........ Wadhifa…………………………………………

Nembo na Mhuri wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala umebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kwa kufuata Azimio lililopitishwa kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika mnamo tarehe …….. mwezi ………………..Mwaka 2018.

…………………………… JUMANNE K. SHAURI, MKURUGENZI WA MANISPAA HALMASHAURI YA MANISPAA ILALA …………………………… CHARLES KUYEKO MSTAHIKI MEYA, HALMASHAURI YA MANISPAA ILALA

NAKUBALI

…………………………… SULEIMAN JAFO (MB), WAZIRI OFISI YA RAIS TAMISEMI

DODOMA TAREHE .........../............./ 2018

Get in touch

Social

© Copyright 2013 - 2024 MYDOKUMENT.COM - All rights reserved.